Maeneo gani ni mazuri kwa kuishi na familia hapa DsM

Habari wadau..!

Zamani wakati nipo chuo pale Mlimani nilikuwa naamini maeneo mazuri kwa kuishi DsM ni Sinza na Survey maana maeneo hayo yana totozi nzuri na bata za kufa mtu kwa kipindi hicho.

Hivyo nilijitahidi kila mwaka wa masomo lazima nipate chumba Survey au Sinza .

Ila sasa nina familia napata ugumu kuchagua sehemu ya kuishi na kulea familia,maana familia inahitaji maeneo yenye utulivu na penye huduma zote za jamii na pasiwe wachawi au vigagura na msongamano wa nyumba kama za huku kwetu Buza.

Hivi kwa hapa Dar ni maeneo gani yametulia kwa kuishi na kulea familia ,ambapo hautajutia kujenga au kununua nyumba ya kuishi maeneo hayo.
Masaki
 
Kinondoni, karibu na kwa tarimba pametulia, kinondoni kule kwa mengi apmerulia pia. Mi napenda kinondoni ni rahisi kwa kazini na shule kwa watoto. Sema sio ukakae kinondoni nyumba ya watu kumi nyumba yako mwenywe ndo naona ubora
Kwa malezi ya familia kinondoni , mwanayamala , hazifai niliwahi kupanga miaka ya nyuma , asee huvuki nyumba tatu bila kukuta mtoto teja
 
Habari wadau..!

Zamani wakati nipo chuo pale Mlimani nilikuwa naamini maeneo mazuri kwa kuishi DsM ni Sinza na Survey maana maeneo hayo yana totozi nzuri na bata za kufa mtu kwa kipindi hicho.

Hivyo nilijitahidi kila mwaka wa masomo lazima nipate chumba Survey au Sinza .

Ila sasa nina familia napata ugumu kuchagua sehemu ya kuishi na kulea familia,maana familia inahitaji maeneo yenye utulivu na penye huduma zote za jamii na pasiwe wachawi au vigagura na msongamano wa nyumba kama za huku kwetu Buza.

Hivi kwa hapa Dar ni maeneo gani yametulia kwa kuishi na kulea familia ,ambapo hautajutia kujenga au kununua nyumba ya kuishi maeneo hayo.
Ni zamu yako na weye uwapelekee totoz wazuri.Kwani wale totoz wazuri uliokuwa ukiwakuta huko ulidhani hawakuwa na wazazi?Mbona unafurahisha sana?Hamia hukohuko.
 
Kisemvule ndo mpango,kutokana na magonjwa haya epuka kukaa sehemu yenye watu wengi,kuishi nje ya mji Raha sana
 
Kwa malezi ya familia kinondoni , mwanayamala , hazifai niliwahi kupanga miaka ya nyuma , asee huvuki nyumba tatu bila kukuta mtoto teja
Ndio maana nikamtajia hizi sehemu nilizokaa. Kule kwa mengi kila mtu ndan ya get lake hao mareja labda wawe wamefungiwa humo magetini
 
Back
Top Bottom