Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
MAENEO AMBAYO WAISLAM WANAWAPIGA BAO WAKRISTO.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Watibeli tunazichukulia dini kama shule na vyuo ambavyo hupika wafuasi wao na kutengeneza imani kupitia mafundisho Yao. Watibeli tunajua dini zote lengo lake ni Maadili na sio zaidi ya hivyo. Watibeli tunajua Dini zote zinalenga kuwafanya Watu wawe na tabia njema.
Hata hivyo Mapokeo yaliyoingizwa kwenye sheria za dini ndio huzua mitafaruku baina ya Dini na Dini. Mila na desturi zilizoingizwa kwenye Dini ndio huzua utata mkubwa.
Silika na Hulka za binadamu zinafanana karibu Ulimwenguni kote. Ndio maana sheria nazo zinafanana Kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine. Sheria za usiye, usizini, usiibe, usiseme Uongo, heshimu wazazi wako, fanya kazi, na usitamani Mali ya jirani yako miongoni mwa Sheria zingine zipo karibu kila jamii. Lengo ni kuweka mahusiano baina ya MTU na MTU kuwa mazuri.
Hata hivyo yapo Mapokeo ambayo ndio hutofautisha dini na Dini nyingine. Mapokeo hayo hutokana na Mila na desturi ya waanzilishi wa dini husika.
Na leo Taikon nitaenda kueleza Kwa kifupi baadhi ya mambo(Mapokeo) yaliyopo kwenye Dini ya kiislam ambayo yameiacha mbali dini ya Kikristo.
Ni kama ifuatavyo;
1. Mahari (Mwanamke ndiye husema Mahari yake)
Sheria ya Mahari ni sheria za kimila, ni Mapokeo na hazihusiani na sheria za Mungu Kabisa. Mahari kwenye Biblia imeripotiwa mara kadhaa lakini sio kama amri, Ila ni Mapokeo ya wazee.
Kwenye Quran Mahari imetajwa, lakini pia ni Mapokeo. Ninapenda sheria ya Mahari Kwa mujibu wa Quran Kwa sababu imemgusa mlengwa mwenyewe(muolewaji), Mwanamke kwamba ndiye atamke kiwango cha Mahari anayotaka kuolewa nayo. Hii inamaanisha kuwa upendo wa mwanamke kama Mhusika Mkuu kwenye tukio hilo utamzingatia Mumewe mtarajiwa. Hapo Mwanamke ataangalia uwezo wa kijana na pia ataangalia uhitaji wake wa kuolewa. Hivyo automatically hakutakuwa na kizuizi cha ndoa Kufungwa ikiwa matukio yote yatawahusu walengwa Wawili yaani Muoaji na muolewaji.
Hii ni tofauti na Ukristo, Kwanza Ukristo umeacha ishu ya Mahari kuamuliwa kimila zaidi ilhali muda huohuo Ukristo unachukulia mambo ya Mila na utamaduni ni upagani(hapo tunaona contradiction). Upande wa Mila na tamaduni wanaoamua Mahari ni Wazazi na Wazee wa ukoo Jambo ambalo linaweza athiri mchakato wa Ndoa. Kwani wao sio Wahusika Wakuu Ila Wahusika Wasaidizi. Zingatia mhusika Mkuu anaweza kuendelea na Majukumu hata bila ya mhusika Msaidizi.
Sio ajabu ni rahisi Kwa kijana wa kiislam kuoa kwani ni maelewano yake na Mchumba wake. Tofauti na Vijana WA Kikristo ambao kwao kuna kizuizi cha Mahari kutamkiwa na wasiohusika na ndoa Yao Mpya.
2. MAZISHI
Suala la MAZISHI kwenye Quran limezingatia kanuni ya Jumla zenye misingi ya kiutu, kiuchumi, na kiafya.
Mapokeo yaliyoripotiwa kwenye Quran kuhusu mazishi yanalenga tabaka na hadhi zote za wanadamu.
Mtu akifa Watu walie na kuomboleza Kwa kufiwa na sio wapate msongo wa mawazo kuwaza Sanduku la maiti.
Waislam mtu akifa Mapokeo yanawataka wazike mapema zaidi kadiri itakavyowezekana.
Wakristo wao hawana hiyo Kanuni. Na hii imesababisha Misiba siku hizi ya Wakristo kuwa moja ya mambo mazito zaidi hasa ukizingatia Msiba haunaga taarifa.
