Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Kwa magufuli kila goti litapigwa hongera jpm kwa kazi nzuri tunakuombea sana tu.
 
Magu alifika hapo kwenye hilo kanisa kukamilisha mpango wa kuidhinisha mashoga.trust me.

Swissme
 
Kweli kabisa tumeishiwa hekima kiasi hiki? Sishangai wanaohama makanisa kila siku. What has Magu done so far kwa ufisadi? Nonsense
 
Kweli kabisa tumeishiwa hekima kiasi hiki? Sishangai wanaohama makanisa kila siku. What has Magu done so far kwa ufisadi? Nonsense
Kuna fisadi kanyang'anywa viwanja...hujui?
 
Kesho magu atawapelekea barabara, Umeme na maji
Yule jamaa kule ubungo tunampelekea barabara ili waumini wasipate shida
 
Habari za jioni na usiku!

Kwa nini naendelea na nitaendelea kumkubali Rais John Pombe Magufuli??

Hapa naachana na ukada na kujikita kwenye kweli na weledi.

HEBU JIULIZE AU FUATILIA YOTE YALIYOSEMWA NA MAGUFULI KAMA AHADI AU ILANI YA CHAMA CHAKE KAMA KUNA AMBALO HAJAAANZA KULIFANYIA KAZI...?

Mimi nitayataja yale ambayo yalinivutia sana kiasi cha kuamua kumkubali,kumsupport ,kumpigania na kumpigia kura.

Moja:
Kuhusu kupambana na mafisadi ...na hapa aliapa kupambana nao kwa hali zote...
Aliahidi mahakama maalumu ya mafisadi.
Tumemsikia na tumeona dhamira yake ya kupambana nao mafisadi kiasi cha kuhisi anataka kuingilia uhuru wa mahakama pale alipowaahidi wanasheria kuwa atawapatia fungu la fidia za kesi zitokanazo na kuwafunga mafisadi.

Kupitia waziri wa sheria mchakato wa kuundwa mahakama ya mafisadi uko mahala pazuri na ifikapo mwezi wa saba tunatarajia mahakama hiiitakuwa tayari imeanza kazi.

Wana JF tuseme nini juu ya hili hasa ukizingatia kuwa forum hii ni kinara wa kupambana na mafisadi?

Kuhusu swala la elimu...Magufuli aliahidi kushughulikia suala la mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.Alihoji iweje kupata mkopo iwe ni shida wakati wanaokopeshwa watalipa?Tumeshuhudia wanafunzi wa elimu ya juu wakipatiwa mikopo yao on time huku bodi ya mikopo na utendaji wake ukipitiwa upya.

Kuhusu afya Magufuli alikerwa na issue ya ukosekanaji wa dawa na vifaa tiba pamoja na huduma mbovu katika hospitali za umma...
Tumejionea nginjanginja kwenye sekta hii ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa huduma kwenye zahanati kuu ya taifa...CT SCAN inafanya kazi.
Ingawa hapa bado kuna changamoto inayofanyiwa kazi ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwenye zahanati zote nchini...dhamira yake imeonekana na pia kupitia waziri wa afya kile Magufuli alichoahidi kuhusu bima ya afya ya jamii kuwa ya wote yaani universal covarage ya health insuarance ni sera inayokuja mwezi wa tisa.

Magufuli alilaani sana kuhusu mabwanyenye wachache kujilimbikizia ardhi kiasi cha kupelekea migogoro ya ardhi nchini...mabwanyenye hawa walitajwa na mifano ipo.tuliijadili sana wakati wa kampeni..kina lowasa na Sumaye walitajwa na leo hii tunaona baadhi yao kuanza kutemeshwa ardhi walizojimilikisha isivyo halali kutokana na vyeo vyao.

Kuhusu uchumi wa Viwanda tumejoonea msisitizo wa Rais katika kila hotuba zake kuhusu ujenzi wa viwanda ...Tumeisikia mikakati na ya uwekezaji wa serikali sekta hii kwa kuandaa mazingira bora ya uwekezaji...hata mkuu wa TIC alitemwa kwa kukosa kasi ya utekelezaji huu.

Kuhusu kujitegemea kiuchumi
Hapa tumejionea harakati za Magufuli kuyabana matumizi yasiyo na tija na pia utekelezeja wa kuhakikisha kodi ya serikali inakusanywa.

