Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Inasikitisha sana,

Kwanza hio ni sinema tu imetengenezwa, na wamepangwa kufanya hivyo, ili wamkoshe roho Mkuu tu.

Pili, ukijiona unaipenda au unajiunga na CCM, ujue wewe ni mjinga na upeo wako wa akili ni mfinyu mithili ya kokwa la ubuyu, hata kwa maombi maalum hauponi wewe. Hao wenyewe waliopo CCM na vyeo vyao wanatamani kuondoka leo kabla ya kesho waingie upinzani na wengine waanzishe vyama vyao wale ruzuku, ila wanaogopa cha moto.

NB Jiungeni tu salama vijana na CCM, ila chonde chonde mje muanze kulalamika ""ooh hakuna ajira mtaani"" au ""oooh hela ngumu"". Mtafurahi na roho zenu kwa matusi mtakayopata.
 
Hata wasipounga mkono juhudi za Jiwe, 2020 lazima ccm ishinde kwa 99.8% hata watanzania wote msipoenda kupiga kura.
Mbona watu wanapenda kupoteza muda wao bure tu ktk propaganda zisizo na tija kwa Taifa hili.
 
Vijana mbagala wamvaa magufuli daaaah[emoji15][emoji15][emoji15]
 
Umerejesha matumaini kwa wananchi wazalendo na wanyonge ambao walichagua kukaa kimya wakati rasilimali za nchi yao zilipokuwa zinaporwa huku mapato ya kodi zao yakiwanufaisha wachache huku wao umaskini ukiwaandama na kupata huduma duni za afya, elimu, maji nk

Leo tunashuhudia ulivyoamua kusimama kwa ujasiri na upendo mkubwa kwao kuhakikisha rasilimali za nchi yao zinawapa ustawi wa maisha na kuipa nchi maendeleo. Tumeshuhudia namna ulivyoamua kila senti inayoingia serikalini iende kuboresha maisha ya wananchi wako kwa kupunguza kwa kiwango kikubwa matumizi yenye sura ya anasa na ufujaji kwa viongozi wa serikali.

Hakika imani ni amana. Deni la fedha hulipwa kwa fedha, deni la hisani hulipwa kwa hisani vivyo hivyo deni la imani hulipwa kwa imani kupitia mwenendo na vitendo bora kabisa ili kukidhi matarajio ya waliokupa imani, Rais Magufuli umetulipa imani tuliyokupa.

Matokeo ya haya yote tumeshuhudia elimu bila malipo kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne, ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kutoka Dar-Dodoma kilomita takribani 700, usambazaji umeme vijijini kwa gharama nafuu, ununuzi wa ndege sita mpya kwa ajili ya kuliimarisha shirika letu la ndege ATCL, upanuzi wa bandari za Dar es Salaa, Mtwara na Tanga; ujenzi wa miradi ya kuongeza uzalishaji wa umeme nchini kupitia gesi asilia kama kule Kinyerezi II, III, & IV pamoja na maji kama ule wa Stieglers gorge ili kuipa nchi yetu umeme wa uhakika na nafuu. Vile vile tunashuhudia uwekezaji na ujenzi wa viwanda vya kati na vikubwa ukifanyika kwa kasi kubwa maeneo mbalimbali ya nchi yetu hakika unastahili pongezi na sifa.

Kazi yako inastahili heshima mbele za wanadamu na hata mbele za Mungu. Tunakuombea afya njema ili uendelee kuwatumikia watanzania wenzako.

#ChapaKazi
 
Mkuu umesahau weka namba ya Simu waeza pata uteuzi..

Yaan watu wakishajuaga udhaifu wa MTU huutumia ipasavyol
 
Nimeifuatilia kwa Karibu ziara ya Rais Magufuli katika mikoa ya Mwanza, Simiyu, Mara na Singida kwa kweli kasi ya kuibua maovu na kuyashughulikia kwa haraka imenifurahisha sana. Unapokuwa na Rais aina ya Dr Magufuli hauhitaji mwenge wala wapinzani kufichua uovu, serikali inatosha. Niishie hapo!
 
Nyie ndio mnaofanya Trump atuone Waafrika ni useless.

Ndio maana kukawa na viongozi wa chini yake wa kumsaidia.
 
Mkuu duniani hamna case enayo pelelezwa siku moja inasikilizwa siku huyo na inaukumiwa siku hiyo, tena kwenye mkutano wa hadhara hizo ni kiki za kisiasa kwa kiingereza zinaitwa "cheap popularity" tena kibaya zaidi na ma RC na DC wameiga hiyo style RC anakua hakimu katika case ambayo hana utaalamu nao......hilo ni jambo baya sana kwa taifa hili.
 
Hivi kumbe kazi mojawapo ya mwenge ni kufichua mafisadi?
 
Unajitahidi sana, ipo siku na wewe utaonwa kwenye teuzi, endelea na moyo huo huo. Awamu hii inahitaji watu kama nyie.
 
Great thinker
 
Kila dikteta duniani anaamini anatosha mpaka pale akichokwa na iko siku wanachokwa
 
Bado yule aliepiga 1,5t
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…