Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Umesahau kuweka namba yako ya sim tu
Kwenye uzi wako

Ova
 
Bila kuthamini HAKI na UTU wa binadamu wenzake mengine yote ni batili chini ya jua.
 


Wananchi Wilayani Maswa Mkoani Simiyu wamempongeza Rais John Pombe Magufuli kwa kutekeleza ahadi aliyoitoa wakati wa ziara yake mkoani humo mwaka jana ya kuwajengea barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 1.5.
Wakizungumza Mtanzania leo Mei 22 mara baada ya Mwenge wa Uhuru kukagua barabara hizo wamesema wameridhishwa na kasi ya ujenzi ya barabara hizo zilizosimamiwa na wakala wa barabara za mjini na vijijini (TARURA) ambazo zimewekewa taa ili zitumike pia nyakati za usiku.

‘’Tunamshukuru rais Magufuli kwa kutekeleza ahadi yake alipokuwa wilayani Maswa na sisi kama wananchi tunamwahidi tutaitunza na kuifanyia usafi ili idumu kwa muda mrefu na wananchi waone manufaa ya barabara hizi za mitaa,’’ amesema Mercy Emmanuel.

Naye kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Mkogea Ally amewashukuru viongozi wa serikali katika wilaya hiyo kwa kusimamia ipasavyo ujenzi wa barabara hiyo uliozingatia viwango vya kiuhandisi na kufikia asilimia 98 ya ujenzi wake.

SOURCE: MTANZANIA DIGITAL
 
Tumechoka dharau kutoka kwa vijinchi vidogovidigo mh. Raisi turudishe kwenye chati ya Afrika turudishe heshima we are big nation.
Kweli kabisa eti kiji nchi km Rwanda kipind cha kikwete kilikua kinamdharau kikwete na nchi kwa ujumla kwa kashfa nzito ila jamaa mchomba magu karudisha heshima kwa uchumi tulio nao Rwanda it must just dream out haiwez tupata.Halla magufuli
 
We ndo lofa kweli! Yaani hadi leo hufahamu kwamba akiondoka ndipo akina nyie mtakavyojua huyu mnayemshangilia ni mtu wa aina gani kwa sababu hapatakuwa tena na mtu wa kuficha maovu aliyofanya! Mkapa wakati yupo madarakani alifikia hadi kujiita eti Mr. Clean! What happened baada ya kuwa ameondoka?!

Ndipo tukaja kufahamu mambo ya EPA!
Ndipo tukaja kufahamu mambo ya rada ambayo deal ilikamilika kwenye utawala wake!
Ndipo tukaja kufahamu issue ya IPTL ambayo kwa kiasi kikubwa ilivurundwa wakati wa utawala wake!
Ndipo tukaja kugundua amejiuzia mgodi wa makaa ya mawe kule Kiwira
Ndipo tukaja kufahamu wakati akiwa Ikulu alianzisha kampuni ya AnBen!

Hayo ni machache ya makando kando kadhaa ambayo Mkapa aliyafanya lakini kutokana na staili ya utawala wake; hayakujilikana! Sasa ngoja Magu aondoke madarakani uone hayo madudu! Sema ndo hivyo tena manake pamoja na madudu yote hayo ya Mkapa lakini kuna malofa utawasikia Mkapa was best president!!
 
Unashangaa nn sasa? SA si wana balozi wao hapa Tz? Wanatujua tunapenda nn hasa kwa wakimbiza ligi ya sasa....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…