Kama tunavyokumbuka serikali ilifanya zoezi la upimaji wa viwanja maarufu kama 20,000.
Zoezi lilienda vizuri na upimaji ulifanyika vizuri kwa kuacha baadhi ya maeneo kuwa ya wazi kama ilivyo katika miji na majiji mengine ulimwenguni.
Kuna eneo moja Mbweni karibu na kituo cha polisi liliachwa kuwa eneo la wazi na majirani walikuwa wakiyachunga yasivamiwe. Siku za karibuni wananchi waliona shughuli zinazoashiria kuporwa kwa eneo hilo.
Kwa vile eneo hilo lina watu wenye uelewa mkubwa, waliamua kufuatilia kujua kinachoendelea. Baada ya kufuatilia waligundua kuwa eneo hilo limegawiwa kwa kamishna mkuu wa TRA, na kujua kuwa hawawezi kufanya chochote tena kwani uvamizi utakuwa umewahusisha vigogo wa ngazi za juu.
Haya yamefanyika baada ya kuondolewa Lukuvi ambaye alikuwa amewakatalia watu mbalimbali waliotaka kuvamia eneo hilo, na kuna naibu waziri aliyepelekwa hapo kwa kazi maalumu.
Tunarudi nyuma kwa kasi ya ajabu, Mungu atusaidue