KERO Maeneo mengi ya Mjini Jiji la Mbeya yana changamoto ya miundombinu, iboreshwe inatia aibu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Saguda47

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
11,784
Reaction score
22,106
Itoshe tu kusema Jiji la Mbeya ni moja ya miji yenye miundombinu duni kabisa Tanzania hii.

Jiji lisilo na mpangilio maalumu, barabara duni, mifereji ya majitaka mibovu na inasababisha kujaa maji hovyo katikati ya maeneo muhimu. Hizi ni picha za eneo muhimu la Kabwe jijini Mbeya, zimepigwa mnamo 2/2/2026 jioni.

​

Hali hii ya miundominu mibovu siyo hapo tu, kuna maeneo mengine kama Chuo cha Teofilo - Kisanji na Teku huwa yanapata changamoto za maji kujaa na njia kuziba inapotokea kuna mvua.



Juzi tu hapa tumeona Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Patrick Mwalunenge akisimamisha msafara wake baada ya kukutana na dimbwi kubwa la maji katika Barabara ya Soweto, kero ambayo Wananchi walimweleza imekuwepo kwa zaidi ya miaka mitatu bila kuchukuliwa hatua stahiki.​
 
Majiji yote Tanzania ni hivyo hivyo ukitoa Dom
 
Kwani mkoa upi kuna afadhari? Ccm ni laana kwa Tanzania
 
Nyie si mlitamba kuwa mnampa kura Tulia Ackson kwa vile ni Rais wa maspika wa dunia. Imekula kwenu na dada uspika hata wa bunge la Dodoma katemeshwa
 
Mbeya ni Kijiji kubwa siyo jiji ddm imeipiku mbeya na arusha ddm inakimbiza sna
Ukiacha majengo ya Serikali na barabara zake na wafanyakazi wake, Dodoma bado ni maskini tu.

Sijui wewe ni Dr wa nini? Maana akili yako unaijuwa mwenyewe
 
Kama unaishi Dar naomba upige picha za Ikulu Magogoni hadi Posta ya zamani ambayo haitakuwa na Bajaj.

Acheni kuibeza Mbeya, kila jiji lina sehemu yake mbaya na umaskini wake
冷静一点,我完全没提到达尔。
 
Huu mji kinachowaponza ni ubishi wa watu wa mbeya, Suala la mipango miji ni ubovu wa Halmshauri yenu, Musije Mukafananisha kijiji chenu Kilichoumuka na Hii Tanga ya bandari na miradi mikubwa ya mafuta, viwanda vikubwa. Tumewaacha mbali sana ,
 
Nyie si mlitamba kuwa mnampa kura Tulia Ackson kwa vile ni Rais wa maspika wa dunia. Imekula kwenu na dada uspika hata wa bunge la Dodoma katemeshwa
Kwa hiyo Mwabukusi alikuwa sahihi kusema, Mbeya ni mkusanyiko wa Vijiji!
 
Kwa hiyo Mwabukusi alikuwa sahihi kusema, Mbeya ni mkusanyiko wa Vijiji!
Yupo sahihi, nenda Tanga kaone mji ulivyopangwa hadi uswahilini lkn barabara zipo na zinapitika na zinakutana, Na wananchi wa Tanga ni Wasikivu hutokuta mtu kajenga kuingilia barabara,viwanja vimepimwa na bikoni zimetembea maji yamefika kila kiwanja hata kama mtu hajajenga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…