Inategemea unanunua wapi na kama kuna sale.
Kuna dogo nimemnunulia hizi
hapa juzi kama $60 hivi, online naona wanauza $90.
Timbs kuna za $100 mpaka $200, lakini mimi najua outlets wanauza mpaka $60.
Kuna outlets za Clarks kiatu cha $100 unapata hata $40, halafu unapata deal la buy one get one for $10, kwa hiyo unaweza kupata mikwaju miwili mikali kwa $50 ukicheza nao vizuri.
Halafu mimi kila nikinunua napata points, kwa hiyo unaweza kuwa na points za kukuondolea $20, kwa hivyo unaweza kupata katika hiyo $50, unaondolewa $20 unanunua viatu viwili kwa $30.
Ni suala la kujua ununue wapi, muda gani, kwenye sale gani etc. Karibu mara zote mimi sinunui full price, labda nikienda duka la Johnson & Murphy nikaona mkwaju wa kweli nimeutaka na sitaki kusubiri sale.