Maeneo mengi ujenzi wa SGR umesimama

Maeneo mengi ujenzi wa SGR umesimama

Malori na mabus mengi ni yao usitegemee SGR itakamilika
 
JPM mwenyewe ali complicate tu ila hata kungekuwa na fair ground kiasi gani hakuna ambaye angemshinda uchaguzi uliopita! Hili sitaki hata kubishana na mtu.

BTW ninaposema CCM kurudi kwenye mikono ya wananchi ni fursa kwa kila mwanachama kuchaguliwa bila influence ya fedha, kufuata katiba na kanuni kikamilifu zao wenyewe bila lobbyings na janja janja. Hii itaondoa dhana ya kubebana ambayo inaondoa uwajibikaji zaidi ya maigizo.

CCM kuhamisha focus ya watu kwa Rais hasa kipropaganda imefanya wapone lawama nyingi. Mfano sasa hivi tunaona awamu ya tano na sita ni kama wapinzani! Wapinzani halisi nao wanaingia kwenye mtego huo huo wa makundi hayo.

Wametengeneza awamu zinazopingana na kutusahaulisha adui halisi! Msoga vs Lupaso , Jiwe vs Msoga ! Sasha vs Jiwe Matatizo yanasalia yale yale ila tunafurahi tusiowapenda wakisulubiwa kijanja janja.

Hakucomplacate kwa bahati mbaya uchaguzi ule, bali hata kama angeshinda sio kwa ushindi aliotaka. Hakuna mwenye tatizo na yeye kushinda kihalali, bali ushindi aliokuwa anautaka asingeweza kuupata, na kibaya zaidi hata chama chake kisingekuwa na uwezo wa kupata 2/3 ya kuwawezesha kufanya maamuzi watakavyo bungeni. Hili hutakiwi ubishane na yoyote bali ndio ukweli, na ingekuwa kinyume chake Magufuli asingepora uchaguzi.

Hakuna CCM ya kurudi kwa wananchi, na siku ikitokea hivyo ndio utakuwa mwisho wa CCM. Kwa sasa hivi na kizazi hiki tofauti, nguvu halisi ya CCM iko ndani ya mbeleko ya vyombo vya dola, na nguvu hiyo inaweza kupangaliwa na watu wachache sio hao wanachama unaoita wananchi. Kama ikitokea hakuna kubebana ndani ya CCM, ni wazi hakutakuwa na kubebana nje ya CCM pia, jambo ambalo halitaisaidia CCM zaidi ya kuifikisha mwisho wake.

Wanachokifanya wapinzani sio kuingia kwenye ugomvi wa hayo makundi, bali ni kuchochea moto baina ya mahasimu wa hizi awamu, maana ugomvi wao ni faida kwao.
 
Kwa hili kusema ukweli awamu ya 5 na 6 hawana tofauti. Labda tofauti iliyopo mabango ya awamu ya 6 ni makubwa zaidi na yamekaa kiprofesheno wakati yale ya awamu 5 yalikuwa ya kishamba sana hayakuwa kiprofesheno

johnthebaptist
Awamu ya sita ambayo kimsingi haipo kikatiba.

Ina mabango mengi ambayo kiuhalisia yanayosemekana kufanya humo hayapo kabisa.

Awamu ya Tano wakisema wamefanya jambo ukifuatilia unaliona mwenyewe kwa macho Yako .

Hawa wa Sasa maneno meengi utendaji sifuri.
 
tatizo usifiaji umekuwa mkubwa kuliko uhalisia wa mambo

sasa imagine hata viporo tu kumalizia ni shida,je itawezekana kuanzishwa kwa miradi mipya mingine?

Mungu tu asaidie kuvusha hili Taifa.
"mama" hata apewe miaka 20 hatofanya lolote, kitu alichokosea toka mwanzo ni alipojiweka karibu na walamba asali
unaachiwa gari ya Boss alafu unakuwa na ukaribu na makonda waliofukuzwa na dereva wa Mwanzo

Jiwe hata kama alikuwa anapiga pesa ila alijuwa kabisa wenzake ni wezi mno hivo akiwaachia wapige mambo hayaendi
 
Kinachonipa moyo ni jinsi wananchi walivyojitambua , tungekuwa hatushtuki ningeumia mno ila soon kijani itakuwa nyekundu
 
Yawezekana wamehamia kipande cha Tabora-Isaka kuanza tuta.
 
