Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Unalipwa kiasi gani wewe kwa siku na huyo magufuli wako? Maana muda wote unawaza kumsifia, kumsujudia, kumpamba na kumtukuza tu! Hivi huchoki?
Na wewe unalipwa kiasi gani kumpinga Magufuli?hiv uchoki Kupinga Kila kitu kizuri anachofanya Magufuli?
 
Kutokana na kukosekana kwa uwazi, hadi Mkapa anaondoka madarakani Watanzania hawakujua lolote kuhusu Radar, EPA, Deep Green, Kagoda, Meremeta, na kashifa zingine kadhaa!!!

Hatukufahamu hata Mkataba wa IPTL ulivyokuwa unachezewa mara kwa mara!! Hatukujua hata Mkapa alivyoamua kujiuzia mgodi wa Kiwira let alone kuanzisha AnnBen Company pale Ikulu!

Na kutokana na kukosekana huko kwa uwazi, hadi Mzee Mkapa akawa anatamba kwamba yeye ni Mr. Clean, na watu wakamuamini kwamba ni Mr. Clean! Ni yale yale ya Magu kujiona ana sifa za kuwa kiongozi wa malaika, na kustahili kuongoza kwa miaka mingi zaidi kwa sababu akiondoka yeye, wengine hawataweza kufanya kama yeye!!!!

Alipoondoka madarakani, salaleeee!!!

Ndipo ikaja kugundulika ni namna gani serikali ya Mkapa ilivyokuwa inaficha ufisadi wa kutisha!!

Na hilo la kukosekana uwazi kwa sasa lipo maradufu!! Wanapotaka kupeana tenda kwa ushikaji, vinawekwa vigezo vya kikanda ili kuwaondoa wasiotakiwa kama ilivyokuwa imewekwa vigezo vya kumtafuta Contractor wa kujenga Chato International Airport!

Wenye akili zao, wakajua kabisa hili shavu anaandaliwa Bwana Steven Makigo, Swahiba Mkuu wa Magu tangia wakiwa Lake Secondary School!

Bwana Stven Makigo yule yule ambae alivutwa na Magu kuwa Mjumbe wa TEMESA na miezi michache, TEMESA ikapewa sahavu la kununua kivuko cha MV Bagamoyo!!

Kila mmoja anafahamu kilichotokea kwenye MV Bagamoyo!!

Sasa ikiwa yote hayo yamefanyika, tutajuaje ikiwa huko behind the door hayafanyiki mambo ya hovyo zaidi?

Unaweza kutudadavulia hapa mchakato wa ununuzi wa ndege ulivyoendeshwa?!
 
Mimi silipwi na yeyote Mkuu,Mimi Uongozi wa Magufuli umerufidisha uzalendo wangu anafanya mambo makubwa mno
Unalipwa kiasi gani wewe kwa siku na huyo magufuli wako? Maana muda wote unawaza kumsifia, kumsujudia, kumpamba na kumtukuza tu! Hivi huchoki?
 
Na wewe unalipwa kiasi gani kumpinga Magufuli?hiv uchoki Kupinga Kila kitu kizuri anachofanya Magufuli?

Kumbe mko wengi hivi! Hebu nijibu basi kwa niaba ya ndugu yako Mikocheni Junction. Huwa mnalipwa kiasi gani kwa siku, saa, wiki, mwezi, nk. Na huwa hamchoki kumsifia?
 
Mimi silipwi na yeyote Mkuu,Mimi Uongozi wa Magufuli umerufidisha uzalendo wangu anafanya mambo makubwa mno

Acha uongo mkuu! Wenzako wanakula buku 7 kwa siku! halafu wewe unafanya kazi bure? Nenda faster Lumumba ukachukue mafao yako. Unafanya kazi kubwa sana.
 
Kumbe mko wengi hivi! Hebu nijibu basi kwa niaba ya ndugu yako Mikocheni Junction. Huwa mnalipwa kiasi gani kwa siku, saa, wiki, mwezi, nk. Na huwa hamchoki kumsifia?
Acha watu watoe hoja zao kwa uhuru usipende Sana kuzimisha mawazo yako yawe sawa na wengine
 
Inamaana huyo jamaa angeendelea kuingia atm na bar kwa miaka mngine mitano ungekuwa na hali gani?
 
Mkuu usipaniki! Nimeuliza tu maswali ili nifahamu. Natambua praise team mnafanya kazi kubwa sana.
Kwani yeye akimsifia wewe inakuuma Nini au unapungukiwa nini? Mbona yeye hajakuingilia kwa kitendo chako Cha kumponda magufuli.wote tuna id fake na hatujuani sasa kwanini unamwambia mwenzako analipwa?
 
Reactions: nao
 

Attachments

  • VID-20191016-WA0019.mp4
    815.6 KB
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Huyu mzee anajitahidi ingawa hali ya maisha ya wananchi haijabadilika bado.
Nilikuwa nampinga kila leo kwa miaka 3 au 4 mfululizo but now nimeona ngoja nimuunge mkono.
CCM siiungi mkono maana ndio iliyotuharibia nchi yetu kwa ufisadi na undugu.
Nilikuwa na sababu lukuki za kumpinga huyu mzee ila sasa nimepata sababu zenye nguvu za kumuunga mkono na mguu ikiwezekana.
Sasa nitaanza kumpigia kampeni kila kona na ikiwezekana atawale 15 yrs.
Najua nina nguvu ndogo ktk jamii ila ninauwezo wa kumwongezea kura mia moja 2020 kwa kampeni nitakayompigia kazini na mitaani.
Leo najisikia kumuheshimu sana hadi title yangu nimemwita kwa majina yake yote kamili. Kuna jambo kanifurahisha sana.
Simuhukumu asiyemuunga mkono ila ninamtaka achunguze na kuzipitia upya sababu zake zinazomfanya asimuunge mkono.
2014 nikiwa nafanya kazi BARICK sasa Acacia mgodini Bulyanhulu niliwahi kuwaambia wenzangu kuwa hii nchi tungempata Magufuli ingetulia. Ingawa alipoingia tu baada ya miezi michache 2016 aliposimamisha stahiki za watumishi kwaajili ya uhakiki ndipo nikaanza kumchukia. Sasa simchukii tena.
 
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Yupo Kazini Saa Zote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…