Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

MAGUFULI Vs BARICK
Huu ulikuwa mtihani mzito sana kwenye utawala wa Magufuli uliopelekea kuagizwa maafisa wakuu wa Barick waliufyata wakatulipa $300 million dollars, mikataba ilirekebishwa. Kwenye hili mzee wa MIGA aliiitisha sana Serikali lakini mafanikio makubwa yalipatikana

MAGUFULI VS MIKATABA MIBOVU ya mashirika ya umma kama TTCL, AIRTEL, GEPG, yote ilifumuliwa ikaaanza kunufaika

Yapo mengi saana lakini kwa Leo niishie hapo
 
- Ujenzi wa bwawa la nyerere nao ulipigwa sana na wanamazingira.
- Ujenzi wa reli nao alinyimwa mkopo ikabidi atumie fedha za ndani kwenye awamu ya kwanza.
 
Kila siku naona watu wanajitoa ufahamu na kumsifia Magufuli kafanya mambo makubwa kwa Nchi ya Tanzania kuliko watangulizi wake.

Hivi mambo hayo makubwa ni yapi hasa kayafanya?? Tangu ameingia huyu jamaa madarakani naona shida na umaskini kwa watanzania umeongezeka.

Utawala wa Magufuli unaongoza kwa kupika data na uongo uongo mwingi ,rejea suala la kufikia uchumi wa kati.

Magufuli ameshindwa kuajiri vijana wengi,amefilisi biashara za watu,kadhulumu hela za wakulima wa korosho.

Utawala wa Magufuli umejenga uoga mkubwa kwa watumishi wa umma na wananchi wa kawaida.

Hiyo miradi mnayomsifia kujenga imeleta faida gani hadi sasa kwa nchi zaidi ya kutuongezea umaskini.

Mnamsifia kaijenga Dar lakini kumbuka asilimia kubwa ya watanzania hawana huduma ya uhakika ya maji safi na salama,barabara nyingi za vijijni ni mbovu,hiyo elimu bure mnayopayuka nayo kila kukicha ni ovyo tupu watoto wanarundikana darasani kama chawa!!

Huyu Magufuli mnamsifia kwa lipi la maana alilofanya au ile tabia yake ya kuteua na kutengua hadharani,kufoka foka ovyo ndo mnamwona kafanya mambo makubwa??

Au kula mhindi pale dumila ndo mnaona amefanya mambo makubwa?

Au kuzawadiwa jogoo pale Nangurukuru ndo mnaona kafanya mambo makubwa.

Jamaa mnamsifia bure tu ila kaharibu sana na kavuruga uchumi wa nchi yetu hafai tena kuongoza baada ya October 2020.
 
*SHUJAA WETU RAIS DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI LAZIMA AREJEE MADARAKANI KWA USHINDI MKUBWA WA KISHINDO UCHAGUZI MKUU OKTOBA 28, 2020.*

Kwa Kazi Kubwa iliyofanywa na Rais wetu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Pamoja na Serikali yake ( 2015 - 2020 ), Watanzania wote wenye Mapenzi Mema na Nchi yetu, Tunaokipenda Chama chetu Cha Mapinduzi na Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli, tunapaswa Kuhamasishana sasa Kuwa ON. Hakuna Kulala wala Kubweteka, Tunawajibu Mkubwa wa Kuhakikisha Shujaa wetu Rais Dkt. John Pombe Magufuli anarejea Madarakani Kwa Ushindi Mkubwa wa Kishindo.

Tusilale Ndugu zangu na Kujifariji, Tunapaswa Kuingia Vitani sasa, Kwa hii Miezi Miwili Tujitoe Kwelikweli Kuifanya Kazi ya Kutafuta na Kulinda Kura za Rais Magufuli na Wagombea Ubunge Kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi.

Arusha Tuko Tayari Kumkabiri Goriati anayejiita CHADEMA NA Ndugu zake wengine; ACT Wazalendo, CUF, NCCR Mageuzi[emoji35][emoji1377]

*Robert PJN Kaseko*
*Arusha.*
 
Onesha na jinsi alivyoua demokrasia na kuleta ubaguzi kati ya makabila.
 
Mkuu hiyo picha ya HEP sio ya Tanzania kama kuna namna ya kuitoa itoe.

Ya Tanzania hii hapa
 
Shujaa analindwa na mijegeja muda woteπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Sipangiwi na mtu kura yangu kwa Lisu suwezi kumpigia mtu kura kwajenga barabara kwa kutumia pesa zetu za kodi na pesa za mabeberu.
 
Sema shujaa wako wewe. Mradi wa kwake uliokamilika ni ndege tu ambao mpaka kuwafanyia figisu Fastjet ili mbaki peke yenu, ambao pia kwa mujibu wa SieJii mliyemtoa ni kwamba shirika linajiendesha kwa harasa.
 
NAMPA MITANO TENA MAGUFULI:

Ujenzi wa Julius Nyerere Hydropower Station(JNHS) kwa Africa ni mradi wa nne kwa ukubwa wa aina yake na ni wa tisa duniani.

Ambao utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuzalisha Megawatts 2115. Ambao unatarajiwa kumalizika 2022.

Uwekezaji wa mradi huu ni usd 3.9 billion ambazo ni sawa na Tsh trillion 6.558 ambao unajengwa kwa pesa za ndani, Lengo kuu la mradi huu ni kuifanya Tanzania kuwa na umeme wa uhakika kuelekea uchumi wa viwanda.

Umeme ambao utavutia zaidi wawekezaji katika sekta muhimu ya viwanda na kama mjuavyo viwanda vinapokuja na ajira zaidi zinakuja.

Ikumbukwe hii ilikuwa ni ndoto ya Hayati baba wa taifa iliyotelekezwa na John Pombe Joseph Magufuli.

Na ndio maana nasema;
#NitampaTANOTENAMAGUFULI
 
Mtoa mada utakua Mwanamke au Mzee au mkazi wa Kijijini au Ngumbaru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…