Mwandishi Mwingereza aitwaye Lewis Carroll aliwahi kusema, ''If you don't know where you are going, any road will get you there''.
Wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu, tuliwasikia UKAWA wakimponda mgombea Urais wa CCM kama hana lolote kwa sababu CCM ni ile ile. Kuna wengine walidiriki kusema CCM imeishiwa pumzi na iwekwe kando. Wengine wakasema kama CCM ni kitanda chenye kunguni kama Dk. Magufuli anavyosema, basi wao hawataki kuhangaika kuwauwa kunguni bali watakichoma moto na kununua kitanda kingine.
UKAWA walicheka na kumdhihaki Rais Magufuli aliposema amepania/kudhamiria kuleta mabadiliko bora pindi atakapoingia madarakani kwa kubana matumizi ya serikali, kuongeza mapato ya serikali, kuboresha mfumo wa utendaji na ufanisi, kupitia kodi na ushuru unaowaumiza wakulima, wafugaji na wavuvi, kupitia upya baadhi ya sheria zinazoleta kero kubwa kwa wananchi, kuunda serikali ndogo, kupunguza au kumaliza kero za watumishi wa umma na kupendekeza muundo wa kitaasisi ili kutekeleza kwa ufanisi ahadi zake.
Two weeks down the line, UKAWA kwa sasa wameanza ''kudandia treni'' ya Rais Magufuli kwa mbele wakati huo huo baadhi yao hawajatuambia kama wanamtambua ni Rais wa Tanzania.
Eti wanadai wameanza kumkubali Rais Magufuli kwa sababu ameanza kutimiza Ilani ya UKAWA! Wamesahau ni wiki mbili zilizopita walikuwa wanasema Rais Magufuli hana lolote jipya katika mchango wa mabadiliko bora nchini. Kuna wengine kwa sasa watadai Rais Magufuli ni UKAWA. Wanachofanya kwa sasa ni kutaka kuhalalisha hii dhana ya kuitwa nyumbu na bendera fuata upepo!
Kabla ya viongozi wa UKAWA kuanza 'kudandia treni' ya Rais Magufuli kwa mbele, lazima wawaombe radhi Watanzania kwa kutaka kuliangamiza taifa kupitia mgombea wao wa Urais wa Tanzania ambaye walituletea na kuanza kutuuzia kwenye gunia wakati wanafahamu ni mra rushwa, fisadi na hafai kuwa Rais wa Tanzania.
Mtu muungwana ni yule anayeomba radhi na pia taifa la waungwana ni lile linalosamehe baada ya kuombwa radhi.
UKAWA kabla hamjaungana na juhudi za Rais Magufuli, lazima muombe radhi kwa wapiga kura wengi, otherwise, endeleeni kusimama na Lowassa mkisaidiwa na Ilani yake ya Uchaguzi yenye vipao mbele vitatu, 1)Elimu, 2)Elimu na 3)Elimu.
Kwa wale wanaoamini uwepo wa Mwenyezi Mungu, kwa sasa wanasema Mwenyezi Mungu bado analipenda Taifa letu kwa kutuletea Rais Magufuli.
Kama Magufuli ataendelea hivyo basi watakaoumia ni CCM na sio wapinzani.
CCM miaka yote inawekwa madarakani kwa rushwa na pesa za rushwa zinapatikana kupitia mikataba feki na kufanya manunuzi kwa bei ya kuruka.
Pesa nyingi zinazoiweka CCM madarakani ni zile za kuchota kwenye mashirika ya umma kinyemela.
Sasa kama Magufuli atagoma kufanya huo ushetani uliofanywa na watangulizi wake basi ni dhahiri CCM itaporomoka huku Magufuli akibakia na kura zake mkononi na UKAWA watapaa kwa kasi kwani wabunge wengi walioko CCM wanaingia madarakani kwa mahela ya wizi wanayochoteana huko juu. Ndio maana walinunua masanduku ya ziada ya kura na kupiga kura kabla na kuzigawia kila majimbo .
Hivi leo Magufuli akisema anataifisha Majumba waliyogawana huku serikalini watakaolia ni UKAWA CCM .
Leo Magufuli akisema anawatimua kazi hao wafanyakazi wenye Vyeti feki watakaoumia ni CCM mana watoto wao wengi ndio wamefoji vyeti na wameajiriwa kwenye mashirika na idara mbalimbali. UKAWA watashangilia kuona kuwa walichokua wanakipigania kinatekelezwa.
Amini usiamini baada ya miaka miwili maadui wakubwa wa Magufuli watakua wapo ndani ya CCM.
Vigogo wengi wa CCM ndio wanaomiliki majumba na biashara nyingi za malori.
Leo hii Magufuli akitengeneza Reli na kuboresha usafirishajo wa treni watakaolia na kufilisika ni wanachama na vigogo wa CCM na sio UKAWA.
Leo hii pakiwa na katiba na sheria bora watakaoumia ni CCM maana walishazoea ulaghai na uovu .
Jambo lolote jema litakalofanywa katika hili taifa litawaumiza sana CCM na mabosi wao waliokua wanawakuwadia mali za watanzania. UKAWA hawajawahi kunufaika na mikataba feki na wawekezaji.
Mirija ya unyonyaji ilikua inatumiawa na CCM na watoto wao.
Leo hii kuna wabunge,waandishi wa habari na wanachama wa CCM wanaojifanya sana kumuunga mkono Mh.Magufuli lakini wamelenga madaraka ya uwaziri na sio maemdeleo kwa wananch .Hawa ni wanafiki na wote wako CCM na sio UKAWA.
Hata Kikwete walimsifu na kutoa kila tamko jema juu yake huku wakilenga madaraka na walipopata wakageuza nchi kuwa shamba la bibi.
Baada ya kipindi hiki cha mgao wa vyeo ndani ya serikali ukipita basi hawa apambe watapukutika sana