ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Kama ni msimu wa mvua Kwa nini ujenzi usisimame?Taarifa za uhakika ni kuwa Ujenzi wa Reli ya SGR hasa vipande vinavyohusu kampani ya waturuki umesimama na kazi zinazoendelea ni chini ya asilimia kumi, yaani ni kama wanaweka watu wachache kwenye sites ili kusionekane hakuna watu kabisa.
Ni vema serikali kama kweli inawalipa ikachunguza ni nini kinaendelea huko, kama kuna matatizo pengine yanayotokana na madhara ya tetemeko la ardhi au kampuni inayumba kifedha basi hatua za haraka zichukuliwe.
Hii sio siri tena na mwisho itaonekana kama vile wananchi wanadanganywa, hali hii inasikitisha sana … kama kampuni imekwama basi watakiwe kutafuta mbia haraka.
Pia kama hawalipwi inavyostahili wanaweza Kusua sua pia,aidha juzi Kati hapo Wafanyakazi wao waligoma huko Singida.