Mafanikio katika maisha hayana formula. Acha kuiogopa kesho yako

Mafanikio katika maisha hayana formula. Acha kuiogopa kesho yako

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari!

Mada kuu mahali popote walipo wawili, watatu au hata mtu mmoja ni pesa (mafanikio).

Ukikaa maingilio ya Kariakoo asubuhi utajionea maelfu ya watu wakitembea kwa haraka sana kufukuzana na pesa au mafanikio. Mchezo wa kusaka pesa (money game) ni wa milele. Mtu huacha kuwaza pesa pale anapopoteza fahamu au kufa.

Point yangu ni ipi?

Point yangu ni kwamba mafanikio ni methali mpya iliyokosa jibu kila siku. Hayana formula. Fanya kilicho mbele yako ili tu upate kula na kusurvive ila kuhusu mafanikio ni bahati.

Unaweza kufanya kazi Ikulu ukapitwa pesa na mama nitilie wa Tandika, unaweza kuwa manager wa ofisi lakini Crane operator akakupita mafanikio.

Unaweza kuwa na PhD lakini account yako ikawa na pesa kidogo zaidi ya mvuvi wa Sangara wa Mwanza ambaye ni STD 7 tu.

Mtaa ninaoishi watu wenye pesa nyingi wako kama 7 hivi ambao wote ni lasaba tu. Wanamiliki magari ya kubebea mchanga, tofali na uani kwao magari ya kutembelea yamejaa.

Wasomi sisi ndio tunabangaiza na kumiliki vi Suzuki, mwingine Escudo, ist na spacio. Hapa simaanishi kuwa ukiwa na elimu hufanikiwi. No unaweza kumiliki hata billion nakuendelea.

Mafanikio hayaletwi na formula. Tunatafuta ili tu kutimiza amri kuwa tusipofanya kazi tisile ila kuhusu kufanikiwa sio kazi ya mwanadamu.
 
Kama una mikosi hata uajiriwe TRA utaishi kwa dhiki mpaka kifo
Mkuu

Hilo nimeliona KWA macho yangu!

Kuna WATU wabaya Huwa wanaseti pin code kwenye Maisha ya WATU,hadi ziwe decoded ndio mtu anasonga!

Ili kuzidecode Hadi upate mtumishi wa kweli wa Mungu mwenye karama au tabibu makini wa kisomo ndio utoboe!!!

Sio masikhara hilo!

Seen it!
 
Tatizo binadamu wa ckuiz Ni Wabishi Sana ila ndio ukweli wenyewe.
 
Mkuu

Hilo nimeliona KWA macho yangu!

Kuna WATU wabaya Huwa wanaseti pin code kwenye Maisha ya WATU,hadi ziwe decoded ndio mtu anasonga!

Ili kuzidecode Hadi upate mtumishi wa kweli wa Mungu mwenye karama au tabibu makini wa kisomo ndio utoboe!!!

Sio masikhara hilo!

Seen it!
Kuna jamaa ni tax officer tra. Kateseka mpaka kifo chake.
Hii dunia hii
 
Kuna jamaa ni tax officer tra. Kateseka mpaka kifo chake.
Hii dunia hii
Hakupata msaada wa kujua Tatizo liko WAPI!!!

Huwezi tatua Tatizo Hadi ujue HASA tatizo ni lipi!!

Kuna ulevi wa kupindukia hadi hujali familia na watu wakakusema vibaya Sana wakati mwanzoni ulikuwa mtu makini Sana tena mfano wa kuigwa!!!

Msipokua makini Ndugu mnazika MAPEMA sana!!!

Hivyo tu!!
 
Maisha sio tatu mzuka wala jatu.

Kama ujaweka kuthubutu usijidanganye yani ukae hapo pesa zije.

Basi kusingekuwa na majambazi, matepeli, wezi, wafanyabiashara, wakulima na n.k.

Kufanikiwa ni kuthubutu ndio maana kompyuta ilianza kwenye kikokotoo mwanzoni
 
Back
Top Bottom