Maeneo gani ni mazuri kwa kuishi na familia hapa DsM

Maeneo gani ni mazuri kwa kuishi na familia hapa DsM

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2018
Posts
2,490
Reaction score
3,584
Habari wadau..!

Zamani wakati nipo chuo pale Mlimani nilikuwa naamini maeneo mazuri kwa kuishi DsM ni Sinza na Survey maana maeneo hayo yana totozi nzuri na bata za kufa mtu kwa kipindi hicho.

Hivyo nilijitahidi kila mwaka wa masomo lazima nipate chumba Survey au Sinza .

Ila sasa nina familia napata ugumu kuchagua sehemu ya kuishi na kulea familia,maana familia inahitaji maeneo yenye utulivu na penye huduma zote za jamii na pasiwe wachawi au vigagura na msongamano wa nyumba kama za huku kwetu Buza.

Hivi kwa hapa Dar ni maeneo gani yametulia kwa kuishi na kulea familia ,ambapo hautajutia kujenga au kununua nyumba ya kuishi maeneo hayo.
 
Maendeleo ya mtaa unaopanga si ya kujivunia, Bali maendeleo ya Mtaa wenye nyumba yako ama kiwanja chako.
Mimi binafsi sehemu ya kupanga, nazingatia iwe karibu ama rahisi, kufika kwenye shuguri zangu za kiuchumi.
Pendekezo lako ni maeneo gani,?maana kuna maeneo hayafai kwa malezi ya familia na utulivu sio ishu ya maendeleo tu.
 
Kinondoni, karibu na kwa tarimba pametulia, kinondoni kule kwa mengi apmerulia pia. Mi napenda kinondoni ni rahisi kwa kazini na shule kwa watoto. Sema sio ukakae kinondoni nyumba ya watu kumi nyumba yako mwenywe ndo naona ubora
 
Ubungo-Kibamba. Hiyo njia haina shida. kama hujaelewa ishi Mbagala utakuja kunielewa baada ya miaka 10 ijayo
Aanzie kimara mwisho Hadi kiluvya

Kuanzia resort Hadi ubungu Kuna mitaani Ina vigagula na vibaka hatari .

Ila Kuna kuna baadhi ya maeneo yako poa

Mfano korogwe pale upande wa kushoto Kama unaelekea mjini ndani ndani kule kupo POA kumetulia Sana .

Na baadhi ya maeneo msewe Hadi kule karibu na udsm

Kwengine kote wezi, vibaka, vigagula,bangi tupu

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom