Maeneo mengi ujenzi wa SGR umesimama

Maeneo mengi ujenzi wa SGR umesimama

Phillemon Mikael

Platinum Member
Joined
Nov 5, 2006
Posts
10,557
Reaction score
8,673
Taarifa za uhakika ni kuwa Ujenzi wa Reli ya SGR hasa vipande vinavyohusu kampani ya waturuki umesimama na kazi zinazoendelea ni chini ya asilimia kumi, yaani ni kama wanaweka watu wachache kwenye sites ili kusionekane hakuna watu kabisa.

Ni vema serikali kama kweli inawalipa ikachunguza ni nini kinaendelea huko, kama kuna matatizo pengine yanayotokana na madhara ya tetemeko la ardhi au kampuni inayumba kifedha basi hatua za haraka zichukuliwe.

Hii sio siri tena na mwisho itaonekana kama vile wananchi wanadanganywa, hali hii inasikitisha sana … kama kampuni imekwama basi watakiwe kutafuta mbia haraka.
 
Kuna muda utafika, unakutana na mkenya, Mrwanda n.k, anakuuliza wewe ni Mtanzania? Unakataa tu, unasema sio Mtanzania, unataja tu walau kabila lako yatosha kabisa!

Kuna kaaibu fulani nakaona kwa hapo mbele kujitambulisha kama Mtanzani eti!

Hii nchi inafeli kila pahala sasa, mafisadi ndio wenye nchi na hawatishiwi nyau, kufeli kwa miradi ni sababu za mafisadi tu

Nchi inatafunwa mpaka tunakosa pesa ya kuendeshea miradi sasa!
 
Nilisikia pia mradi wa kufua umeme situation ipo hivyo.

Hali ni Tete kila mahali ila ndio hivyo mabango ya kusifia nayo ni mengi sana mjini.

Hili la kampuni ya uturuki serikali iwe makini ..wasije kusema matetemeko ya ardhi yamewafilisi na kisheria ni natural disaster ..wataitumia kama sababu ya kuanza kupiga danadana …..

Au kama report ya CAG imewastua sana TRC tuambiwe ….na Madilu arudishe chenchi ya 1.5 trillion
 
Taarifa za uhakika ni kuwa Ujenzi wa Reli ya SGR hasa vipande vinavyohusu kampani ya waturuki umesimama na kazi zinazoendelea ni chini ya Asilimia kumi …yaani ni kama wanaweka watu wachache kwenye sites ili kusionekane hakuna watu kabisa …

Ni vema serikali kama kweli inawalipa ikachunguza ni nini kinaendelea huko , kama kuna matatizo pengine yanayotokana na madhara ya tetemeko la ardhi au kampuni inayumba kifedha basi hatua za haraka zichukuliwe ….

Hii sio siri tena na mwisho itaonekana kama vile wananchi wanadanganywa , hali hii inasikitisha sana … kama kampuni imekwama basi watakiwe kutafuta mbia haraka …..
Reli ya kati na TRC ilihujumiwa hadi zikafa kabisa na wahujumu hao ni wale wale. Hata SGR wapo ambao haiwafurahishi. We need total overhaul kuweka sawa Taifa letu otherwise tunaelekea nyakati ambazo tutakuwa na mfumo wa kifisadi mgumu mno kuuvunja.

Kwanza CCM yenyewe ambayo kuna watu wanajinasibu ni yao irudi kwa wananchi ili iwepo fair ground ya kujenga nchi bila individuals au some elites influences.
 
Mtandao wote wa ubadhirifu wa mali za uma umerudi kwa kasi kubwa ni kama vile wanashtuana kila mahali ni mwendo wa kupiga tu.

Kama kuna wazalendo bado wasikae kimya ila kama sote tumekubaliana kuwa Taifa lisilojali vizazi vijavyo kwa kufanya ufujaji Wacha wizi uendelee.
 
CCM kurudi kwa wananchi ni sawa na kuota Ndiyo ya mchana.
 
tatizo usifiaji umekuwa mkubwa kuliko uhalisia wa mambo

sasa imagine hata viporo tu kumalizia ni shida,je itawezekana kuanzishwa kwa miradi mipya mingine?

Mungu tu asaidie kuvusha hili Taifa.
 
Mtandao wote wa ubadhirifu wa mali za uma umerudi kwa kasi kubwa ni kama vile wanashtuana kila mahali ni mwendo wa kupiga tu.

Kama kuna wazalendo bado wasikae kimya ila kama sote tumekubaliana kuwa Taifa lisilojali vizazi vijavyo kwa kufanya ufujaji Wacha wizi uendelee.

Dhalimu alipora uchaguzi akajaza wanaccm wenzake bungeni eti kuwa ni wazalendo, hao ndio inabidi wahoji huo wizi maana wao tuliambiwa ni wazalendo.
 
Reli ya kati na TRC ilihujumiwa hadi zikafa kabisa na wahujumu hao ni wale wale. Hata SGR wapo ambao haiwafurahishi. We need total overhaul kuweka sawa Taifa letu otherwise tunaelekea nyakati ambazo tutakuwa na mfumo wa kifisadi mgumu mno kuuvunja.

Kwanza CCM yenyewe ambayo kuna watu wanajinasibu ni yao irudi kwa wananchi ili iwepo fair ground ya kujenga nchi bila individuals au some elites influences.

Irudi kwa wananchi vipi wakati tumeambiwa walishinda kwa 95% kwenye uchaguzi?!
 
Kuna muda utafika, unakutana na mkenya, Mrwanda n.k, anakuuliza wewe ni Mtanzania? Unakataa tu, unasema sio Mtanzania, unataja tu walau kabila lako yatosha kabisa!

Kuna kaaibu fulani nakaona kwa hapo mbele kujitambulisha kama Mtanzani eti!

Hii nchi inafeli kila pahala sasa, mafisadi ndio wenye nchi na hawatishiwi nyau, kufeli kwa miradi ni sababu za mafisadi tu

Nchi inatafunwa mpaka tunakosa pesa ya kuendeshea miradi sasa!
Wewe kwani Mtanzania ?
 
Back
Top Bottom