Maeneo mengi ujenzi wa SGR umesimama

Maeneo mengi ujenzi wa SGR umesimama

17 January 2023
Bucharest, Romania

YAPI MERKEZI YASAINI MKATABA WA EURO MILIONI 45 KUKARABATI RELI ZA NCHINI ROMANIA


Video kipande cha kutoka Bucharest hadi Craiova nchini Romania kufanyiwa ukarabati wa nguvu na kampuni ya Uturuki ya Yapi Merkezi, shirika la reli la nchini Romania la CFR latangaza.

Yapi Merkezi yazidi kusaini mikataba ya sekta ya reli na ujenzi duniani huku website yake ikionesha mafanikio ya kikazi ndani ya Turkey yenyewe pia nchi za ngambo hasahasa UAE- the United Arab Emirates, Saudi Arabia, Sudan, Algeria, Morocco na Ethiopia.


Yapı Merkezi signs 45 mln euro railway upgrade deals in Romania​

AuthorNicoleta Banila
Published
Jan 17, 2023 17:39 EEST
BUCHAREST
Yapı Merkezi signs 45 mln euro railway upgrade deals in Romania
Source: CFR
January 17 (SeeNews) - Romanian railway operator CFR said on Tuesday that it signed 11 contracts worth a total of 221 million lei ($48 million/45 million euro) with Turkish company Yapı Merkezi for upgrades on the railway connecting Bucharest to Craiova.
Following rehabilitation works, the 24 km railway section will allow for train speeds of up to 120 km/h, CFR said in a press release.
Works under each of the 11 Quick Wins contracts should be completed within 24 months. Financing is secured through non-refundable funds under Romania’s National Plan for Recovery and Resilience, PNRR.
Yapı Merkezi Construction and Industry has so far developed buildings, heavy construction and railway projects both in Turkey and abroad, especially in the United Arab Emirates, Saudi Arabia, Sudan, Algeria, Morocco and Ethiopia, according to its website


Hiyo ni light weight railway …kazi tuliyowapa hapa ndio kubwa zaidi kwao kupata kuifanya …maana hapa unaongelea almost kilometer 1,000 sio Jambo dogo
 
Unaweza kutupa mifano japo ya picha kuona hali halisi ilivyo! maana sisi huku kwetu mbwinde tunaona Yapi Merkezi waliendelea na shughuli za hapa na pale

Shughuli za hapa na pale ndio hizo kusua sua ..hujasikia hadi wafanyakazi wao wanagoma …au unafikiri hii ni siasa >??
Contractor ana namna nyingi za kuchelewesha kazi …..anaweza kila siku anaenda site ili tu waonekane lakini hawapigi hatua …
Hujasikia hadi magari yao mengine wamepaki ..hawaweki mafuta ……kipande cha Dar - moro kila siku mnaambiwa kinaanza mwezi ujao toka mwaka 2021 tunaambiwa wako asilimia 95%
 
Unasema habari za uhakika kutoka kwa nani? Mkiendeleza uongo itabidi tumwambie webmaster akufute . Kama ni mawazo yako usiseme habari za uhakika sema kwa mawazo yangu!

Mwambie basi anifute ….acha kutisha watu …au unataka kutuambia wewe ndio commanding officer wa Webmasters …????
Kwani mfano ingekua uwongo kwanini ukasirike hivyo na hata kuona anayewaza tofauti afutwe ?? Kuna mambo mangapi yanaandikwa humu ndani kwanini hili tu ndio likukere …
Ifike makali tuwe wazalendo …na tuache hyena hyenaaaa
 
Kwani ni hela za wañaccm, hizo ni kodi zetu, sio vibaya CDM wakichukua sehemu ya makusanyo ya kodi zao kisheria. Au unaumia ww jizi la kura?
Kwahiyo zile kiki za kujifanya mnavunga kuvuta mkwanja wa ruzuku kwani wanacdm walikuwa hawalipi kodii??
 
Awamu ya sita ambayo kimsingi haipo kikatiba.

Ina mabango mengi ambayo kiuhalisia yanayosemekana kufanya humo hayapo kabisa.

Awamu ya Tano wakisema wamefanya jambo ukifuatilia unaliona mwenyewe kwa macho Yako .

Hawa wa Sasa maneno meengi utendaji sifuri.

Awamu ya tano ilisema reli ya SGR kipande cha Dar-Moro kitaanza kazi kufikia desemba 2019, hadi leo hadithi. Walisema wamejenga viwanda 4,000, weka viwanda hata 200 vilivyojengwa hiyo awamu ya tano ili tukavione kwa macho maana ww uliona hivyo vyoye 4,000+.

Tuliambiwa kwa mbwembwe kubwa mwaka 2017 pale chongoleani Tanga kuwa bomba la mafuta ya Uganda litakuwa limefika Tanga November 2020. Hadi leo ni porojo tu. Je haya uliyaona kwa macho, au macho ya kiroho?
 
Taarifa za uhakika ni kuwa Ujenzi wa Reli ya SGR hasa vipande vinavyohusu kampani ya waturuki umesimama na kazi zinazoendelea ni chini ya asilimia kumi, yaani ni kama wanaweka watu wachache kwenye sites ili kusionekane hakuna watu kabisa.

Ni vema serikali kama kweli inawalipa ikachunguza ni nini kinaendelea huko, kama kuna matatizo pengine yanayotokana na madhara ya tetemeko la ardhi au kampuni inayumba kifedha basi hatua za haraka zichukuliwe.

