Ndugu zangu ni usiku wa manane na pamoja kwamba nina usingizi, nimeona niwaletee hii ili liwe somo kwetu sote.
Raisi wetu Mheshimiwa J. J Magufuli alipotamka sera ya kudhibiti Corona katika taifa, tulitiliwa mashaka na hata kubezwa na watu mbali mbali wakiwemo watu wa hapa kwetu. Jambo la kuhuzunisha ni pale ambapo waliamua kulichukulia suala hili kisiasa na mazoea ya kukanusha kila jambo hata kama ni jema namna gani maadamu likidhi mitazamo ya kisiasa.
Hata rais alipoagiza watu wote tuombe Mungu na kumshukuru, waliendelea kubeza wakati huo huo ukiangalia, wanasema wana dini. Wengine walitabiri kwamba tutakwisha huku rais wetu akifedheheshwa na kutupiwa kila takataka . Lakini Rais wetu amekuwa kiongozi wa pekee sana katika Africa na dunia katika mambo mengi likiwemo hili la Corona. Dr. Lumumba alisema "Anachokiona Magufuli kwa sasa akiwa amekaa, WHO watakiona baadaye sana wakiwa wamesimama".
Haukupita muda, tunasikia Mataifa mbali mbali wanaanza kuitisha maombi ya kitaifa.
Baadaye wanaanza kusema maisha yaendelee tujifunze kuishi na huu ugonjwa kama magonjwa mengine.
Wengine wanakataa kufungiwa ndani na hata wanauawa na polisi kwa kutojifungia!. Sijui kifo cha risasi na cha corona kipi ni kifo na kipi ni nini.
Wengine ndio kama hawa wa Berlin.
Wakati huo huo, mbinu zote zinazoshabikiwa na wabezaji, hazijaonyesha kwamba ndiyo njia za mafanikio ya moja kwa moja katika Corona.
Ombi langu ni kwa Watanzania kuacha kubeza juhudi za Rais wetu wa pekee sana.
Naomba tuongeze uwezo wa kuelewa mazuri na kushirikiana na wanaotuongoza katika hayo kwa manufaa yetu. Kama hujui kinachoendelea, kunyamaza ama kuuliza huwa ni uungwana kuliko kupanga mbegu mbaya hata kwa wengine wakati kumbe na wewe hujui.
Ubishi bila maarifa ni fedheha.