sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Kuna jirani hapa nilishangaa sana alipomuachisha chuo kijana wake akiwa mwaka wa pili, Huyu kijana alikuwa anasomea degree ya procurement, mzee wake akamwachisha kinguvu.
Nikaja kujua kwamba mzee alikuwa anahofia sana mtoto wake anaweza kutekwa na maisha ya kuajiriwa na kuacha kabisa biashara ya mzee wake ikiwa haina mrithi hasa ikija kutokea kijana kapata ajira mkoa mwengine.
Unaweza leo hii ukawa na biashara na ukapanga kuirithisha kwa watoto lakini elimu yao ikaingilia kidogo huku kwenye biashara tofauti na mtoto ambae shule aliishia au mlifanya aishie huku chini ili mumfundishe biashara.
Mfano leo hii unaweza ukawa una biashara nzuri ina faida ambayo ni mara 5 ya mshahara wa kazi anayoitaka mtoto wako, ila bado mtoto akapenda zaidi kuajiriwa na biashara ikakosa mrithi wa damu yako.
Kiukweli hii inauma, kijana anajazwa sumu huko na wenzake kwamba ajira hio haina risk atapokea mshahara kila mwezi huku biashara inaweza ikafilisika kwa hiyo akatawaliwa mawazo kwamba akomae na ajira, hii sumu ndio ambayo wahitimu wengi inawafanya kupenda ajira.
Je wewe una deal na hii hali vipi