Habari za jioni na usiku!
Kwa nini naendelea na nitaendelea kumkubali Rais John Pombe Magufuli??
Hapa naachana na ukada na kujikita kwenye kweli na weledi.
HEBU JIULIZE AU FUATILIA YOTE YALIYOSEMWA NA MAGUFULI KAMA AHADI AU ILANI YA CHAMA CHAKE KAMA KUNA AMBALO HAJAAANZA KULIFANYIA KAZI...?
Mimi nitayataja yale ambayo yalinivutia sana kiasi cha kuamua kumkubali,kumsupport ,kumpigania na kumpigia kura.
Moja:
Kuhusu kupambana na mafisadi ...na hapa aliapa kupambana nao kwa hali zote...
Aliahidi mahakama maalumu ya mafisadi.
Tumemsikia na tumeona dhamira yake ya kupambana nao mafisadi kiasi cha kuhisi anataka kuingilia uhuru wa mahakama pale alipowaahidi wanasheria kuwa atawapatia fungu la fidia za kesi zitokanazo na kuwafunga mafisadi.
Kupitia waziri wa sheria mchakato wa kuundwa mahakama ya mafisadi uko mahala pazuri na ifikapo mwezi wa saba tunatarajia mahakama hiiitakuwa tayari imeanza kazi.
Wana JF tuseme nini juu ya hili hasa ukizingatia kuwa forum hii ni kinara wa kupambana na mafisadi?
Kuhusu swala la elimu...Magufuli aliahidi kushughulikia suala la mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.Alihoji iweje kupata mkopo iwe ni shida wakati wanaokopeshwa watalipa?Tumeshuhudia wanafunzi wa elimu ya juu wakipatiwa mikopo yao on time huku bodi ya mikopo na utendaji wake ukipitiwa upya.
Kuhusu afya Magufuli alikerwa na issue ya ukosekanaji wa dawa na vifaa tiba pamoja na huduma mbovu katika hospitali za umma...
Tumejionea nginjanginja kwenye sekta hii ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa huduma kwenye zahanati kuu ya taifa...CT SCAN inafanya kazi.
Ingawa hapa bado kuna changamoto inayofanyiwa kazi ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwenye zahanati zote nchini...dhamira yake imeonekana na pia kupitia waziri wa afya kile Magufuli alichoahidi kuhusu bima ya afya ya jamii kuwa ya wote yaani universal covarage ya health insuarance ni sera inayokuja mwezi wa tisa.
Magufuli alilaani sana kuhusu mabwanyenye wachache kujilimbikizia ardhi kiasi cha kupelekea migogoro ya ardhi nchini...mabwanyenye hawa walitajwa na mifano ipo.tuliijadili sana wakati wa kampeni..kina lowasa na Sumaye walitajwa na leo hii tunaona baadhi yao kuanza kutemeshwa ardhi walizojimilikisha isivyo halali kutokana na vyeo vyao.
Kuhusu uchumi wa Viwanda tumejoonea msisitizo wa Rais katika kila hotuba zake kuhusu ujenzi wa viwanda ...Tumeisikia mikakati na ya uwekezaji wa serikali sekta hii kwa kuandaa mazingira bora ya uwekezaji...hata mkuu wa TIC alitemwa kwa kukosa kasi ya utekelezaji huu.
Kuhusu kujitegemea kiuchumi
Hapa tumejionea harakati za Magufuli kuyabana matumizi yasiyo na tija na pia utekelezeja wa kuhakikisha kodi ya serikali inakusanywa.
Kuhusu kodi za ajabu ajabu kwenye mazao ...tumeshuhudia baadhi ya kodi kwenye korosho na kahawa kuanza kufutwa.
Kuhusu kuulinda Muungano...tumeshuhudia jinsi Rais alivyoweza kulihandle suala la Zanzibar bila damu kumwagika.
Kuhusu kupunguza msongamano Dar nadhani sasa tunashuhudia wakazi wa Dar wakitumia chini ya dakika 45 kufika na kutoka katikati ya jiji.
Kwa ufupi na kwa maoni yangu haya ni baadhi ya mambo ambayo Magufuli ameyafanya ndani ya muda mfupi tena bila ya kutumia bajeti iliyoandaliwa na serikali yake.
Kwa wale wasiopenda kufahamu ninawafahamisha.
kwa wale wasiotaka kukubali tupingane kwa hoja kinzani.
Kwa wale wazungusha mikono njooni mtukane!
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!