Tigershark
JF-Expert Member
- Oct 9, 2018
- 7,051
- 12,566
Si kweli,kuna watu wanajua wanashiriki tu uchaguzi kwa malengo mengine lakini sio kwenda ikulu!hahahaha hata yy anamalengo ya kuelekea ikulu mkuu angekuwa hana nia angeacha kama alivyofanya TLP chama chochote kile kilichobeba form ya urais ujue ni mpinzani Wa CCM
Kwenye vita mtu yoyote anaekujia na upanga ni adui yako haijalishi ukubwa wala makali ya upanga wake.Rungwe mnamuonea tu!Wala yeye hapambani kushinda,hapa ni CCM vs CHADEMA,basi!So ukisema upinzani uwe unarefer CDM!
Rungwe nae unamuita mpinzani. Yule ni commedian. Halaf hapambanii kushinda. Kwa sasa anatafuta platform ya chama chakeNaunga mkono hoja. Magufuli kushinda ni lazima hilo halina ubishi kwa upinzani wa sera za ubwabwa na kuku rosti njia ni nyeupe mpaka ikulu.
Kwenye vita maadui wanatofautia uwezo. Si wote wako sawa.Kwenye vita mtu yoyote anaekujia na upanga ni adui yako haijalishi ukubwa wala makali ya upanga wake.
Mitano mingine kwa Magufuli.
Rungwe ni miongoni mwa wagombea wa kiti cha urais hivyo ni mpinzani wetu. Ccm tunahitaji kura nyingi kadri inavyowezekana hivyo sio busara kumpuuza RungweRungwe nae unamuita mpinzani. Yule ni commedian. Halaf hapambanii kushinda. Kwa sasa anatafuta platform ya chama chake
Wapinzani pia wanataka kujua waliomtwanga risasi 38 Lissu na wanataka pia kujua watekaji na wauawaji , usisahau kumwambia na hilo alifanyie kaziNaamini humu jamvini wapo vijana wako na watakufikishia taarifa hii na nyingine nyingi zinazoandikwa na wanajamii forum.
Kila jambo lililo jema linalopigiwa kelele na wapinzani kwa ajili ya manufaa ya nchi yetu lifanyie kazi wakati huu wa kampeni. Tunaamini serikali bado ipo. Endeleeni kuboresha na kuweka mikakati mbalimbali ya kupambana na kila changamoto inayoibuliwa na wapinzani kwani kwa kufanya hivyo kufikia October 28 mashimo yote yatakuwa yamesha sawazishwa na njia itakuwa nyeupe.
Hapo atakaa kimyaWapinzani pia wanataka kujua waliomtwanga risasi 38 Lissu na wanataka pia kujua watekaji na wauawaji , usisahau kumwambia na hilo alifanyie kazi
Approach yake haimfanyi aonekane kama mpinzani. Sera mbovu mizaha mingi. Ana safari ndefuRungwe ni miongoni mwa wagombea wa kiti cha urais hivyo ni mpinzani wetu. Ccm tunahitaji kura nyingi kadri inavyowezekana hivyo sio busara kumpuuza Rungwe
Tusiwe wanafki kwenye ukweli tuusemeAsante Rais Magufuli kwa kutupeleka Tanzania katika uchumi wa kati
Umepeleka umeme kila kijiji, Zahanati kila kijiji, elimu bure
Sisi Watanzania tutakuchagua kwa kishindo October 28
AminaAsante Rais Magufuli kwa kutupeleka Tanzania katika uchumi wa kati
Umepeleka umeme kila kijiji, Zahanati kila kijiji, elimu bure
Sisi Watanzania tutakuchagua kwa kishindo October 28
Kama angeamua kua muoga hiiiiiiiiiiiiiiiiii hata kampeni zisingekuwepo kabisa kwa hiyo uchaguzi usingefanyika kabisa, nikukumbushe hawa jamaa zetu walitaka tufungiwe ndani na mifano ipo pale wapo toka bungeni, lakini pia hata lisu mwenye alibeza sana hatua alizo chukua magu alibeza kwa mtindo wa dharau sana lakini magu akasimimia anacho kiamini hapo ndio tuone hawa jamaa wenyewe wapinga tu hata kama ni jambo jema, tuulizane kama rais angeamua kufungia watu ndani wangefanyaje na angesema hakuna uchaguzi kabaki kua rais halafu wanakuja na ngonjera ya haki wanataka haki gani?Wanasema mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, mimi LICHADI nilijiunga jf Mwanzoni mwa mwaka 2015, wote pitieni thread zangu za nyuma sijawahi kuipenda ccm wala kumkubali Magufuli hata 2015 kura yangu ilienda kwa Lowassa, naongea haya ili msije sema mataga wapo kazini.
