Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Miako 10 ya Kikwete ni The Lost Ten Years.

Kikwete hakujua uzito wa Jukumu alilokuwa nalo hata kidogo wala hakuwa anajua nini kinaendelea hata pale Ikulu alone
Aisee huyu jamaa Mungu ampe maisha m?refu ajioe yatakayoendelea.
 
magufuli alikuwa msimamizi kwenye uuzwaji wa nyumba za umma. sina cha kumsifu hapa hata kidogo labda arudishe nyumba zetu alizogawa kwa bei ya kutupwa kama njugu.
uongozi wa kikwete ulichemka sana kwa hili maana nakumbuka kuna yule waziri kutoka nchi jirani aliyekuwa anaitwa pilot wa meli aliishi hotelini na kutugarimu mamilioni ya kodi zetu kisa tu kateuliwa kuwa waziri wa mabunduki.


 
?Asiyefunzwa na Ccm, atafunzwa na Magufuli.

Huo ndio msemo halisi ninaoweza kuutumia, hali imezidi kuwa tete ndani ya Ccm na pumzi ndo inazidi kuisha kwa mafisadi.

Mwanzo walimshangilia kwa sasa wanajutia, walisupport kwa nguvu na unafiki kuwa iundwe mahakama ya mafisadi bila kujijua kuwa mafisadi ni wao wenyewe.
Sasa hebu niwaulize kitu wana ccm wote, je magufuli aweke mahakama ya mafisadi?

Serikali ya Mh John Pombe Joseph iko imara na haiendi kwa kushinikizwa, ngoja muisome namba vizuri na mkimsusa tuachieni tena jembe lingine tuuwashe moto kumbukeni wapinzani tunao Lowassa na Sumaye tayari, So kazi kwenu kuendelea kuugulia maumivu au kubwaga manyanga.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Trust me TRA kuna uwezekano mkubwa wakawa wanakusanya trillion 2.5 kwa mwezi katika kipindi cha kuanzia miezi 6 ijayo. Kuna jamaa yangu anadai amepigiwa simu na bosi wake (Mchina) katika hali ya dharura (urgency ya ajabu) na kwa kushtukiza (as if mtu anaepiga simu fire/ambulance) akimsihi na kumsisitiza atoe risiti za TRA kwa kila mzigo atakaouza hata ukiwa ni mzigo Wa millioni 50, ahakikishe anaandika risiti ya 50m exactly bila kupunja hata 100 kwa kuandikia nusu risiti Kama wafanyavyo wafanya biashara wengi. Wakati Mchina huyo anapiga simu hiyo alikuwa akihema kama anakimbizwa, ikabainika alikuwa anarush ku-solve ishu nzito ya Mchina mwenzake alie tiwa nyavuni na mamlaka kwa masuala ya ukwepaji kodi..., ni mkimbizano na mtifuano mkali sana unaendela kwa sass..
 
Ahsante kwa kuwasilisha ila kwa nini hii post ipo kwenye "Tech Gadgets & Science"??
 

Mambo yote hayo katika hii miaka kumi itatosha!?? Labda tupige kura za maoni tumuongezee miaka kumi mingine
 
mkuu bandari tu tukiibana vizuri na hawa matajiri wa madini , utalii bila shaka tutaweza kufika hadi 4.0 triolion kwa mwezi mark my words
 

Mkuu mimi naona hapo hujatabiri kitu chochote
kwani ulichokisema hata mtoto wa vidudu anaweza
kukibashiri kwani kwa kasi liliyopo kwa sasa na hakika
hakuna atayesalimika.

Hilo la kuongezeka mapato kwa kasi iliyopo sasa ni lazima
kwani ulichokibashiri ni sawa na mtu uende kwa mganga wa
kienyeji unaonekana mwingi wa mawazo , halafu anaanza
kukwambia kuwa unaonekana una matatizo lukuki yanakuandama
katika maisha yako.

Sasa wewe hapo unadhani kutakuwa kweli kuna utabiri...?? zaidi ya kutumia
muonekano wa hali yako kubashiri mambo aliyokuambia.
 
Huo si utabiri wakati ni jambo la dhahiri
 

Haahaaahaa.., aya bhana.., ila naanza kuelewa kwanini elimu bure inawezekana kabisa.., huko TANAPA na MADINI nasikia kuna mapato bwerere yanamwagikia chini.., magufuli apeleke ndoo za kukingia mapato kule..
 
mkuu bandari tu tukiibana vizuri na hawa matajiri wa madini , utalii bila shaka tutaweza kufika hadi 4.0 triolion kwa mwezi mark my words
Sure..? Hivi kwenye madini tunatakiwa ukapa mrahaba/mrabaha wa asilimia ngapi vile?
 
Mahakama ya mafisadi ikianza Lowasa hatoki bila kusahau rostamu Azizi.
 
Wengi tunafurahi yanayoendelea. Na mengi yanafuata sheria kwa sababu kuna watu waliachwa muda mrefu na wakazoea kuishi kwa taratibu zao. Kwa upande wa Serikali, ni nini kitatokea?
1. Kwa muda mfupi, mapato yataongezeka maana watu watalipa kodi na hata madeni yao.
2. Uchapa kazi utaongezeka kwa watumishi wa Umma ambao ni wazembe, walevi na watoro.
3. Miradi iliyokwama itafufuliwa na kuendelea.
Kwa Watanzania; Kuna madhara hasi na chanya.
Chanya;
1 . Mategemeo yetu ya ufanyaji kazi wa Serikali yataonekana
2. Huduma zitaimarika na nidhamu kule tunapopata huduma itaonekana
3. Dhana ya kazi na wajibu, itarudi na tutaona rushwa zikipungua
4. Bei ya baadhi ya bidhaa huenda ikapungua kutokana na watu wenye pesa nyingi za kupata kwa njia zisizoeleweka kupungua. Hapa nazungumzia viwanja, kodi, malighafi, elimu kwenye sekta binafsi nk
Hasi
1. Wengi wetu watapoteza kazi hasa kwenye sekta zenye madeni au zenye kukwepa kodi. Sekta hizi zitakuwa hazina uwezo wa kulipa madeni kwa kushtukizwa
2. Baadhi yetu tutalazimika kuhamisha watoto kutoka shule binafsi na hata kupunguza outings kutokana na udhibiti wa mapato ya serikali
3. Biashara itasinyaa kwa sababu hakuna pesa za kutumia na hivyo kusababisha watu kupunguzwa kazi au mishahara kupungua na hata kubaki vilevile.
Kwa kuzingatia mchakamchaka huu kwa muda mfupi, serikali itaongeza mapato lakini kwa muda mrefu mapato yatakuwa sawa maana madeni yatakuwa yamelipwa, wazalishaji wamepungua lakini huenda uwekezaji ukaongezeka. Kwahiyo purukushani hizi zina manufaa kwa muda mfupi, in the longrun net effect ni zero na huenda ikapungua.
 
Ee Mungu simamia hawa ndugu zangu Watanzania wazidi kumuoombea rais wetu Magufuli. Nakuomva pia uzidi kumpa ulinzi wqoko wa heri ili azidi kufichua yote yaliyojificha. Baba katika jina la mwanao Yesu Kristo ninaomba na kuamini kuwa utazidi kutenda miujiza na kuzidi kumbariki Magufuli.
Mungi ibariki Tanzania
Mungu M bariki Magufuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…