Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Hizi harakati za wiki nzima Ikulu ni kupotezea issue ya CAG kwenye jamii, na kweli wamefanikiwa.
 
Furaha ya kuwafukarisha watanzania mpaka wakose hela ya kula,kuteka,kuua,kufunga kwenye viroba,kufukuza watumishi kwa kuonea eg vyeti feki na darasa la saba madereva,kutopandisha mishahara na madaraja, kuhakiki mashamba ya korosho,kutoajiri kwa miaka3, kesi za uonezi, visasi, kuminya demokrasia,haki za binadamu, kutofuata utawala bora,wizi1.5 tillioni,kutumia pesa bila idhini ya bunge, kuteua viongozi wasio na sifa ma RCna ma DC,kula hela za rambirambi ya wahanga wa kagera, kudhulumu mifugo ya watu kwenye hifadhi,kupima samaki kwa rula, kupunguzs mzunguko wa fedha ,kudhulumu wafanya biashara ya viroba.yapo mengi sana.
 
Yaani hivi tu buku 7 tayari?
 
Naomba utujulishe kuwa ni serikali ya chama gani ilipoteza hizo siha katika nyuso za watanzania
 
Endeleeni kujidanganya hivo hivo halafu muone 2020 wananchi watamuweka Nani madarakani
Relax sasa mkuu mbona wasiwasi mwingi? Mimi nimeongelea utaratibu wa malipo ya posho, vyuma vikazwe zaidi ili tuongeze mapambio na tuzivune kwa uhalali kabisa hizo buku07 zetu ambazo ni kodi zetu wenyewe, tayari wewe umerukia 2020 bila kujua hata kesho ni nini kinaweza kutokea. Je uchaguzi ukifanyika 2022 kama tunavyoanza kuandaana kisaikolojia?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani sijuwi Lissu huko aliko yu hali gani kwa sasa, jamaa kajilostisha sana juzi kwenye ile interview.....mtu anaulizwa maswali simple tu yeye anaropoka na kutaka kulia huku akitoka nje ya mada. Kama hajajiua basi atakuwa ICU kanaswa na kidole tigoni wakati anajipiga usiku ule kwa hasira zake.
 
Tumeona ulianza na wasomi ,baraza la mawaziri ,ndani ya baraza ni kuanzia Dr na ma Professor, hapo ukawafunga midomo kila mmoja akabaki ana subiri kama vile fisi alivyo subiri mkono wa binadamu kuwa huwenda utadondoka ili autafune, zaidi ukawingizia kale kaujanja ka utumbuaji, ukawa unatumbua asubuhi Dr na jioni ameingia Pr, kwa hilo ndo ukawamaliza kweli kweli.
Ukaona bado , ukaja na uanzishaji watume mbali mbali za uchunguzi zilizo husu mali zetu hasa kwenye sekta ya madini ambayo mabeberu walikuwa wajichotea wanavyo taka.
Hizi tume zika jaa wasomi , lo hapo ndo kabisa ukamaliza mchezo, wote wakaamua kwa dhati kabisa kukutungia wimbo wa kukusifu ili waendane na kasi yako ya uteuzi.
Ulipo ona kawimbo kao kamechanganya ukawaandalia kongamano pale chuo kikuu , ili watanzania wote sasa tuusike huo wimbo, na kweli ulikuwa wakuvutia sana make ulijaa sifa mwanzo mwisho.
Kwa hili kwanini tusikupongeze ? Ukaenda mbali sana ukaona wengine kila siku wako kwenye vyombo vya habari kazi yao ni kukiongelea chama vibaya, hao nao ukawarushia chambo cha madaraka ndani ya chama, bila ya kujitambua wakakimeza, hao sasa ndio wamekuwa wapiga debe wazuri ndani ya chama.
Kwa nini tusikupongeze kwa hili pia ?
Huko umemaliza.
Majuzi tumeona viongozi wa dini nao tayari umesha washika tena wao sasa ni kwa kikombe tu cha kahawa .
Ile habari kila wakati kukicha wana waraka tena kwa kushindana hawa wakiandika huu kesho yake wengine nao wana amka na huu, lililo baki tunashuhudia wale walio kuambia ukatubu sasa wanatubu wao.
Kwa nini tusikupongeze kwa hili nalo?
Umewafanya kuwa na wimbo mmoja wa sifa.
Oooh nilitaka kusahau , kwenye vyama vya upinzani wale vihere here wote ukawavuta , na kuwapa nafasi za kuwa Ma DC, RC, Makatibu kwenye wizara, na hata Uwaziri kabisa, kwa madiwani na Wabunge ukaja na ile Sera ya kata mti panda mti.
Hongera sana kwanini tusikupongeze kwa hili pia ?
Kwa wale vichwa ngumu ndani ya upinzani wasio taka kukuimbia nyimbo za sifa wao ukaona ni vema wakajifunze kutunga nyimbo hizo wakiwa lupango, tena kabla uliwatumia ujumbe kupitia yule rafiki yako , ukimwambia awafikishie ujumbe kuwa waache vihere here wataishia kwenye vyuo vya mafunzo ,na ndivyo ulivyo Fanya ,sasa ni kwa nini tusikupongeze?
Asiye taka kukusifu na kukupongeza huyo ana lake jambo.
Nasema tena hongera Mr president umefaulu kwa hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera sana Rais John Pombe Magufuli Kwa Ujenzi wa Stiegliers gorge, Komaa Kazi Ifanyike usiku na Mchana,Na Atakae Fanya any Delay Muondoe au Kuhujumu,Wananchi Tunataka Umeme nafuu,Biashara zikue.

Yaani Kati ya Yoooooote shikilia hapa hapa. Ukianguka kwenye Huu Mradi. Umekwisha na hakuna atakaekuthamini wala Kukukumbuka RAIS Dr.JOHN POMBE MAGUFULI! Tena Na Ubora wa Kazi Uwepo!

Tafuta Consultant wa Kukagua Mradi huo ukichanganya na Wazawa wazoefu!
Wapo,Mabwawa tunayo!

Peleka watu waende nje wakajifunze,
Umeme unagusa Maisha ya Kila Siku ya Watanzania 95%.

Fanya Kila Uwezalo Mradi huu Ukamilike tena Kwa Wakati!
BIG UP!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…