Msiba WA kiislam utahitaji, Maiti, shimo la Kaburi, wazikaji na sheikhe au Ostadhi.
Msiba WA Kikristo utahitaji Maiti yenye nguo nadhifu, shimo la Kaburi, Sanduku, wazikaji na mchungaji au kiongozi wa dini, na chakula.
3. Usafi na Stara
Waislam kwenye ishu ya usafi wako mbali Mno. Uislam ni usafi ukisema hivyo Watu hawatakushangaa. Usafi wa mwili hasa unazingatiwa, mambo ya Rohini ni wewe na Mungu wako. Ila uislam unaanzia kwenye Mwili.
Wanawake wa kiislam hasa utawatofautisha pakubwa na Wanawake WA dini zingine kwenye mambo makubwa mawili. Usafi na Stara.
Dunia hii hakuna Watu wasafi na wenye stara kama Waislam.
Hata wawe Maskini vipi kama ni Waislam hasa ni lazima wawe wasafi.
Nenda chooni, nenda misikitini mwao, nenda majumbani mwao.
Dini Yao imewapa muongozo WA namna ya kuwa msafi.
Hii ni tofauti na Wakristo, mkristo hata kama ameshika dini Sana mpaka awe msafi ni kazi ngumu Mno.
Nenda mkoani, au maeneo yenye Wakristo wengi, ingia chooni, angalia uungwana kama utaukuta, usiende Kwa Watu wasomi au wenye vipato. Nenda Kwa Watu wakawaida. Fanya utafiti wako.
4. Heshima ya Wanawake Kwa wanaume
Waislam Wanawake suala la kuheshimu Waume zao lipo kivitendo zaidi sio Porojo za Wakristo. Wakristo wao husema Kwa mdomo lakini kivitendo ni waongo wakubwa ukiita Wanafiki wala hutokuwa umekosea.
Ni marufuku Mwanamke wa kiislam kusimama Mbele ya wanaume kuhutubia, hiyo ni heshima. Mwanamke hawezi kumuongoza mwanaume.
Lakini Ukristoni ni Jambo la kawaida kumkuta Mwanamke amesimama Mbele ya wanaume anahubiri na kuhutubia utadhani hakuna wanaume au wanaume wameisha.
Heshima zingine ni pamoja na kwenye Ndoa. Mitafaruku ya Ndoa za Kikristo hasa Wanawake wakiwa na mdomo zinatokana na kuwa Ukristo hauna sheria za ndoa lakini uislam unao.
Ukristo hutumia sheria za ndoa za Mila na desturi za jamii ambazo ni kosa kubwa kwani Jamii zipo nyingi na kila jamii ina Mila na desturi zake. Hii ni tofauti na Waislam wao wanatumia sheria z kiislam bila kujali unatoka jamii Gani. Uwe mmasai, more, Mzungu, mhindi au vyovyote. Ikiwa tuu ni Muislam na ndoa ilifungwa kiislam basi sheria zitakazofuatwa ni kiislam. Na moja ya sheria ni Mume kumuongoza Mkewe Kwa kila kitu, na kumheshimu. Hakuna cha matrilineal wala Patrilineal societies hapa.
5. Talaka na mgawanyo wa Mali
Kwenye uislam Talaka ni moja ya mambo yanayozungatiwa. Ni sehemu ya ibada ya kuzingatiwa Kwa uangalifu. Hii sio Mapokeo Bali ni sheria na amri ya Mungu mwenyewe(Allah).
Mgawanyo wa Mali upo Kwa mujibu wa sheria za kiislam na sio vinginevyo. Wakristo wao hawana Talaka Ila chaajabu Watu wanaachana kila Siku.
Wakristo wameachia Serikali na tamaduni kuamua mambo ya Waumini wao. Fikiria MTU ni Mkristo lakini ATI anaamuliwa na serikali kuhusu namna ya kugawana Mali na Mkewe. Hiyo serikali Fikiria labda inaongozwa na mpagani ambaye anaabudu mizimu. Hapa Waislam walikuwa Mbele ya Muda walipoamua kuwa mambo ya Ndoa yaamuliwe Kwa Sheria za kiislam ili kuepuka siku moja kuamuliwa na makafiri/wapagani n.k.
Mambo yapo mengi Kwa leo tuishie hapa.
Tujadili Kwa Hoja. Mihemko ya kijinga tuweke pembeni.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam