Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Waasalaam ndugu wanajukwaa nampongeza sana Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufanya nchi hii kila mtu amechangamka penye riziki hapakosi fitina ndo maana unaona joto la wapingaji kila kona wakidai mambo ambayo hawana hoja nayo ila wanasubiri afanye ndipo waanze kubweka.

Tunafaham fika kuwa watu wengi sana hawapendi kuona wakipotezwa kwenye ulimwengu wa siasa na mtu mmoja tena kutoka CCM hawapo tayari ila hawana namna ni kutulia tu dawa iwaingie vizuri.

Nategemea povu zito kutoka kwa wapingaji maana hawatakuja na hoja bali watapinga tu..
EHQ6rZmX4AA-8sv.jpeg
 
Nikiufuatilia utendaji wa serikali ya awamu ya 5 naona yaliyoahidiwa na vyama vya upinzani mwaka 2015 ni kama yameshatekelezwa yote.

Ilani ya CCM kwa kuwa ilisheheni vitu vingi sana kutokana na uwezo mkubwa wa kifikra wa wale walioiandaa imetekelezwa kwa zaidi ya 90% na ifikapo September 2020 itakuwa imekamilika kwa 100%

Nauona upinzani ukifutika kabisa kwenye ramani ya Tanzania.

Maendeleo hayana vyama!
 
@"johnthebaptist,
Ingekuwa vipi kama Kikwete asingeruhusu kukosolewa kuweka TBC mara zote yupo live na kuminya uhuru wa habari?
 
@="johnthebaptist,
KWELI kabisa!

1:Watu wengi wamepotea! kama Ben Rabiu Sanane.

2:Azory Gwanda mwandishi wa gazeti la Mwanainchi.

3:Watu kuokotwa kwenye viroba wanaelea wakiwa wafu.

4:Kuzima uhuru wa habari(bunge live) na kujiweka mwenyeqe live!

5:Kuielekeza mahakama kuamua kadiri ya interest zake.

6:Kuwashughulikia wapinzani na kubambikia kesi mahakamani.

7:Kupotea trion 2 kutonekana kwenye riport ya CAG.

8:Bomu la ajira kutoajiri karibu batch 5 zilizohitimu chuo kikuu.

9:Kulitia Bunge mfukoni kwa kufanya miradi mikubwa pasipo IDHINI YA BUNGE kama ilivyo takwa la kikatiba.

NI KWELI AMEFANYA MENGI 😂😂😂😂😂😂😀😀😀😀😀😀😀

😅😅😅😅😅😅😅😅😅😅😅😆😆😆😆😆😆😆😆😆😆😆 POMBE SIO CHAI!
 
@="johnthebaptist,
"WEWE ,WAULIZE NDUGU ZAKO WAKUANGALIE WATAKUAMBIA" quote from Member of JF last week.
 
Nikiufuatilia utendaji wa serikali ya awamu ya 5 naona yaliyoahidiwa na vyama vya upinzani mwaka 2015 ni kama yameshatekelezwa yote.

Ilani ya CCM kwa kuwa ilisheheni vitu vingi sana kutokana na uwezo mkubwa wa kifikra wa wale walioiandaa imetekelezwa kwa zaidi ya 90% na ifikapo September 2020 itakuwa imekamilika kwa 100%

Nauona upinzani ukifutika kabisa kwenye ramani ya Tanzania.

Maendeleo hayana vyama!
Je, watanzania ni wazito wa kufikiri? Ethiopia inazo ndege nyingi sana na inashindana na nchi za ulaya, Ethiopia inajenga bwawa kubwa sana la umeme na Ethiopia ina reli ya kipimo cha kati (SGR) na ni makao makuu ya AU, lakini wananchi wake kila siku wanakamatwa wakipita Tanzania kuelekea Afrika Kusini, wanaikimbia nchi yao. Watanzania wa leo tunaamini Rais anayefanya manunuzi kila siku basi ni kiongozi bora licha ya sisi kuwa mbali na vitu hivyo. Hapo ndipo tunapoona mkazi wa kijijini Mbaba Bay akishabikia SGR huku akilalamika hana maji, barabara na huduma za afya. Kama kuwa na hivyo vitu ni maendeleo kwa wananchi basi waethiopia hawana sababu ya kukimbia nchi yao. Uajabu wetu ni pale mtu anaposifia utajiri wa mwingine kama vile ni wake huku akilala njaa.
 
Nauona upinzani ukifutika kabisa kwenye ramani ya Tanzania.

Maendeleo hayana vyama!
Mkuu unaweka mambo kinzani, kama maendeleo hayana vyama sioni sababu ya huo upinzani kufutika kwani kazi ya huyo mnae mwimbia pambio si 100% kwenye kukidhi yale watanzania wayatakayo. Kumbuka pia upinzani sio issue ya sera mbadala peke yake bali kuikosoa serikali pale inapokosea hasa kwenye yale mambo amabayo wa ndani hawawezi au hawataki kuyaona. Bahati mbaya au nzuri kutegemea unasimamia wapi, serikali hii inayo amini kuwa uCHAMADOLA ni filosofia ya kiungwana hawataki vyama vya upinzani au upinzani nje ya chama usikike wanapenda sana kusikia sauti zao tu na kuamini kuwa wao pekee ndio wana fikira sahihi.
Nyerere aliwahi kuwashangaa hawa CCM kuwa "mazuri yangu wanayaacha lakini mabaya yangu ndio wana ya shikiria". Hivyo si ajabu wewe kuomba usiku na mchana upinzani ufutike wakati unaendeleza u-chama dola na likatiba lenye mambo ya hovyo.
 
Hoja Na mambo ya kumkosoa magu Ni mengi sana.mgombea yeyote Wa urais akishindwa Sera anione tu.bado Ni mengi kibao.kwa mfano bodi ya mikopo badala ya kutoa mikopo ya ELimu ya juu kiubaguzi itoe kwa watu wote.pia mikopo waombaji wenyewe wapendekeze kiasi cha kukopeshwa.mambo Ni mengi hatari
 
Back
Top Bottom