Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Ninafisi nampongeza rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania mhe,john magufuri kwa kazi nzuri inayoonekana machoni mwa watanzania tangu 2016 hadi leo
Magufuli akitoka madarakani yaani kama akitoka madarakani basi watz watamlilia sana kipenzi chao
 
Sasa hivi lengo la serikali ni kutaka wananchi wa kawaida wapate huduma bora zaidi, nampongeza Rais kwa hilo hapepesi macho
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Huyu mzee anajitahidi ingawa hali ya maisha ya wananchi haijabadilika bado.
Nilikuwa nampinga kila leo kwa miaka 3 au 4 mfululizo but now nimeona ngoja nimuunge mkono.
CCM siiungi mkono maana ndio iliyotuharibia nchi yetu kwa ufisadi na undugu.
Nilikuwa na sababu lukuki za kumpinga huyu mzee ila sasa nimepata sababu zenye nguvu za kumuunga mkono na mguu ikiwezekana.
Sasa nitaanza kumpigia kampeni kila kona na ikiwezekana atawale 15 yrs.
Najua nina nguvu ndogo ktk jamii ila ninauwezo wa kumwongezea kura mia moja 2020 kwa kampeni nitakayompigia kazini na mitaani.
Leo najisikia kumuheshimu sana hadi title yangu nimemwita kwa majina yake yote kamili. Kuna jambo kanifurahisha sana.
Simuhukumu asiyemuunga mkono ila ninamtaka achunguze na kuzipitia upya sababu zake zinazomfanya asimuunge mkono.
2014 nikiwa nafanya kazi BARICK sasa Acacia mgodini Bulyanhulu niliwahi kuwaambia wenzangu kuwa hii nchi tungempata Magufuli ingetulia. Ingawa alipoingia tu baada ya miezi michache 2016 aliposimamisha stahiki za watumishi kwaajili ya uhakiki ndipo nikaanza kumchukia. Sasa simchukii tena.
Kimetokea Nini Hadi Sasa hivi unamkubali? Share nasi hapa,Mimi Toka mwanzo namkubali tu linapotokea kafanya Jambo nisilolipenda hua ninajisemea binadamu hatujakamilika ila mengi nayaona mazuri.Mungu ampe ulinzi na afya tele tu.
 
Kimetokea Nini Hadi Sasa hivi unamkubali? Share nasi hapa,Mimi Toka mwanzo namkubali tu linapotokea kafanya Jambo nisilolipenda hua ninajisemea binadamu hatujakamilika ila mengi nayaona mazuri.Mungu ampe ulinzi na afya tele tu.
JPM kanifanya niishi maisha ya unafuu zaidi ya zamani. Pia kajitahidi kuwanyoosha miungu watu waliokuwa wakiyainua mabega yao kisa pesa au vyeo vyao.
Dar es salaam vichochoro vingi vimepigwa mkeka. Haya ni maendeleo.
Kuna mambo kalegea kidogo. Kama maslahi ya watumishi na ajira kwa vijana. Inabidi ageukie haya mambo mawili soon kwa ustawi wa Taifa.
 
Habarini za mchana wanajamvi...

Hakika Mh Magufuli ni kiongozi mwenye nia ya dhati kabisa kuipeleka Tanzania mbele,

Tumuunge mkono atafanya makubwa zaidi ya haya tunayoiona,

Ni kiongozi mwenye commitment kubwa sana, hata ukiwa Baba wa familia na huna commitment familia yako haitokuja kupata maendeleo hata siku moja,

Twendeni na Magufuli ni Kiongozi wa kuigwa,tulimsubiri kwa muda mrefu kiongozi kama huyu tumempata bado tunapiga kelele tutulie huyu ndiye kiongozi tuliyemsubiri kwa muda mrefu

MTU anajenga reli ya standard gauge, MTU anatoa elimu bure,amehamisha serikali Dodoma, Vituo vya afya vinajengwa kila kona,Barabara zinajengwa,nyumba za polisi zinajengwa,tumejenga fly-over, stiglers gorge ects tunataka nini zaidi?

Nani angeweza kufanya haya yote?

Kwamba hatutaki maendeleo?

Nani hataki kodi yake isitumike vizuri?

