Prakatatumba abaabaabaa
JF-Expert Member
- Aug 2, 2022
- 1,842
- 6,087
Definition ya mafanikio ni kubwa sana, inategemea na mtu anaonaje mafanikio lakini uhalisia unabaki kuwa mafanikio ni pesa/umiliki wa mali.
Nimekaa sehemu nikaona vijana wanatembeza muha wanakata vipande 100/200 nikaingia kwenye tafakuri nzito kidogo.
Muhubiri 9:11
Nikarudi nikaona chini ya jua ya kwamba si kila wenye mbio washindao katika michezo,wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo, lakini wakati na bahati huwapata wote.
Nikiwa kwenye tafakuri akapita mtu akiwa ndani ya prado gari jipya plate number EAA, alikua ameshusha vioo vijana wakaanza kumjadili kwa sana huku wakinung'unika wengine wakisema anafanya kazi usalama, wengine wakasema dah, hata hela ya kula sina.
Kwenye tafakari pia nikawa najiuliza maisha ni juhudi au bahati? Nikasema ni juhudi lakini moyo unakataa maana wanaobeba zege, kuponda mawe, machinga wanaotembea barabarani n.k wanajuhudi sana lakini maisha ni ya kawaida sana.
Watu wanaishi kwenye ndoto kubwa saana ambayo kiuhalisia au kiukweli ni ngumu sana kukamilisha kutokana na mazingira yanayowakabili.
Africa bado tupo kwenye cycle ya poverty ukifanikiwa kutoka kidogo kuona mwanga unakuta unao ndugu weengi wanaosubiria uwashike mkono.
Maisha ni bahati tu tupiganie ndoto zetu lakini tusiwe disappointed kuona hatujayafanikisha tunayoyawaza, tuepuke kua na stress za mafanikio sana.
Mwisho tusipende kutumia msemo kwamba Mungu amempa huyu na huyo hajampa binafsi naamini Mungu hana upendeleo ikiwezekana labda hausiki kabisa na mafanikio yetu ya kidunia, ila dunia inaendeshwa kwa nature tu na bahati.
Unaweza kupambana na kuteseka kutafuta hela na usizipate hela zenyewe.
Mwisho
Tupigane kuzifanikisha ndoto zetu lakini tupigane kutafuta amani ya moyo, tuwe na furaha katika haya maisha lakini jua ya kwamba sio kila ndoto uliyonayo utaitimiza.