Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Sijasomea uhasibu ila kupata taarifa kamili ya kimahesabu yaani Balance Sheet lazima madeni pia uyajumlishemo.
 
Hakika Rais Magufuli ana uthubutu ambao sijawahi ona...

Kila nikitafakari amewezaje kuyafanya haya kwa muda mchache hivi, tena kwa fedha zetu wenyewe naona watangulizi wake walikiwa wazinguaji sana...

Hapo bado 8 ways, stigler gorge na SGR. Hakika Mungu ampe maisha marefu Rais wetu
Wakati ndani ya miaka 3 Magufuli amenunua ndege ambazo impact yake ni maajaliwa ya Mwenyezi Mungu, aliyemtangulia ndani ya miaka 3 tayari kulikuwa na wanafunzi wa mwaka kwanza UDOM...

Tayari alishamwaga ajira kwenye sekta kadhaa za umma

Tayari alishaanzisha kampeni kubwa ya udahiri wa walimu wanafunzi ili kupunguza tatizo sugu la walimu!!

Na kila ambae alimaliza ualimu, haraka haraka alipata ajira ili akafundishe watoto na ndugu zetu!!

Tayari alishaongeza udahiri wa wanafunzi kwenye fani ya afya... na kila alimaliza, hakubaki muda mrefu mtaani!!

Tayari watumishi ambao walikuwa na elimu ndogo walishapewa opportunity ya kujiendeleza na wale waliotumia fursa, hadi anaondoka madarakani walishakuwa na shahada na wengine masters wakati walikuwa na certificate tu! Na kama kuna ambae JK aliingia akiwa na certificate na hadi anaondoka alikuwa na certificate hiyo hiyo, basi huyo hadi anaingia kaburini, shahada ya chuo kikuu atafanya kuisikia tu!!

Huo ndio uchumi! Uchumi kwa watu na sio kwa vitu; tena vitu visivyo na direct economic impact at large!

Sasa endeleeni kufurahia vitu vya kijinga, na moja ya mambo ya kijinga kabisa ni kununua ndege wakati nchi ina changamoto kibao!!!!!
 
..tangu tununue ndege tumepata FAIDA kiasi gani?

..au tangu tununue ndege serekali imetoa RUZUKU kiasi gani kwa ATCL?

..Je, CAG atatupa majibu ktk taarifa yake inayokuja?

Au atazuiwa kukagua mahesabu ya ATCL?

Cc chige
Mkuu JokaKuu,

Kwenye hili la ndege binafsi sipendi kung'ata meno hata kidogo! Ingawaje kuna baadhi ya mambo sikubaliani nayo kwenye SGR, lakini generally, SGR kwangu ni okay but ndege; HAPANA kwa kweli!!!

Nimefanya study ya kutosha sana kuhusu airline business, and there's no way mtu anaweza kunishawishi kwamba tuna favorable condition kwa hii biashara at least for the next 10 years!!

Mbaya zaidi, uchumi unaojengwa na Magufuli haushawishi kuifanya airline business kuwa competitive business, labda ndo hivyo aendelee kuyatilia fitina mashirika mengine ya ndege kama walivyofanya kwa FastJet... na hicho kitakuwa ni kifo cha ATCL vile vile kwa sababu huwezi kufanya biashara kwa kutegemea mbeleko!

Kuna watu wakisikia ndege ya ATCL inaenda India au Pakistan wanaanza vijembe huku wakidhani ndo tayari ATCL are doing big bila kufahamu that's just an airline route! Kupata route ni jambo moja, kuwa competitive enough kwenye route husika ni jambo lingine!

Why should Kanjbhai board ATCL Plane to Mumbai and not Air India... hili ndilo suala tunalopaswa kujadili!!! Why Should Mr. Abdulhussein Aziz book ATCL plane to Dubai and not Emirates, hili ndilo tunatakiwa kujadili!!!

ATCL wakidhani kupata route ndo wamemaliza kazi, am telling you, kama watakuwa commercially decisive, usije kushangaa wanamwaga manyanga kwenye hizo routes in less than 1 year huku wakianza na kupunguza idadi ya flights!!

Tena bora tungejikita kwenye regional routes and then Africa!
 
