Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

lazma tufatilie na tuchallenge............
umetoa points sana mkuu...
same old story
 
Hapo nitatofautiana na wewe. Yapasa kujua kuwa ile Dec-Jan mwaka huu kuna watu walikuwa wanafunga mahesabu ya mwaka lakini pia kulikuwa na makampuni yaliyopewa muda wa kulipa kodi. Hapo lazima utaona baada ya mambo hayo kupita, actual revenue collection almost inakaa katika normal margin, na kwa hiyo uwezo wetu unacheza hapo yaani kati ya 800-1004bn/-(0.8-1.04tn/-)
 
Imagine popularity ya JPM, mimi nilidhani ni DRC peke yake, wapi bwana mpaka hapa kwa mzee M7. kila kitu utasikia aaaaa huyu dawa yake JPM...... mhh inamaana mpaka huku? mimi nilifikiria ni Kenya na DRC tu.... wakati hii slogan ya @WhatWouldMagufuliDo? bado inavuma sana Why?

Heshima kwako Rais wangu
 
Tanzania tumempata Rais hakuna nchi ya Africa haitamani kuwa na Rais wa hivi mm ni chadema dam ila kiukweli hii kasi ata lowasa asingeiweza hata hayati baba wa taifa hakufikia hapa maguful ni Rais wa kipekee ana uchungu na nchi hii tajiri ila waliifaidi wachache sasa wanatakiwa waishi kama mashetani maskini waishi kama malaika.... huyu maguful ni Rais hataki mchezo ikiwezekana katiba ibadilishwe awe Rais wa milele..... tuu kwa maana hamna namna sasa matajiri wafanyabiashara wanamchukia ila maskini usiongee juu ya maguful utapigwa balaa..

acha waisome namba ee maguful mbele kwa mbeleeeeeeeeeeeeeee

tumbua majipu baba mungu yupo na ww na sisi tunasali na kukuombea daima mungu kwanza mbele
 
Kazi ipo tutayaona mengi
Ivi kwa wananchi gani?wakati huku kitaa njaa Kali kila mtu ukimuambia habari ya majipu hajui faida yake kwani njaa bado ipo pale pale bidhaa kila siku zinapanda bei au wewe upo nje ya nchi? Hacha kutoa post za kipuuzi kama unataka aongoze milele ataiongoza family yenu mana nahisi hapo nyumbani kwenu amna kiongozi
 
mkuu Acha jazba unataka awaletee ela milangon kumbuka bajet mnayotumia ni ya mzee wa msoga

lipa kodi, risit, fanya kazi Acha kupiga umbea maendeleo yanaletwa na ss wenyewe Acha mihemko kaz ya Rais ni kuwabana wanatumia pesa vibaya Rais hawezi kukuletea ela nyumbani ukiwa na mkeo mmelala
 
Nampongeza sana Rais Magufuli kwa kutekeleza ahadi zake na hivyo kutufanya watu tulomchagua kutembea kifua mbele huku mtaani tukitamba dhidi ya wale walotubeza kuwa Magufuli hatoweza kuubadili mfumo ulomlea
Sasa nadhani wanaona haya. Viva Magufuli
 
Raha sana, raha sana. Utendaji wa Magu umetupaisha sisi tuliomchagua. Aibu imewakumba waliotubeza. Kofia na T-shirt za ccm tunavaa, hakuna wa kuinua mdomo. Asante Magu.
 
Nampongeza sana Rais Magufuli kwa kutekeleza ahadi zake na hivyo kutufanya watu tulomchagua kutembea kifua mbele huku mtaani tukitamba dhidi ya wale walotubeza kuwa Magufuli hatoweza kuubadili mfumo ulomlea
Sasa nadhani wanaona haya. Viva Magufuli

Mwenzetu ulikuwa jela nini? Rais aliahidi kugeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda, tayari ameshatekeleza ahadi hii? Hebu tunapozungumza maisha ya mtanzania yamebadilika kipi kikubwa kulinganisha na pale JK alipotuacha? Hebu kama hamna cha kusifia kaeni kimya toeni muda tuone mwelekeo na sio kusifia tu wakati bado ndio asubuhi kabisa. Hiyo ya kufukuza watumishi wa umma bado hakujawa na matokeo ya moja kwa moja kwa maisha ya mwananchi zaidi ya matangazo ya hao watumishi wanaofukuzwa. Toa muda wa kusifia kwani utaupata tu wakati muafaka.
 
Dah... nimecheka sana.....eti mwenzetu ulikuwa jela nini..........hasira zote za kutoswa na mchepuko na hii hali ya hewa zimeisha.......jf ni nouma sana.
 
Nampongeza sana Rais Magufuli kwa kutekeleza ahadi zake na hivyo kutufanya watu tulomchagua kutembea kifua mbele huku mtaani tukitamba dhidi ya wale walotubeza kuwa Magufuli hatoweza kuubadili mfumo ulomlea
Sasa nadhani wanaona haya. Viva Magufuli
Kumbe na wewe unakubali kuwa alilelewa na mfumo fisadi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…