Mbolabilika
JF-Expert Member
- Jul 30, 2019
- 2,128
- 2,867
Ningeshangaa ungepata like hata moja maana haya maneno hayana uhalisia ndio yaleyale maneno ya chadema
- Ifuatayo ni tathmini yangu juu ya utawala wa rais Magufuri katika miaka yake mitano.Lengo ajue wapi amefaulu wapi bado ili arekebishe makosa kama atapata miaka mingine mitano.
1.Pamoja na kujengwa miradi mikubwa Kama SGR, Stiegersgorge ,Ununuzi wa ndege .
A. Hali ya Umaskini imeongezeka sana ndani ya miaka mitano.mzunguko wa pesa umepungua kutoka bilioni 220 mpaka bilioni nane .
B .Wafanyabiashara wengi wakubwa wamehama nchi baadhi wamekwenda Zambia hivyo kuathiri mzunguko wa pesa na ajira .
C. Biashara nyingi zimefungwa hii ni kutokana na makadilio makubwa ya kodi hivyo wafanyabiashara wakaamua kufunga biashara hivyo kuathiri mzunguko wa pesa na ajira .
D . Ukosefu wa ajira ndani ya miaka mitano serikali imeshindwa kuajiri kama serikali iliyopita ilivyofanya ,serikali hii imeajiri kiujanjaujanja .
E . Serikali imeshindwa kupandisha mishahara ndani ya miaka mitano ,hivyo kushindwa kuongeza mzunguko wa pesa .
F . Mahusiano ya kimataifa , serikali hii imeshindwa kuimarisha mahusiano ya kimataifa Kama ilivyoyakuta chini ya JK na awamu zilizopita. Kumbuka balozi wa umoja wa Ulaya alitimuliwa hivyo , umoja wa Ulaya kusitisha misaada na kusema unaangalia upya mahusiano yake na Tanzania.Barua mbalimbali za masikitiko za ubalozi wa marekani ,Sweeden , Uholanzi kuhusu Ukiukaji haki za binadamu, demokrasia na utawala bora .Awamu hii imekuwa na matukio mengi sana ya ukiukaji wa haki za binadamu , watu kupotea , kufungwa , kuwekwa ndani bila mahakama kuthibitisha makosa ,kesi za ajabu za wakosoaji wa awamu ya tano zimejaa tele zisizokuwa na sababu .
G. Ukiukaji mkubwa wa sheria na katiba awamu hii tumeona nchi inaendeshwa kwa amri za rais za papo kwa papo bila kujali sheria zinasemaje? Mifano mingi watumishi wateule wa rais kufukuzwa papo bila kujali sheria ,katiba na haki zao.
H . Serikali kufanya Manunuzi na matumizi ya mabilioni ya pesa bila idhini ya bunge ,mfano mzuri ununuzi wa ndege.
J . Serikali kulisimamia bunge badala ya bunge kuisimamia serikali rejea maagizo aliokuwa anapewa Ndugai na rais.
K . Serikali kuingilia muhimili wa mahakama .
L .Kuzolota huduma za afya ,mfano awamu hii kina mama wakijifungua mtoto wa kiume Tshs 50000/=.Mtoto wa kike 40000/=Tofauti na awamu iliyopita.
M . Ukandamizaji mkubwa wa uhuru wa vyombo Vya habari.
N . Ukandamizaji mkubwa wa demokrasia hasa uhuru wa vyama vya siasa , ambavyo havina madhara yoyote kwa serikali.
O . Kuzolota kwa mifuko ya hifadhi ya jamii , hivyo Kupeleka wastaafu kulipwa kwa shida awamu nne , kidogo kidogkidogo.
P . Serikali ya awamu ya tano kuendeshwa kwa propaganda zaidi kuliko uhalisia ikiwemo kuficha takwimu mbalimbali mpaka kutungwa sheria ya kuzuia watu kutoa takwimu .
q .Ukuaji u humi ,Enzi za JK uchumi ulikuwa kwa 7% ,Sasa hivi tunaambuwa uchumi unakuwa kwa 7% ,Sasa alichofanya kwenye Ukuaji uchumi nini ? Ingawa WBna IMF wanasema 2020 /2021 makadirio ya Ukuaji uchumi ni 2% kabla ya Corona.Wakuu itaendelea . Stay tuned . Unakaibishwa kuongeza , kuchangia ,maoni , ushauri.