Saguda47
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 11,784
- 22,106
Itoshe tu kusema Jiji la Mbeya ni moja ya miji yenye miundombinu duni kabisa Tanzania hii.
Jiji lisilo na mpangilio maalumu, barabara duni, mifereji ya majitaka mibovu na inasababisha kujaa maji hovyo katikati ya maeneo muhimu. Hizi ni picha za eneo muhimu la Kabwe jijini Mbeya, zimepigwa mnamo 2/2/2026 jioni.
Hali hii ya miundominu mibovu siyo hapo tu, kuna maeneo mengine kama Chuo cha Teofilo - Kisanji na Teku huwa yanapata changamoto za maji kujaa na njia kuziba inapotokea kuna mvua.
Juzi tu hapa tumeona Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Patrick Mwalunenge akisimamisha msafara wake baada ya kukutana na dimbwi kubwa la maji katika Barabara ya Soweto, kero ambayo Wananchi walimweleza imekuwepo kwa zaidi ya miaka mitatu bila kuchukuliwa hatua stahiki.