Mafanikio ndani ya biashara ya dhahabu

Mafanikio ndani ya biashara ya dhahabu

Kuna rafik angu kaanza na mtaji wa 10milioni japo ata milioni 2 nasikia watu wanaanza kutokana na eneo lilipo
Anachukua msumbiji anauzia Dar
Mara ya kwanza alienda na gram 100 akapiga faida ya milion 1.8 akitoa usafir n.k akabaki na milion 1.5
Akaenda tena second time faida ni million 1.875000
Saiz anaenda sokoni kwa mwez Mara 3
Uhakika wa milion 4+ anao ndani ya mwezi mmoja tu gramu kule saiz ni laki moja mgodini
sokoni dar ilikua laki na 25 japo aitabirik muda wowote ina change kama dola
Alafu ni kijana wa 20+ saiz yupo msumbiji wiki hii anazama dar tena kuuza mzigo

We ulianza na mtaji wa shingapi uko chunya?
Maana kama Mimi nikiwa na milioni 2 ni gram 20 sasa from msumbiji to dar mhmm Mara kuchomwa gram zishuke kidogo faida itaishia nauli tu

Je huko kujisajili kama mnunuzi shingapi vibali ?
Wewe unauzia wapi dhahabu ?
Nashukuru mkuu mungu akubariki sana umeongeza kitu hapa
 
Je, dhahabu hutengenezwa nini mkuu maana mzigo mdogo wa dhahabu unakipunga hatari.
Je, products zake zitakuwaje sasa
 
Biashara ya dhahabu haina tofauti na beting!!! Wengi tunaliwa anapata mmoja! Invest what you van loose
Watanzania bana! Kilimo wanasema ni betting,kufuga betting,Kusoma betting,madini betting sa sijui wanaweza nini? Kila kitu kisingizio ni kwao ni betting au uchawi.

Jamani maisha ni kuweka mikakati na kuitekeleza! Tuache kuamini katika bahati na uchawi!
 
Mkuu cha kwanza inabidi uwe timamu wa akili cha pili kuna kutafuta leseni ya uchimbaji cha pili ukiipata leseni jeh!? Hio leseni yako inaenda kuathiriy vipi mazingira unakutana na watu wa mazingira ili wakadirie uharibifu utakao ufanya katika mazingira ufanye malipo ya uharibifu ndo uanze kazi
Mbona nina PML na naendelea na kazi na sikuambiwa kuwa lazima nionane na NEMC?
 
Bei ya dhahabu inaendana na bei ya soko la dunia?
Bei kwenye Masoko ya Dhahabu Tz huendana na Bei ya Soko la dunia,
Ubora wa dhahabu ndio mchawi, unaweza kuwa na dhahabu kubwa ila inasoma asilimia ndogo hivyo utapata hela kidogo
 
Kuna rafik angu kaanza na mtaji wa 10milioni japo ata milioni 2 nasikia watu wanaanza kutokana na eneo lilipo
Anachukua msumbiji anauzia Dar
Mara ya kwanza alienda na gram 100 akapiga faida ya milion 1.8 akitoa usafir n.k akabaki na milion 1.5
Akaenda tena second time faida ni million 1.875000
Saiz anaenda sokoni kwa mwez Mara 3
Uhakika wa milion 4+ anao ndani ya mwezi mmoja tu gramu kule saiz ni laki moja mgodini
sokoni dar ilikua laki na 25 japo aitabirik muda wowote ina change kama dola
Alafu ni kijana wa 20+ saiz yupo msumbiji wiki hii anazama dar tena kuuza mzigo

We ulianza na mtaji wa shingapi uko chunya?
Maana kama Mimi nikiwa na milioni 2 ni gram 20 sasa from msumbiji to dar mhmm Mara kuchomwa gram zishuke kidogo faida itaishia nauli tu

Je huko kujisajili kama mnunuzi shingapi vibali ?
Wewe unauzia wapi dhahabu ?
Ila kiuhalisia huwezi toa dhahabu Msumbiji ukaiuzia Dar ndo maana masoko yamekuwa mengi, umehesabu tu bei ya kuuza hujaweka asilimia ya hiyo dhahabu na 7% ya Serikali na Service Levy. Hivyo haiwezi kuuzwa kwa 125K

Pia kama kainunua kwa 100000 faida yake haitazidi 9000 kwa gram labda asilimia yake iwe 98
 
Songea njia ya muhukulu mitomoni akunaga usumbufu kule Mara zote na kule sio mbali na kuna usalama kule mpakani
Kuna kipindi jamaa yangu alianza biashara ya kuwavusha mto Ruvuma pale alipiga Sana hela enzi flani hivi.
 
Hi Nyekundu, ahsante kwa kushare nasi ujuzi wako .
Je huu ni ujuzi wako wa darasani(theory) ama ni practical ? Wewe uliipataje hiyo fursa ya kuingia kwenye madini at that under 25yrs na una muda gani huko, kuna mafanikio unayaona ama bado bado?