Hasa kwenye mitandao, kuanzia "Shangazi", Miss Sarungi, Miss Ndosi, TLS (ndio), na "the so called" wanaharakati wa "Demokrasia" pamoja na vyama karibu vyote vya ukinzani wanakereka wakikusikia unayapenda na kuyazungumzia mambo haya mazuri, rais wetu JP Magufuli anayofanya, wanakunyamazisha kistaarabu kwa kuongelea swala la uhuru wa habari na demokrasia nchini, wale wachache wasiokuwa na hoja watakimbilia matusi ya kutisha!
Ila JPM hasa kafanya nini? Wanachama wake wanadai kwa miaka 3 tu chini ya utawala wake..
  • Kwa kuondoa wafanyakazi hewa na wenye vyeti feki, amelinusuru Taifa kuibiwa na wale wajanja Bilioni 378...
  • Amepunguza kwa kiwango kikubwa rushwa iliyokuwa imetawala kwenye kila sekta nchini...
  • Kajitahidi kuisafisha TRA...kwa kufukuza na kuwashtaki wahusika...
  • Kajitahidi kulinda rasilimali na maliasili zetu...
  • Migodi iliyokuwa ikiingiza Bilioni 300 huko nyuma kwa kipindi cha miaka 10 sasa imeingiza Bilioni 194 kwa 2017/18 tu!
  • Amepunguza sana ile misafara iliyokuwa haina tija huko na kuokoa mabilioni..
  • Huko nyuma kabla ya utawala wake, mapato ya kodi kwa mwaka yalikuwa Trilioni 9, ila sasa yamefikia Trilioni 14!
  • Amekaribisha wawekezaji nchini wasiopunguwa 3000!
  • Amelifufua shirika la ndege (ATCL) na kununua ndege zisizopunguwa 9!
  • Na kwa sasa serikali yake inawekeza siyo chini ya $62m kwa ajili ya bajeti hiyo kila mwaka!
  • Tukiingia kwenye miundo mbinu ndiyo usiseme...
  • SGR
  • Kilometa 19.2 barabara ya Kimara...
  • Serikali yake imesaini mkataba kwa kuzalisha umeme Fufiji (HEP) plant ambao unategemea kuzalisha 2,115!
  • Ufunguzi wa ujenzi wa daraja la Tanzanite..
  • Uwanja wa ndege (Terminal 3)..
  • Barabara kem kem na madaraja ya kufa mtu...
Lakini bado tunalalamika! Hasa swala la demekorasia, wakati TZ tofauti na nchi zingine kadhaa kuna makampuni ya magazeti yasiyopunguwa 200 na vituo vya radio na TV pia visivyopunguwa 200! Uo uhuru wa demekrasia hasa na kujieleza tunaoulalamikia ni upi?!
 
Hasa kwenye mitandao, kuanzia "Shangazi", Miss Sarungi, Miss Ndosi, TLS (ndio), na "the so called" wanaharakati wa "Demokrasia" pamoja na vyama karibu vyote vya ukinzani wanakereka wakikusikia unayapenda na kuyazungumzia mambo haya mazuri, rais wetu JP Magufuli anayofanya, wanakunyamazisha kistaarabu kwa kuongelea swala la uhuru wa habari na demokrasia nchini, wale wachache wasiokuwa na hoja watakimbilia matusi ya kutisha!
Ila JPM hasa kafanya nini? Wanachama wake wanadai kwa miaka 3 tu chini ya utawala wake..
  • Kwa kuondoa wafanyakazi hewa na wenye vyeti feki, amelinusuru Taifa kuibiwa na wale wajanja Bilioni 378...
  • Amepunguza kwa kiwango kikubwa rushwa iliyokuwa imetawala kwenye kila sekta nchini...
  • Kajitahidi kuisafisha TRA...kwa kufukuza na kuwashtaki wahusika...
  • Kajitahidi kulinda rasilimali na maliasili zetu...
  • Migodi iliyokuwa ikiingiza Bilioni 300 huko nyuma kwa kipindi cha miaka 10 sasa imeingiza Bilioni 194 kwa 2017/18 tu!
  • Amepunguza sana ile misafara iliyokuwa haina tija huko na kuokoa mabilioni..
  • Huko nyuma kabla ya utawala wake, mapato ya kodi kwa mwaka yalikuwa Trilioni 9, ila sasa yamefikia Trilioni 14!
  • Amekaribisha wawekezaji nchini wasiopunguwa 3000!
  • Amelifufua shirika la ndege (ATCL) na kununua ndege zisizopunguwa 9!
  • Na kwa sasa serikali yake inawekeza siyo chini ya $62m kwa ajili ya bajeti hiyo kila mwaka!
  • Tukiingia kwenye miundo mbinu ndiyo usiseme...
  • SGR
  • Kilometa 19.2 barabara ya Kimara...
  • Serikali yake imesaini mkataba kwa kuzalisha umeme Fufiji (HEP) plant ambao unategemea kuzalisha 2,115!
  • Ufunguzi wa ujenzi wa daraja la Tanzanite..
  • Uwanja wa ndege (Terminal 3)..
  • Barabara kem kem na madaraja ya kufa mtu...
Lakini bado tunalalamika! Hasa swala la demekorasia, wakati TZ tofauti na nchi zingine kadhaa kuna makampuni ya magazeti yasiyopunguwa 200 na vituo vya radio na TV pia visivyopunguwa 200! Uo uhuru wa demekrasia hasa na kujieleza tunaoulalamikia ni upi?!
Orodhesha na waliouawa/walioonewa etc kwa utawala wake. Ukimaliza hili kulijibu, then come again tujadili yote kwa pamoja
 
