Napenda niungane na Mamilioni ya Watanzania kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kufanya uamuzi wa Kila mfuko uendelee na kikokotoo Cha zamani Cha asilimia 50 na kibaki hivyo mpaka 2023.
Huu Ni uamuzi wa kiujasiri na wa kihistoria uliopokelewa kwa shangwe na alama isiyofutika kwa Kila Mtumishi. Leo hii Waalimu, Madaktari, Wahandisi, Watendaji na Watumishi wote Ni vicheko vitupu.
Watu waliotumia muda wao, nguvu zao zote, akili zao zote kulitumikia kwa uaminifu Taifa walikuwa walazimishwe kulipwa kidogo kidogo stahiki zao halali Kama vile kustaafu Ni dhambi kubwa wameitenda. Ahsante sana Rais Magufuli kuingilia Kati kwa kuwatetea Watumishi, Mwenyezi Mungu pekee ndio atakayekulipa kwa maamuzi haya yenye tija kwa umma.
Naam! Ni uamuzi wenye tija kwa maana kitendo Cha kuongeza kikokotoo toka 25% hadi 50% utaongeza wigo wa nguvu kazi kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii na kuleta matumaini makubwa kwa Wazee wetu wastaafu hapa nchini.
Pia uwepo wa kikokotoo Cha 50% utaongeza haki ya mikopo ya makazi kwa Watumishi ambao Sasa wataweza kujenga au kununua nyumba Kama awali ilivyokuwa.
Zipo faida nyingi kiukweli. Kwa kifupi, Matumaini ya Wastaafu ama hata ya nguvu kazi zilizopo kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii imerejeshwa Tena na Rais Magufuli.
*Mungu Mbariki Rais Magufuli*
*Mungu Ibariki Tanzania*
*Shilatu E.J*
Sent using
Jamii Forums mobile app