JPM anastahili kupongezwa hasa katika kutetea wafanya biashara wadogo kama wamachinga na wengineo , kipindi cha Jk hawa watu walikuwa wanateseka sijawahi kuona, ukipita mjini huko walikuwa wananyanyaswa na wagombo hadi unawaonea huruma, yaani walikuwa wanafanya biashara kama wezi wakiona wagambo wanakimbia, wanapandishwa kwenye makarandinga kama wakimbizi
Tokea JPM aingie alipinga sana hawa watu kunyanyaswa akahitaji waachwe wafanye biashara hamna wa kuwasumbua, na ndio maana ukipita mjini sasa hivi wamachinga wanafanya biashara kwa uhuru, wale ni watu na wanafamilia wanategemewa , wafanya biashara ndogo ni wengi kuliko walioajiriwa kwenye sekta binafsi na serikalini, hivyo JPM kuwapa uhuru ni credit moja wapo ya kuongeza ajira za kujitegemea, usisubirie kuajiriwa
2. JINSI ALIVYO KUWA NA MSIMAMO KWENYE JANGA LA CORONA
Katika sehem ambayo kama Rais angekuwa muoga basi ni kipindi hichi cha Corona, kama Jpm angeruhusu Lockdown na watu kujifungia ndani basi leo hii kuna watu mngeshakufa na njaa na ajira zingepukutika , Leo hii watu mngekuwa vijijini huko
Lakini JPM hichi kipindi alisimama kama mwanaume kweli kweli, akawaambia watu huu ugonjwa upo kimkakati zaidi na unakuzwa kuliko unalisia, akasema kuwa hata vipimo haviaminiki na kuna watu wamekufa kwa kupewa majibu ya uwongo, watu wakamuona kama chizi.
Baadhi ya viwanda na makampuni yalishaanza kupunguza watu na mengine kufungwa kwa uwoga , lakini JPM alisimama na kuondoa watu hofu akisema kuwa watu wachape kazi hamna kuwa waoga huu ugonjwa kuna mchezo unachezwa na wazungu, ni kweli upo lakini unakuzwa, akasema watu wapige nyungu waache uwoga, waliofunga makampuni wafungue
Akaamuru shule zifunguliwe, hapo walimu sekta binafsi waliokuwa taabani wakapata nafuu, akaamuru makampuni yaendelee na uzalishaji waache uwoga, watu waliopunguzwa kazini mdogo mdogo wakarudishwa hali ikajirudia kama kawaida
Akaamuru makumbi ya starehe, mikutano maharusi yapige kazi, now mamc wamiliki wa kumbia na wengine wengi waliokuwa taabani kazi zinaendelea ,.mean alisimama bila uoga kuokoa ajira za watu
Kama tungekuwa na Raisi muoga kama Kenyatta basi leo tungekuwa taabani,
Ni kweli kawekeza sana kwenye miundombinu huku ajira za serikali zikiwa chache si kama zamani, lakini tukumbuke kaokoa ajira za watu wengi sana kipindi hichi cha Corona na kuwapa uhuru wafanya biashara ndogo ndogo kutobugudhiwa
Hata ukimchukia mtu mahali alipofanya vizuri mpe sifa yake...
LICHADI
HihiiKama angeamua kua muoga hiiiiiiiiiiiiiiiiii hata kampeni zisingekuwepo kabisa kwa hiyo uchaguzi usingefanyika kabisa, nikukumbushe hawa jamaa zetu walitaka tufungiwe ndani na mifano ipo pale wapo toka bungeni, lakini pia hata lisu mwenye alibeza sana hatua alizo chukua magu alibeza kwa mtindo wa dharau sana lakini magu akasimimia anacho kiamini hapo ndio tuone hawa jamaa wenyewe wapinga tu hata kama ni jambo jema, tuulizane kama rais angeamua kufungia watu ndani wangefanyaje na angesema hakuna uchaguzi kabaki kua rais halafu wanakuja na ngonjera ya haki wanataka haki gani?
Lissu hataki kuukubali ukweli.Tusiwe wanafki kwenye ukweli tuuseme
Hahahahaaaaaaaaaa umenichekesha hatariLissu mwenyewe anamkubali kisirisiri
Ameweza hadi kuna wanaoomba pooAkiweza kudumishs hii speed, hakika nchi itarudi kwenye mstari