Wanasema mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, mimi LICHADI nilijiunga jf Mwanzoni mwa mwaka 2015, wote pitieni thread zangu za nyuma sijawahi kuipenda ccm wala kumkubali Magufuli hata 2015 kura yangu ilienda kwa Lowassa, naongea haya ili msije sema mataga wapo kazini.
JPM anastahili kupongezwa hasa katika kutetea wafanya biashara wadogo kama wamachinga na wengineo , kipindi cha Jk hawa watu walikuwa wanateseka sijawahi kuona, ukipita mjini huko walikuwa wananyanyaswa na wagombo hadi unawaonea huruma, yaani walikuwa wanafanya biashara kama wezi wakiona wagambo wanakimbia, wanapandishwa kwenye makarandinga kama wakimbizi
Tokea JPM aingie alipinga sana hawa watu kunyanyaswa akahitaji waachwe wafanye biashara hamna wa kuwasumbua, na ndio maana ukipita mjini sasa hivi wamachinga wanafanya biashara kwa uhuru, wale ni watu na wanafamilia wanategemewa , wafanya biashara ndogo ni wengi kuliko walioajiriwa kwenye sekta binafsi na serikalini, hivyo JPM kuwapa uhuru ni credit moja wapo ya kuongeza ajira za kujitegemea, usisubirie kuajiriwa
2. JINSI ALIVYO KUWA NA MSIMAMO KWENYE JANGA LA CORONA
Katika sehem ambayo kama Rais angekuwa muoga basi ni kipindi hichi cha Corona, kama Jpm angeruhusu Lockdown na watu kujifungia ndani basi leo hii kuna watu mngeshakufa na njaa na ajira zingepukutika , Leo hii watu mngekuwa vijijini huko
Lakini JPM hichi kipindi alisimama kama mwanaume kweli kweli, akawaambia watu huu ugonjwa upo kimkakati zaidi na unakuzwa kuliko unalisia, akasema kuwa hata vipimo haviaminiki na kuna watu wamekufa kwa kupewa majibu ya uwongo, watu wakamuona kama chizi.
Baadhi ya viwanda na makampuni yalishaanza kupunguza watu na mengine kufungwa kwa uwoga , lakini JPM alisimama na kuondoa watu hofu akisema kuwa watu wachape kazi hamna kuwa waoga huu ugonjwa kuna mchezo unachezwa na wazungu, ni kweli upo lakini unakuzwa, akasema watu wapige nyungu waache uwoga, waliofunga makampuni wafungue
Akaamuru shule zifunguliwe, hapo walimu sekta binafsi waliokuwa taabani wakapata nafuu, akaamuru makampuni yaendelee na uzalishaji waache uwoga, watu waliopunguzwa kazini mdogo mdogo wakarudishwa hali ikajirudia kama kawaida
Akaamuru makumbi ya starehe, mikutano maharusi yapige kazi, now mamc wamiliki wa kumbia na wengine wengi waliokuwa taabani kazi zinaendelea ,.mean alisimama bila uoga kuokoa ajira za watu
Kama tungekuwa na Raisi muoga kama Kenyatta basi leo tungekuwa taabani,
Ni kweli kawekeza sana kwenye miundombinu huku ajira za serikali zikiwa chache si kama zamani, lakini tukumbuke kaokoa ajira za watu wengi sana kipindi hichi cha Corona na kuwapa uhuru wafanya biashara ndogo ndogo kutobugudhiwa
Hata ukimchukia mtu mahali alipofanya vizuri mpe sifa yake...
LICHADI