Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

 
Well said mkuu na wenye masikio na wasikie hasa hao vibaraka wa mabeberu. Mh. Rais yeye aendeleee kupiga kazi atuachie sisi hawa vibaraka tunawamudu hasa wa hapa JF.
 
ujenzi wa Chato International Airport pesa zake zilipitishwa kwenye budget ipi labda kwa mfano??

Tuanzie hapo kwanza.
 
Na Emmanuel Shilatu

*A: UADILIFU*
1. Mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi.

2. Wanaotuhumiwa kwa ufisadi Papa na ulaji rushwa wamepandishwa Mahakamani

3. Ameimarisha uwajibikaji, uadilifu na uchapa kazi kwa Watumishi wa umma nchini.

4. Kufufua Mashirika ya umma yaliyokuwa taabani. Mfano shirika la ndege, shirika la simu.

5. Amefanya uchunguzi wa rasilimali za Taifa na kuweka makubaliano mapya kwenye sekta ya madini.

6. Amedhibiti madawa ya kulevya.

7. Tembo na Faru wameongezeka kuashiria kupungua kwa biashara ya nyara za Serikali.

8. Ameimarisha mahusiano mazuri na nchi jirani.

9. Ameweka uwazi wa taarifa na udhibiti wa rasilimali za Taifa.

*B: UZALENDO*
1. Elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari

2. Kupunguza uwepo wa matabaka ndani ya jamii.

3. Ujenzi wa mradi mkubwa wa Mto Rufiji wa kuzalisha umeme zaidi ya Megawatts 2115.

4. Kudhibiti matumizi ya hovyo ya fedha na fedha kuelekezwa zaidi kwenye miradi ya kimaendeleo.

5. Kusimama ukusanyaji na matumizi sahihi ya kodi. Makusanyo yameongezeka kutoka Tsh. Bilioni 800 hadi kufikia Tsh. Trilioni 1.3 kwa kila mwezi.

6. Kudhibiti vyeti feki na mishahara hewa na kubaki historia nchini.

7. Ameimarisha UZALENDO nchini.

8. Amerudisha mashamba na viwanda vilivyobinafsishwa na havikuendelezwa.

9. Amedhibiti usafirishwaji wa makinikia na hayaendi kuchenjuliwa tena nje.

*C: UCHAPA KAZI*
1. Serikali kuhamia Dodoma

2. Ujenzi wa reli ya kisasa ya umeme ya SGR

3. Ujenzi wa viwanda vipya zaidi ya 3000.

4. Uimarishwaji wa amani na Uhuru wa kidemokrasia ndani ya nchi. Mathalani Umoja wa Mataifa (UN) umempongeza Rais Magufuli kudumisha amani na usalama ndani na nje ya nchi.

5. Amesimamia vyema ukuaji wa uchumi uliokuwa na kufikia 7.1%

6. Ujenzi wa vituo vya afya kila kata na ujenzi wa Zahanati kila kijiji.

7. Amedhibiti maandamano ya kisiasa na ya kijamii (Mf. Wanafunzi, Madaktari) na sasa yamebaki historia.

8. Amenunua ndege mpya 6 za kisasa na Leo hii ATCL imefufuka inachanja anga za kitaifa na kimataifa.

9. Ujenzi wa flyover ya Tazara na interchange ya Ubungo.

Itaendelea ...

*Na Shilatu E.J*

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua maana ya Mwamba wa Africa?

Jiwe is not Kelvin, he is John with Jiwe characters behind the scene!

Sema hiv Jiwe ni mwamba wa chato!
 
Watoto, wajukuu wa mafisadi au mafisadi wenyewe watakuja kupinga mirija imekatwa hakuna tena na hata tokea kama Magufuli ni mpango wa mungu
 
Tatizo lake kubwa ni kuruhusu vyombo vya dola kuwatoa roho na kuwatesa wanaomkosoa pale anapokosea..Akubali tu yeye ni mwanaadamu ana sifa ya kukosea
 
UPUUZI MTUPU! mwizi, mzinzi, muongo, fisadi, mbadhirifu, mtekaji, mtesaji, mbambakiaji kesi FAKE na MUUAJI. Mtu hatari sana kwa mshikamano na amani ya Watanzania na janga kubwa la Taifa.

 
Sifa tatu za kokoto
1. Kujengea vyoo
2. Kujengea kuta
3. Kujengea barabara
 
Reactions: BAK
Watakuja wale jamaa wa ufipa street watakwambia uende ukachukue buku saba pale Lumumba.

Yaani yote hayo uliyoyaandika thamani yake ni malipo ya shilingi elfu saba tu!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…