Hakucomplacate kwa bahati mbaya uchaguzi ule, bali hata kama angeshinda sio kwa ushindi aliotaka. Hakuna mwenye tatizo na yeye kushinda kihalali, bali ushindi aliokuwa anautaka asingeweza kuupata, na kibaya zaidi hata chama chake kisingekuwa na uwezo wa kupata 2/3 ya kuwawezesha kufanya maamuzi watakavyo bungeni. Hili hutakiwi ubishane na yoyote bali ndio ukweli, na ingekuwa kinyume chake Magufuli asingepora uchaguzi.

Hakuna CCM ya kurudi kwa wananchi, na siku ikitokea hivyo ndio utakuwa mwisho wa CCM. Kwa sasa hivi na kizazi hiki tofauti, nguvu halisi ya CCM iko ndani ya mbeleko ya vyombo vya dola, na nguvu hiyo inaweza kupangaliwa na watu wachache sio hao wanachama unaoita wananchi. Kama ikitokea hakuna kubebana ndani ya CCM, ni wazi hakutakuwa na kubebana nje ya CCM pia, jambo ambalo halitaisaidia CCM zaidi ya kuifikisha mwisho wake.

Wanachokifanya wapinzani sio kuingia kwenye ugomvi wa hayo makundi, bali ni kuchochea moto baina ya mahasimu wa hizi awamu, maana ugomvi wao ni faida kwao.
Hayo mengine uliyosema kila mtu ana mtazamo wake hivyo ibakie hivyo.

Kuhusu wapinzani kuingia kwenye mtego wa upinzani feki within CCM kwamba wanachochea kuni ni kitu cha kijinga kwao. Kwanza mambo mengi yako engineered na CCM na wao wenyewe wanajua jinsi ya kutatua kama walivyowatumia kumsafisha EL ambaye waliwatumia pia kumchafua.

Shortly tuna upinzani feki huku nje while huko ndani executives ni washkaji na wanajua wanachofanya. Ndio maana tunapoona mtu mwenye msimamo kama Lissu tunatamani asiingie mtegoni akomboe hivi vyama. Bahati mbaya hizi complications za awamu ya tano zinaweza kuwa zimesha mdilute!

Tuna wanasiasa wachache wa ukweli huko upinzani lakini vyama vina wenyewe na ndio wanaoamua directions sio akina Heche wala Lissu wanaoitwa Conservative now days [emoji58]
 
Taarifa za uhakika ni kuwa Ujenzi wa Reli ya SGR hasa vipande vinavyohusu kampani ya waturuki umesimama na kazi zinazoendelea ni chini ya asilimia kumi, yaani ni kama wanaweka watu wachache kwenye sites ili kusionekane hakuna watu kabisa.

Ni vema serikali kama kweli inawalipa ikachunguza ni nini kinaendelea huko, kama kuna matatizo pengine yanayotokana na madhara ya tetemeko la ardhi au kampuni inayumba kifedha basi hatua za haraka zichukuliwe.

Hii sio siri tena na mwisho itaonekana kama vile wananchi wanadanganywa, hali hii inasikitisha sana … kama kampuni imekwama basi watakiwe kutafuta mbia haraka.
Mkuu 'Philemon Mikael' asante kuhusu taarifa hii. Nami kupitia kwako niulize swali: Hivi kile kipande cha kwanza cha ujenzi wa reli toka Dar hadi Morogoro kilisha kamilika na kufanya kazi?

Nikipata jibu sahihi linaloonyesha ukamilifu wa kipande hicho, nitatoa sifa kedekede kwa wahusika.
Lakini kama jibu ni hapana, basi ni wazi kwamba hiyo reli, pengine na miradi mingine inayoendelea haiwezi kukamilishwa chini ya kiongozi huyu tulie naye sasa.
 
Back
Top Bottom