kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
Maendeleo yetu yanafanywa na kuletwa na kodi zetu sote, Sio hisani tunayalipia na tunawalipa watu woote wanaoyaleta, hivyo ni mali yetu sote.
Namna bora ya kuyalinda na kuyaendeleza haya maendeleo yetu yanayopatikana kidogokogo lazima tuyaendeleze na kuyalinda katika kila awamu na kila chama kitakachoingia madarakani, kama tumeamua tujenge reli hadi Congo lazima reli ifike Congo bila kujali ni nani yuko au chama gani kiko madarakani.
Kama tusipokuwa na katiba inayolinda mali na rasilimali zetu basi inawezekana kukatokea chama au kiongozi atakayekatalia madarakani milele kwa hofu na sababu za kutaka kuyalinda mafanikio au kumalizia yale aliyoyanza ambayo hayajakamilika.
Hii itatuletea shida huko mbeleni kama tutakuwa na watu ambao wataachana na miradi iliyotumia kodi zetu na kuiona kuwa ni ya fulani au ya chama fulani, kama vile tulivyoutelekeza uandishi wa Katiba mpya iliyotafuna kodi zetu.
Katiba madhubuti ni muhimu sana.