Uhai wa kiumbe chochote unaanzia kwa kuvuta na kusambaza vizuri hewa safi mwilini na kuitoa iliyotumika nje ya mwili. Watanzania tunayo bahati kubwa ya kumpata mtu anayetuzibulia pua na mapafu ya nchi ili viungo vingine viweze kufanya kazi zake vizuri. Mpaka sasa Rais Magufuli hajakosea kitu chochote hasa kutokana na alivyoikuta nchi.
Nchi ilipokuwa imefikia kwa vyovyote vile ingehitaji mtu kama Rais Magufuli ambae angefufua nidhamu ya kazi, kuondoa mazoea, kufufua utendaji wa jeshi la polisi na watendaji, kufufua barabara, reli, umeme, viwanda, ndege na meli ambayo ndiyo pua, mapafu, moyo na mishipa ya damu ya taifa lolote.
Tumpe kura 2020 ili tumtume tena kuhakikisha kuwa anaboresha na kushuhulikia utawala wa sheria (mahakama, katiba, vyama vingi), uvuvi mkubwa, kilimo kikubwa, uchimbaji mkubwa, utalii, elimu ya kati na ya juu, na kipato cha watumishi wa umma (purchasing power).
Hata wakoloni walifanya hivi, wanafanya hivi na wataendelea kufanya hivyo.