Wacha niseme kutoka moyoni kabisa kuwa mimi CCM na Magufuli hawakupata kura yangu kwasababu ya kile kilichozoeleka kuwa ni watu wa kubebana na kulindana.
Lakini tangu Magufuli ameingia ameanza kunipa tumaini la TZ yangu niitakayo, na nilikuwa namtaka kiongozi ambaye akiingia atawabadilisha watu/watumishi kuwa walizonazo ni dhamana na si kuwa wao ni wafalme ila sisi ( wananchi) ndio mabosi wao.
Nchi ilifikia hatua mkuu wa mkoa/wilaya au wakurugenzi wa wilaya/mkoa ni kama miungu watu akosolewi na muda wote yeye yuko ofisini tu na mwendo wa kuiba tu na kujaza takwimu za uongo. Leo nadhani mnaona wakuu wa mikoa, wilaya,wakurugenzi na hata wakuu wa idara za serikali wanapiga kazi na wanatembelea sehemu za miradi au kusikiliza matatizo ya wananchi.
Leo hii wafanyabiahara walitaka waiendeleza tabia yao ( maana itakuwa hawajaianza leo wameshazoea) ya kuihadimisha bidhaa ili ipande thamani halafu apate faida kubwa sana wakati wananchi tunateketea kwa ukosefu wa sukari kisa eti yeye ana mtaji basi awatese wasiokuwa na uwezo huo.