Naskia bila uchawi na ndumba huwezi kumake hii biashara, je ni kweli huo uchawi unawasaidia hao? Vipi wewe unaamini na kutumia pia?

Kuna hizo risks tunaziskia wachimbaji wanaangukiwa na vifusi muda mwingine, vipi mnachukua tahadhari gani ama ni tahadhari gani za kuzingatia?

Wanasema pesa zinazopatikana kwenye hii biashara wengi wao hawafanyii vitu vya maendeleo mfano other investments(pesa hazikai yaani) vipi ni kweli? Wewe unajionaje ktk hilo?

Thank you in advance!
Uchimbaji mdogo unahusisha watu wa imani tofauti tofauti, watu hupita kwa waganga ili wasomewe ramani na kutiwa moyo, maana hawana vipimo vinavyoonesha urefu wa mwamba ni kiasi gani kushuka chini.

Maduara kudondokea watu ni kutokana na maduara kuchimbwa vibaya au yako ardhi mbaya na hayajajengewa ili yawe magumu.

Kudondoka kwa maduara pia husababishwa na wachimbaji kuvinja nguzo zinazoshikilia maduara.

Vijana wengi wanaojihusisha na dhahabu wanajenga na kufanya miradi mingine kama kawaida.
Vijama wengine wao hawajishughulishi na kitu wanakula raha kuondoa mawazo na fikra za mambo ya ajabu waliyokutana nayo huko chini....

Maduarani waweza kutana na nyoka ambao hutakiwi waua
 
Kuanzishwa kwa masoko ya kanda kumesaidia au kumeharibu biashara ya dhahabu?
Kumesaidia maana huhitaji broker licence kuuza dhahabu, pia imesaidia maana unaenda sokoni unakuta wanunuzi wengi na bei elekezi imewekwa na serikali hivyo si rahisi kupigwa (JAPO UTAPIGWA TU)
 
Mkuu bei ya dhahabu inashuka nakupanda kila siku nimetok Dodoma leo naomba nifike sokoni na porin maeneo ya chunya nitakupatia bei harisi kuanzia kesho naomba unisamehe sana ndugu yangu sitaki kudanganya
Kwani huna namba za watu makota wenzako uwaulize bei?
Kwani huna namba za Dealers uwaulize bei?
 
Biashara ya dhahabu haina tofauti na beting!!! Wengi tunaliwa anapata mmoja! Invest what you van loose
Biashara ya dhahabu si kamari ila uchimbaji bila kupima ndio kamari maana unawekeza hela hujui zitarudi lini.
Wakati mwingine zinarudi na wakati mwingine hutafika safari
 
Je ni kweli kuwa milima yote anayomiliki Geita Gold mine huko mkoa wa Geita Ina dhahabu nyingi na dhahabu yake inapatikana sio kwenye kina kilefu?
Popote pale unapoona makampuni makubwa yanawekeza jua washapima vya kutosha na wanajua kabisa dhahabu wanaipata umbali gani, wingi gani
Wanapiga bei ya kuzalisha kuona faida itapatikana au lah

Wanakuja piga hesabu za wataila kwa muda gani hiyo dhahabu

GGML wataendelea kuwepo pale kwa muda mrefu mno
 
Soko la dhahabu kwa ajili ya kuja kuuza Dar huwa lipo wapi sasa!? Yani ambapo utanunua kwa jumla uje kuuza kwa faida!?

Vipi kuhusu mambo ya utapeli?
 
Nimesikia kuna vibali vimeanza kutolewa kwaajili ya kuwekeza kwenye refinery za dhahabu, hapo awali dhahabu ilikua haisafishwi.?
Ndio ila refinery ni gharama kubwa sana hakuna Mtz mmoja mmoja anaweza wekeza ndio maana hata hizi zilizoko Dodoma na Mwanza zimewekezwa kwa ubia wa makampuni ya nje na ya ndani pamoja na serikali

Dhahabu pure yatakiwa iwe 999.9 hapo maana yake madini yoooote yametolewa imebakia Dhahabu tu.
 
Hapana dhahabu inasafishwa ila kwa wanunuzi wale wa chini kabisa dhahabu hua inachomwa tu moto bila yakusafishwa na kuuzwa
Jikoni unapoenda choma dhahabu wale wanachoma kwa maximum yao wanaondoa impurities zote ila hawana uwezo wa kutenganisha Cu, Fe, Au etc hiyo ni kazi ya refinery ambazo hutenganisha kila kitu kivyake.

Wao kama Dealers wakimaliza wanaisafirisha Dubai au Hongkong huko inapelekwa refin ery sasa.
 
Ili upewe kitalu cha kuchimba dhahabu INATAKIWA uwe na vigezo gani?
Hupewi Kitalu cha kuchimba
Vitalu vingi vinafanyiwa Utafiti na waliofanya Utafiti huombea Leseni za Uchimbaji ili waweze chimba.

Kabla ya hapo lazima utaonana na wamiliki wa maeneo hayo ili wakuuzie au muingie ubia nao
 
Back
Top Bottom