Data zako zinafanya niwe na wasiwasi na bandiko zima! Kanunua ndege ngapi unasema? Hao wawekezaji 3000 mkuu wa wapi? Nilidhani wamepungua kwa sasa!

By the way, hivi Rais akitekeleza kujenga miundo mbinu si ndio kazi yake inayompa mshahara?

Samahani lakini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona hujaweka

1. Waliopotea/kuuwawa kisiasa ndani ya awamu yake.

2.Sakata la Makinikia.

3.Sakata la Sukari?

4.Sakata la Koroshow?

5. Msafara wenye gharama kuliko awamu zote?

6.Doule Standard dhidi ya vyeti feki vya DAB.

7.Miswaada ambayo hata chekechea asingepitisha.

8.Kuganda kwa madaraja na ongezeko la mishahara ya watumishi.

9.Ufisadi wa 1.5trl.

10. Ukabila ktk teuzi.

11. Double Standard ktk uwajibishaji wa wateule wake mf Anna Kilango/Kitwanga/RC Mkuu.
 
Rais Magufuli
🇹🇿Tar. 2. 12. 2018 ameweka jiwe la msingi mradi mkubwa wa maji safi kwa jiji la Arusha, utatoa lita mil. 208 kwa siku tofauti uwezo wa sasa wa lita mil. 94 kwa siku, unagharimu Bil. 520, wanaufaika ni wananchi mil. 1.934 , utakamilika Juni 2020 na utajumuisha maeneo yote ya Hai, Simanjiro na Arusha.

Tar. 10. 12. 2018 amegawa jumla ya vitambulisho laki 6.1 kwa wamachinga ili kuondoa adha kwa wajasiriamali wadogo, kwa hatua ya awali kila Mkoa umepata vitambulisho elfu 25.

Tar. 12.12. 2018 ametia saini ujenzi wa mradi mkubwa na wa kihitoria wa umeme wa Stiegler's Gorge utakao zalisha umeme MW 2100 mara 2 zaidi ya umeme wote wa sasa, mradi huu umegharimu Tirioni 6.2, unataraji kukamilika ndani ya miezi 36, ambapo utaifanya Tanzania iwe yenye umeme nafuu na wa uhakika kwa matumizi ya nyumbani na Viwandani.( Tafsiri sahihi ya Tanzania ya Viwanda). Mradi huu haujawahi kufanywa Afrika mashariki na Kati, ila ni Tanzania pekee imethubutu mradi wa kiwango hiki.

Tar. 18. 12. 2018 ameweka jiwe la msingi eneo la Kimara stop Over Jijini Dar Es Salaam katika barabara ya Morogoro (Kimara- Kibaha 19.2 km) ujenzi wa Barabara 8, madaraja 6, makalavati 36, na ujenzi wa Flyover eneo la Kibamba Hospitali kwenye makutano ya barabara ya Mloganzila na Bunju. Mradi huu utakamilika ndani ya miezi 36, na unagharimu sh. Bil. 141.56 fedha za walipa kodi.

Tar. 20. 12. 2018 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja jipya la "Selander Bridge" linalounganisha eneo la Agha Khan na Coco beach Jijini Dar Es Salaam ili kupunguza msongamono barabara ya Ali Hassan Mwinyi. Daraja lina urefu wa 1030M, upana 20.5M na njia nne za magari na mbili za miguu ambapo linajengwa na barabara unganishi zenye urefu wa Km 5.2. Limegharimu sh. 256 Bil. Litakamilika ndani ya miezi 30 na litadumu kwa miaka 100.