Magufuli go go go go go go

Tuko nyuma yako...
 
tuwape na hongera walio toa mawazo yao (ilani zao) zilizungumza juu ya elimu bure, kuimarisha kila sekta.

tumpe hongera magu kwa kuchukua yale ya msingi kwenye ilani za wenzake
 
Tumeacha siasa za kujadili masuala ya msingi kama ya kisera au hoja shirikishi kwa ajili ya Ustawi wa Nchi tunaselelekea kwenye siasa mfu


Vitu vyote hivi ni viashiria kwamba Rais Magufuli anafanya kazi vizuri na ni kete nzuri kwake dhidi Upinzani dhaifu kuelekea 2020



Kwenye Medani zote Rais Magufuli amefanya kazi nzuri kiasi kwamba MAFIKIZOLO wamekosa hoja zenye mashiko na kuanza kuzusha vitu mfu


Kwa hili wamezidi kumsafishia njia kuelekea Uchaguzi ujao na hatimaye Wananchi watampa tena ridhaa ya kuongoza 2020 kwa kura za kishindo


Bado tunawahitaji kina Magufuli kila sehemu kuanzia ngazi ya Urais mpaka ngazi ya Serikali ya mtaa ili Tanzania ipae kwenye nyanja zote kama Rwanda na Nchi zingine wanavyopiga hatua



Alex Fredrick

Dodoma
 
Hatukatai ila DADAVUA VEMA, NDANI YA MIAKA MINNE WAMEPOTEA WATU HAO, JE AKIMALIZA KUMI SI TUTAPOTEZA WILAYA NZIMA?
 
tuwape na hongera walio toa mawazo yao (ilani zao) zilizungumza juu ya elimu bure, kuimarisha kila sekta.

tumpe hongera magu kwa kuchukua yale ya msingi kwenye ilani za wenzake

Hakika anastahili pongezi na sehemu ambayo amewamaliza kabisa wapinzani wake ni kwenye kuchukua baadhi ya ilani na kuzitekeleza kwa vitendo
 
Rais Magufuli atashinda kwa kishindo Uchaguzi wowote kwa sababu anawajali na kuwatumikia Watanzania
 
Namtakia Magufuli 15 years. Awamu tatu. Zikatusaidia sana. Vijana wetu wenye umri wa miaka 15 watakapo shika madaraka watakuwa na umri wa miaka 30. Watakuwa wamepikwa na uzalendo wa Magufuli.
Katiba ya nchi hairuhusu. Ilipasishwa jinsi ilivyo kwa malengo na maana kubwa. Izingatiwe hivyo.
 
Mimi nina amimi...hakuna mtu humu mwenye legitimate ya kusema magufuli, kiongozi mbaya...ebu nionyeshe mbadala basi..Chadema..ndo hivyo, ukirudi CAF case ileile...ebu tuache utamani jamani, kama masrahi yako yameguswa kwa sababu nchi inanyoshwa...usipandikize chuki kwa wengine....

Sent from my SM-J600G using JamiiForums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: nao
Madaktari husema,almost kila mtu ana element ya ukichaa..ila wanasema ni hatari zaidi pale afya ya ubongo inapokesekana....vitu vinavyoleta athari hiyo ni pamoja na kumchukia pasipo kuwa na sababu....Magufuli alichofanya ni kutokumwonea mtu aibu..akijipambanua tofauti na viongozi waliopita, hiyo ni talent huwezi kuipata kwa kila mtu...Mimi naombeni watanzania..tujifunze kupenda vya kwetu.. Kwa walioenda nje ya nchi...Image ya Tanzania imebadilika kabisa, Ukisema ni Mtanzania u feel proud....Kipindi kile tulikuwa so inferior as poor country na ombaomba...Let us appreciate , itapunguzia ugonjwa wa ukichaa ambao kila binadamu anao ila umezidiana kiwango..tuache wanasiasa wachumia tumbo..TUFANYE KAZI,JENGA FAMILIA SAIDIA KUJENGA NCHI YAKO.

Sent from my SM-J600G using JamiiForums mobile app
 
Kiwanja changu nimenunua miaka minne iliyo pita ilinijenge chaajabu magu kajenga nchi mimi hata msingi bad. ,,,,, nakukubalisana raisi wangu wewe nimpango wa mungu kumbe inawezekana eeeh
 
Back
Top Bottom