Maeneo ya wazi Mbweni yaanza kuvamiwa na vigogo

Gulwa

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2008
Posts
10,597
Reaction score
16,394
Kama tunavyokumbuka serikali ilifanya zoezi la upimaji wa viwanja maarufu kama 20,000.
Zoezi lilienda vizuri na upimaji ulifanyika vizuri kwa kuacha baadhi ya maeneo kuwa ya wazi kama ilivyo katika miji na majiji mengine ulimwenguni.

Kuna eneo moja Mbweni karibu na kituo cha polisi liliachwa kuwa eneo la wazi na majirani walikuwa wakiyachunga yasivamiwe. Siku za karibuni wananchi waliona shughuli zinazoashiria kuporwa kwa eneo hilo.

Kwa vile eneo hilo lina watu wenye uelewa mkubwa, waliamua kufuatilia kujua kinachoendelea. Baada ya kufuatilia waligundua kuwa eneo hilo limegawiwa kwa kamishna mkuu wa TRA, na kujua kuwa hawawezi kufanya chochote tena kwani uvamizi utakuwa umewahusisha vigogo wa ngazi za juu.

Haya yamefanyika baada ya kuondolewa Lukuvi ambaye alikuwa amewakatalia watu mbalimbali waliotaka kuvamia eneo hilo, na kuna naibu waziri aliyepelekwa hapo kwa kazi maalumu.

Tunarudi nyuma kwa kasi ya ajabu, Mungu atusaidue
 
Dar maeneo yote ya waz vitu vinaota, kuwa mpole masta.

Ni mwendo wa fence na ujenz tu, kila mtu kimyaaa..

Kazi iendelee...
 
ndio hata mvua zikinyesha maji yanashindwa pa kwenda matokeo yanajikatizia barabarani na kukata madaraja na njia....yoote hii ni kwasababu ya kutofuata utaratibu wa ujenzi wa mji.. Dar es salaam imekaa kama jalala tu.
Siku la kutokea kama la Uturuki maeneo kama Kariakoo na Posta ndio bas tena...
 
Kidata amepewa lile eneo? Maana ndo anakaa huko mbweni. Kidata nitakuja hapo home unipe kazi TRA
 
Kama tunavyokumbuka serikali ilifanya zoezi la upimaji wa viwanja maarufu kama 20,000.
Zoezi lilienda vizuri na upimaji ulifanyika vizuri kwa kuacha baadhi ya maeneo kuwa ya wazi kama ilivyo katika miji na majiji mengine ulimwenguni.

Kuna eneo moja Mbweni karibu na kituo cha polisi liliachwa kuwa eneo la wazi na majirani walikuwa wakiyachunga yasivamiwe. Siku za karibuni wananchi waliona shughuli zinazoashuria ikuporwa kwa eneo hilo.

Kwa vile eneo hilo lina watu wenye uelewa mkubwa, waliamua kufuatilia kujua kinachoendelea. Baada ya kufuatilia waligundua kuwa eneo hilo limegawiwa kwa kamishna mkuu wa TRA, na kujua kuwa hawawezi kufanya chochote tena kwani uvamizi utakuwa umewahusisha vigogo wa ngazi za juu.

Haya yamefanyika baada ya kuondolewa Lukuvi ambaye alikuwa amewakatalia watu mbalimbali waliotaka kuvamia eneo hilo.

Tunarudi nyuma kwa kasi ya ajabu, Mungu atusaidue
Na mbweni mpigi karibu na shule ya sekondari na zahanati ya mbeni, kulikua na eneo kubwa la wazi, sasahivi washagawqna na wameshaanza kujenga
 
Huyo wanayemsema kamishna wa Tra hata kule mbweni moga masaika street kulikuwa na eneo la soko na viwanja vya michezo kalizungushia ukuta lote na kajenga maofisi sijui na mabanda ya ufugani kuku ni kama hekari 4 hivi likiuwa eneo la wazi lakini serikari ya mtaa ipo na maafisa ardhi wapo wamekaa kimya.
 
Kama tunavyokumbuka serikali ilifanya zoezi la upimaji wa viwanja maarufu kama 20,000.
Zoezi lilienda vizuri na upimaji ulifanyika vizuri kwa kuacha baadhi ya maeneo kuwa ya wazi kama ilivyo katika miji na majiji mengine ulimwenguni.

Kuna eneo moja Mbweni karibu na kituo cha polisi liliachwa kuwa eneo la wazi na majirani walikuwa wakiyachunga yasivamiwe. Siku za karibuni wananchi waliona shughuli zinazoashiria kuporwa kwa eneo hilo.

Kwa vile eneo hilo lina watu wenye uelewa mkubwa, waliamua kufuatilia kujua kinachoendelea. Baada ya kufuatilia waligundua kuwa eneo hilo limegawiwa kwa kamishna mkuu wa TRA, na kujua kuwa hawawezi kufanya chochote tena kwani uvamizi utakuwa umewahusisha vigogo wa ngazi za juu.

Haya yamefanyika baada ya kuondolewa Lukuvi ambaye alikuwa amewakatalia watu mbalimbali waliotaka kuvamia eneo hilo, na kuna naibu waziri aliyepelekwa hapo kwa kazi maalumu.

Tunarudi nyuma kwa kasi ya ajabu, Mungu atusaidue
Haya ndio mambo ya kuripoti Sasa na wasipochukua hatua,wapigeni chini 2025.

Sheria lazima ziheshimiwe na wote na huyo kigogo wa TRA aumbuliwe kama hivi.
 
Back
Top Bottom