Tar. 23. 12. 2018 amepokea Ndege ya tano kati ya saba aina ya Air bus New Brand A220-300 ambayo ndio ya kwanza Afrika na yenye uwezo wa kubeba abiria 134.

Tar. 11.01. 2019 amepokea Ndege pacha ya Airbus A220-300 kutoka Kanada na kufanya shirika letu kuwa na ndege sita ambazo zote zimenunuliwa kwa fedha taslimu za Walipa kodi wa Tanzania chini ya usimamizi madhubuti wa Rais Magufuli, ambapo kwa mara ya kwanza tarehe 6. 01. 2019 usafirishaji wa nyama ya Mbuzi umefanyika kutoka Mwanza kwenda Dubai kwa kutumia ndege za Air Tanzania hivyo ujio wa ndege hizi utaimarisha zaidi biashara za kimataifa na hasa Utalii nchini.

Tar. 11. 01. 2019 ametoa ndege za Rais mbili kati ya tatu zilizopo, zipakwe rangi ya Air Tanzania zianze kufanya kazi za kusafirisha mizigo na abiria ziongeze chachu ya uimarikaji wa shirika letu la Ndege (ATCL). Jambo hili halijawahi kufanywa na Rais yeyote Duniani ila limewezekana kwa Rais John Pombe Joseph Magufuli.

Tar. 11. 01. 2019 amefanya mazungumzo na kampuni ya Airtel ambapo kampuni hii kwa miaka 10 haikuwa ikitoa gawio kwa Watanzania kutokana na hisa zetu tulizonazo. Kampuni itaanza kutoa gawio kwa watanzania, na hisa za Watanzania kwenye Kampuni ya Airtel imeongezeka baada ya mazungumzo, kutoka 40% hadi 49% na wao watabakiwa na 51% kutoka 60 za awali. Hii ni muendelezo wa uwekezaji wa faida kwa pande zote (win win situation) na huu ndio muelekeo sahihi wa Maendelea ya Nchi.

Binafsi naiona Tanzania ya tofauti miezi 30 ijayo, tuendelee kuwa wamoja na tufanye kila jitihada kuilinda Tanzania yetu na kumlinda Rais wetu.
 
Sema lingine tofauti na haya
1.kudhibiti madawa ya kulevya
2.kupunguza ujangili
3.kurudisha ardhi iliyohodhiwa na wenye hela
4.kuondoa watumishi hewa
5.kupunguza ufisadi(mpaka mahakama ya mafisadi imekosa kesi)
6.kupunguza ujambazi
7.kulinda rasilimali madini
8.kupunguza matumizi mabovu kwa serikali
9.kuwajali wakulima kuhakikisha wanafaidika
10.kurejesha nidhamu katika taasisi za serikali mpaka kufanikiwa kuongeza mapato
11.kufufua ATCL
Sasa Ni zamu yako kutaja ya kwako ambayo Bado Magufuli hajayafanya na akiyafanya tu ndio utaanza kumkubali na kuamini Kama Ni mzalendo wa kweli aliyejitolea kwa taifa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivyo alivyovifanya vinatosha sana...kwa upande wangu natamani raisi aanze kula bata tu
 
Kufungwa wapinzani na wale wanamkosoa.
Kununua madiwani na wabunge.
Kupanda hali ya uchumi kukua kwa kasi
 
Kwanza Amfute kazi kazi Mkuu wa Jeshi la Polisi kwa kushindwa kufanya uchunguzi kubaini waliohusika na mashambulizi ya risasi kwa Kaka Tundu lissu pamoja na matukio ya watu kupotea, na kutoa maelekezo kwa Mkuu Mpya wa Polisi kuhakikisha uchunguzi unafanyika na wahusika kupandishwa vizimbani kukabiliana na Mkono wa Sheria.

Aende Mbele na kumuelekeza waziri wa mambo ya ndani kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa haraka na kama inahitajika asisite kuomba msaada wa mashirika ya kipelelezi ya Kimataifa.
 
Mosi, Aache kuzuia mikutano ya hadhara

PILI, Bashite amchukulie hatua kwa Vyeti feki na kuvamia Radio

Tatu, Apandishe mishahara hasa kwa waalimu.
 
Umeshindwa kueleza ELIMU? kwasababu ndio jambo kubwa kwa nchi.

Elimu yenu ya nadharia, mtaala wetu sawa na soko chafu.

Mwisho hela zenu 1.5T zipo kwenye kitanda chake.
 
Back
Top Bottom