Hii sio siri tena na mwisho itaonekana kama vile wananchi wanadanganywa, hali hii inasikitisha sana … kama kampuni imekwama basi watakiwe kutafuta mbia haraka.
Acha upotoshaji hakuna kilichosimama kila mradi unaendelea chini ya Rais Samia Suluhu
 
Tangu Novemba 2019 walitwambia safari za SGR kati ya Dar na Morogoro zingeasha, leo hii ni 2023........kuna kitu gani unatarajia hapo! Huu mradi umeshahujumiwa na unaenda kuwa white elephant pamoja na kutumia matrilioni ya pesa za nchi ambazo ni pamoja na mikopo ambayo tutaendelea kulipa kwa miaka mingi....​
Ni white elephant niliuona hivyo toka awali. Niliamini usingekamilika kwa wakati. Tatizo wala sio waturuki.
 
Hiyo ni light weight railway …kazi tuliyowapa hapa ndio kubwa zaidi kwao kupata kuifanya …maana hapa unaongelea almost kilometer 1,000 sio Jambo dogo

Mradi wa SGR Reli mpya Tanzania umewekwa mbwembwe, nakshi, vikolombwezo n.k nyingi kuliko reli za SGR za bara la Marekani ya Kaskazini, Australia, Bara Ulaya yote Magharibi na Mashariki , India hivyo kuufanya mradi wa SGR Reli mpya ya Tanzania kuwa wa gharama kubwa kupita kiasi huku njia nzima ya reli ya SGR Reli Tanzania pembezoni hakuna viwanda, karakana, mashamba makubwa wala ranchi kubwa za mamilioni ya mifugo kama ya Ukraine, Brazil, USA, Canada n.k


Sijui reli hii ya SGR mpya Tanzania itajilipa vipi kutokana na shughuki za ndani kama usafirishaji wa ndani wa, mazao ya kilimo, viwanda, ufugaji, vipuri vya katakana n.k kama ilivyo kwa nchi zingine hata hiyo Romania, Italy pembezoni mwa reli zao kuna shughuli kubwa za kiuchumi za ndani ya nchi zao.


Treni inayosafiri baina ya mikoa nchini Italy, stesheni zake, mazingira n.k


26 Agosti 2022 Trip report on board Trenitalia's Regionale Veloce Train RV from Torion Porta Nuova to Ventimiglia.
 
Hakuna serikali yoyote unayoifikiria itafanya chochote ndugu yangu. Kila idara ziko dormant kama vile hakuna viongozi katika nchi.
 
Njia sahihi kama ujenzi unasua sua wahojiwe pande zote za mkataba juu ya kusua sua huko ili upate majibu.Kwa kuwa tumewapa dhamna ni wajibu wao kutoa majibu,ikitokea wakatoa majibu yanayomtetea mkandarasi basi wanakua wanakua sababu.
 
Mwambie basi anifute ….acha kutisha watu …au unataka kutuambia wewe ndio commanding officer wa Webmasters …????
Kwani mfano ingekua uwongo kwanini ukasirike hivyo na hata kuona anayewaza tofauti afutwe ?? Kuna mambo mangapi yanaandikwa humu ndani kwanini hili tu ndio likukere …
Ifike makali tuwe wazalendo …na tuache hyena hyenaaaa

Tumechoka utamaduni wa uongo hapa kama ni mawazo yako sema na sio kutudanganya "habari za uhakika" kutoka wapi?? Onyo la mwisho toa hoja acha uongo bila hivyo utaishia kwenye mitandao ya udaku
 
Kuna muda utafika, unakutana na mkenya, Mrwanda n.k, anakuuliza wewe ni Mtanzania? Unakataa tu, unasema sio Mtanzania, unataja tu walau kabila lako yatosha kabisa!

Kuna kaaibu fulani nakaona kwa hapo mbele kujitambulisha kama Mtanzani eti!

Hii nchi inafeli kila pahala sasa, mafisadi ndio wenye nchi na hawatishiwi nyau, kufeli kwa miradi ni sababu za mafisadi tu

Nchi inatafunwa mpaka tunakosa pesa ya kuendeshea miradi sasa!
Utawaambia ikiwa inamilazimu nikujibu suala lako basi mimi ni Mzanzibari! 😂😂😂
 
Hakucomplacate kwa bahati mbaya uchaguzi ule, bali hata kama angeshinda sio kwa ushindi aliotaka. Hakuna mwenye tatizo na yeye kushinda kihalali, bali ushindi aliokuwa anautaka asingeweza kuupata, na kibaya zaidi hata chama chake kisingekuwa na uwezo wa kupata 2/3 ya kuwawezesha kufanya maamuzi watakavyo bungeni. Hili hutakiwi ubishane na yoyote bali ndio ukweli, na ingekuwa kinyume chake Magufuli asingepora uchaguzi.

Hakuna CCM ya kurudi kwa wananchi, na siku ikitokea hivyo ndio utakuwa mwisho wa CCM. Kwa sasa hivi na kizazi hiki tofauti, nguvu halisi ya CCM iko ndani ya mbeleko ya vyombo vya dola, na nguvu hiyo inaweza kupangaliwa na watu wachache sio hao wanachama unaoita wananchi. Kama ikitokea hakuna kubebana ndani ya CCM, ni wazi hakutakuwa na kubebana nje ya CCM pia, jambo ambalo halitaisaidia CCM zaidi ya kuifikisha mwisho wake.

Wanachokifanya wapinzani sio kuingia kwenye ugomvi wa hayo makundi, bali ni kuchochea moto baina ya mahasimu wa hizi awamu, maana ugomvi wao ni faida kwao.
Kwa hiyo unaweza kuweka hata kielelezo hata kimoja hapa kuthibitisha hizo tuhuma si watu walipiga kura na waangalizi wenu
 
Back
Top Bottom