Kuhusu kodi za ajabu ajabu kwenye mazao ...tumeshuhudia baadhi ya kodi kwenye korosho na kahawa kuanza kufutwa.

Kuhusu kuulinda Muungano...tumeshuhudia jinsi Rais alivyoweza kulihandle suala la Zanzibar bila damu kumwagika.

Kuhusu kupunguza msongamano Dar nadhani sasa tunashuhudia wakazi wa Dar wakitumia chini ya dakika 45 kufika na kutoka katikati ya jiji.

Kwa ufupi na kwa maoni yangu haya ni baadhi ya mambo ambayo Magufuli ameyafanya ndani ya muda mfupi tena bila ya kutumia bajeti iliyoandaliwa na serikali yake.

Kwa wale wasiopenda kufahamu ninawafahamisha.

kwa wale wasiotaka kukubali tupingane kwa hoja kinzani.

Kwa wale wazungusha mikono njooni mtukane!

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
 
Kwa magufuli kila goti litapigwa hongera jpm kwa kazi nzuri tunakuombea sana tu.
Tuna imani kubwa sana na Rais Magufuli, he is a God fearing person, mkweli, mtendaji mzuri, ana ethics za seminari kwani uongo ni sumu, afadhali ya mchawi kuliko a liar, a liar is a killer. Dr Magufuli hapendi kudanganywa, sema ukweli na kama ni kosa atasamehe! Ee Mungu, tuma malaika wako wamlinde rais Dr Magu 24/7
 
Wasio elewa Magufuri ni nyumbu wa Ukawa wamekosa hoja wanakimbilia maandamano
 
Asomaye na afaham. Ndugu wa Tz upo msemo unasema nabii huwa hapati heshima kwao ila nje ya kwao anapata heshima kubwa sana. Kama taifa Mungu ktk nyakati hizi ametupa nafasi kiongozi shupavu na mwenye nia ya dhati kuliondoa taifa hili ktk umasikini na kusema ukweli atafanikiwa.

Nilazima wa Tanzania tujuwe Mh Magufuli alipata uteuzi wa chama cha mapinduz kwa ajili yakuleta mabadiliko na sio porojo. Hii ni bahati yakipekee sana baada yamiaka takriban hamsin Tz tumepata Kiongoz wa aina yake.
Hili taifa lilishafika mahali kukawepo na kundi la sisi na wale. Watu ambao walikuwa hawatoki jasho kukuza utajiri wao ila wanakula na kunywa na pesa zinaingia mifukoni mwao. Wakati wachache wakila na kunywa mpaka kusaza. Mamilion walikuwa hawana chakula.

Huyu Rais ameamua kuacha yote nakuhakikisha wote tunapata na ili kuhakikisha azima hiyo inatimia yapo machungu tutayapata ili kufikia nchi ya maziwa na Asali. Haya tunayaona sasa nilazima yatokee ila mh Rais uwenda akawa Rais watofauti kabisa ktk taifa hili akibadilisha kila sector ya uchumi nakuleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi ktk kila nyanja.

Wakati makundi ya watu wachache yana mng'ong'a lipo kundi kubwa litamsifia nakumvika nishani kwakuleta mabadiliko makubwa ktk taifa. Niswala la muda haya yote yatakuwa dhahiri mbele yetu sote.

Na asomae afaham.
 
Sasa huu ni unabii au maoni kuhusu kazi ya JPJM. Huu ni unabii au ni namna ya kuendelea kuimba sifa za "mtakatifu" raisi wa "wadanganyika".

Huu ni unabii au muendelezo wa propaganda za kujaribu juwalainisha au kuwapoza wadanganyika ambao baada ya miaka zaidi ya 30 imewapasa kupanga foleni ili kupata sukari.

Haya mleta mada endelea kuishi udanganyikani. Je, yawezekana wewe nawe ni wa "ulevini lumumba"!

Huu si unabii. Hii ni mhemuko wa propaganda. Utakapoisoma namba uje na unabii wa kweli!
 
Huu unabii wa kuwaongezea masikini mzigo wa kodi?, pombe inaingiza Pesa nyingi kuliko dhahabu au gesi halafu unasema kaja kuwakomboa wanyonge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…