Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Unaweza ukawa uko sahihi kwa unachokiongelea katika uzi wako huu. Hata hivyo, sioni sababu ya kuanza kuwatukana wale unaodhani wana mawazo kinzani na yako. Maendeleo huanza kwa mawazo fikirishi na kinzani, jifunze kuheshimu wenzako.
 
Fanya mambo mawili,la kwanza kajifunze kuandika,la pili Ben Saa8 yuko wapi?
 
Uko sahii mkuu ila namwomba Rais Magufuli asifanye makosa ya Moses.

Moses aliwaahidi waisraeli kuwapeleka Kaanan matokeo yake wakaishia jangwani kwenye Milima ya Sinai, kitu ambacho kiliwafanya waisraeli wengi kuchanganyikiwa na kutamani kurudi tena kwa wamisri.

Rais Magufuli ndiyo na sikatai, anajitahidi sana kama kiongozi mwafrika anajenga majengo mazuri na ya kuvutia, mabarabara kila sehemu na madaraja mazuri pia, ndege zetu na SGR pia Umeme wa Steaglers Gorge.

Walakini ambao upo ni kwamba watu wengi mijini hawana kipato na ili wawe na kipato wanahitaji ajira. Hapo sasa ndipo vijana wengi wa mijini wanashindwa.

Simlaumu Rais wetu, ila kuna kitu kimoja tu ambacho hajakiona bado. Ningemshauri kuwaangalia wajerumani mashariki na ajiulize kwanini wao pamoja na jitihada zote za serikali ya ujerumani na wananchi wake wamezifanya financialyy na morally kuboresha hali ya maisha ya wa east german, imeshindikana. Usoshalist umewalemaza.

Tanzania tunahitaji generation nyingine. Generation ya Mwalim Nyerere na hii ya miaka 30 ya Mwinyi, Mkapa na Kiwete Ni Generation ambazo ni mzigo kwa Rais. Hazita msaidia kitu. Ni mazezeta sisi. Tumezoea vya dezo. Hatujui kujituma na kuchangamkia fursa.

Geration zetu ni sawa swa na kumpigia mbuzi gitaa. Hatutakuelewa. Sisi wengi wetu ni mazombi tunao subiri kuzikwa milele.

Haiwezekani takribani miaka 3.5 sasa unatupigia kelele zilezile kila mara tuchnagamkie fursa, matokeo ni sawa sawa na zero.

Rais Magufuli badili strategy. Kuna kitu hapa hakija kaa vizuri hapa.
 

Hata akina Mkapa na JK walikuwa na wapambe wenye maslahi binafsi na madaraka yao hao waliowapamba. Hapo hakuna jipya na hao waliyofanya ili kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa anayewapeleka chooni.
 
Ni Tz ya sheria na haki, mkubwa na mdogo kuheshimiana. Hakuna tena usemi "unanijua mimi ni nani? " big up JPM
 
Mkuu, haya yote unayoyaona ndivyo haswa hupaswa kufanyika ktt ulimwengu wa kistaarabu, ingawaje bado kuna mapungufu na kasoro nyingi ndani yake. Pamoja na wananchi kubanwa kwa kulipa kodi nyingi, bado tu kuna watu wa aina yako wanaona utendaji wa serikali iliyopo madarakani kama ni muujiza badala ya wajibu wake. Bro, naomba tuwe wa kweli tu.
 

Mapungufu hayakosekani labda tuhamie mbinguni. Muhimu, kwa uungwana, ni kupambana yarekebishwe
 

Cha ajabu anayesifiwa anajua nyingi ya sifa ni za uongo kwakuwa mambo sio mazuri kwa hivyo, lakini hata yeye amejikuta anaamini propaganda hizo kwani wanaotoa sifa hizo ni watu wenye akili timamu.
 
Ni Tz ya sheria na haki, mkubwa na mdogo kuheshimiana. Hakuna tena usemi "unanijua mimi ni nani? " big up JPM

Hizi lugha zipo, sema zimehama toka kwa watu wenye pesa zimehamia kwa viongozi wa serikali kama maDC, RC,s na wanaccm waandamizi.
 
Kumbe anavikwa na maboya alowateua, ???
Watamlamba sana miguu hao maboya, na wengi wao ni Wasukuma
 

 

 
Muongo aliyekubuhu HAACHI ASILI YAKE.


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…