--TOKA MSITUNI MABWE PANDE
____________________________________
Mzarendo mwanye mapenzi ya kweli na Nchi yake, Haijui marekani wala Ulaya toka achaguliwe, yeye ni Moro, Iringa, Tanga, Mbeya, Songea ,Mtwara, Lindi, Lukwa, Sumbawanga anarudi Moshi, Arusha, Dodoma anaingia Singida... Yaani yeye anadili kwa ukaribu Sana na watu wake, anatamani kujua kila tatizo la mtu ili atatue Happ Happ. Huko Nchi za nje Wako Mabarozi na kiongozi wao KABUDI, Mama SAMIA pia yupo atatuwakilisha...
Ni JPM, Msikivu, mvumilivu, Mwenye huruma, upendo Rafiki yao wanyonge na wanaoonewa. Yupo kwaajiri ya waliovunjika moyo ili kuwapa tumaini jipya, Haoni shida kutoa mpaka senti ya mwisho kuwapa wenye uhitaji. Yeye alikuwa fukara kama wao, anajua.
Japokuwa alikuwa mkubwa sana kuzidi wao, alishuka kwa unyenyekevu na kula wanacho kula wao. Hakusahau wa kwao, vijana wa enzi yake aliocheza nao akanywa nao kahawa.
Kila alipopita alitenda mema, akawafuta walioonewa machozi yao, akawafungua wafugwa wao, aliingia magerezani kuwasalimu wafugwa, ubinadamu ndio hisia zake. Akawasamehe waliokosea. Wimbo wa upendo uliibwa machoni pake, utumishi uliotukuka.
Hakujilimbikizia mali, anajua tulikuja tupu tutaondoka tupu... Matani kidogo, masihara kidogo ili tu kuwaonyesha ni Mimi yule yule sikubadilika.
Usingizi hapati akiwaza Tanzania....
Huyu ni Baba mwema sana.
-JPM 5tena-
View attachment 1539148