Hasa kwenye mitandao, kuanzia "Shangazi", Miss Sarungi, Miss Ndosi, TLS (ndio), na "the so called" wanaharakati wa "Demokrasia" pamoja na vyama karibu vyote vya ukinzani wanakereka wakikusikia unayapenda na kuyazungumzia mambo haya mazuri, rais wetu JP Magufuli anayofanya, wanakunyamazisha kistaarabu kwa kuongelea swala la uhuru wa habari na demokrasia nchini, wale wachache wasiokuwa na hoja watakimbilia matusi ya kutisha!
Ila JPM hasa kafanya nini? Wanachama wake wanadai kwa miaka 3 tu chini ya utawala wake..
- Kwa kuondoa wafanyakazi hewa na wenye vyeti feki, amelinusuru Taifa kuibiwa na wale wajanja Bilioni 378...
- Amepunguza kwa kiwango kikubwa rushwa iliyokuwa imetawala kwenye kila sekta nchini...
- Kajitahidi kuisafisha TRA...kwa kufukuza na kuwashtaki wahusika...
- Kajitahidi kulinda rasilimali na maliasili zetu...
- Migodi iliyokuwa ikiingiza Bilioni 300 huko nyuma kwa kipindi cha miaka 10 sasa imeingiza Bilioni 194 kwa 2017/18 tu!
- Amepunguza sana ile misafara iliyokuwa haina tija huko na kuokoa mabilioni..
- Huko nyuma kabla ya utawala wake, mapato ya kodi kwa mwaka yalikuwa Trilioni 9, ila sasa yamefikia Trilioni 14!
- Amekaribisha wawekezaji nchini wasiopunguwa 3000!
- Amelifufua shirika la ndege (ATCL) na kununua ndege zisizopunguwa 9!
- Na kwa sasa serikali yake inawekeza siyo chini ya $62m kwa ajili ya bajeti hiyo kila mwaka!
- Tukiingia kwenye miundo mbinu ndiyo usiseme...
- SGR
- Kilometa 19.2 barabara ya Kimara...
- Serikali yake imesaini mkataba kwa kuzalisha umeme Fufiji (HEP) plant ambao unategemea kuzalisha 2,115!
- Ufunguzi wa ujenzi wa daraja la Tanzanite..
- Uwanja wa ndege (Terminal 3)..
- Barabara kem kem na madaraja ya kufa mtu...
Lakini bado tunalalamika! Hasa swala la demekorasia, wakati TZ tofauti na nchi zingine kadhaa kuna makampuni ya magazeti yasiyopunguwa 200 na vituo vya radio na TV pia visivyopunguwa 200! Uo uhuru wa demekrasia hasa na kujieleza tunaoulalamikia ni upi?!