Aman izidishwe kwenu wana wa jf.
Sii viongozi wa ukawa,sii viongozi wa vyama vinavyounda ukawa,sii wanachama/mashabiki na hata wadau wote wamepoteana na hayupo anayeongoza chombo sasa...
Kama ni ndege nawezakusema haina rubani na kama yupo ndani ya ndege basi kalala fofofo.
Wenye mitizamo mipana wataniunga mkono ila wenye mitizamo mifinyu watanikosoa na kunizodoa kama walivyozoea.
Hivi uko wapi ule utashi mliojaliwa katika kipindi cha nyuma?au kweli jina tu la mh.rais wetu(Pombe)limewalewesha tu kwa hisia?
Au basi inawezekana spidi za mh.rais yamkini zimewachanganya?La hasha msichanganyikiwe na kasi hii...ni kweli hamkuzoea...lakini kwa huyu ndugu yetu,kazi ni jadi yake maana hatujamjua leo.Historically ni mtekelezaji cku zote,wasiomjua ni wanaozaliwa sasa.
Kwa nn nasema haya...?
Mambo yote maovu anayokabiliana nayo mh.rais mf.kutumbua majipu,suala la watumishi hewa,wanafunzi hewa(******)na mengine mengi wao sasa wanayakumbati na kuyatetea kwa gharama yyt kinyume na hapo awali walivyokabiliana nayo.
Wamegeuka kuwa mawakala wa waovu/maovu yote na kukusudia kumkwamisha rais kuyakabili,hali inayonifanya niwaite walevi.
Mbaya zaidi wamekosa uwakilishi hata kwenye jambo mhm(budget)ya serikali ambayo ndio dira ya maendeleo kwa wananchi wote bila kujali vyama.
Kwa makosa ya kujitengenezea wenyewe,viongozi wao mhm kabisa wamefukuzwa bungeni kwa kipindi kirefu,lakin pia waliobaki kwa kukosa busara wamejenga mazoea ya kususia vikao kila cku mpaka bajeti inapita.
Kwa nini nisiwaite walevi?
Kama sii hivyo basi wote mniunge mkono kwamba kumbe kelele za watu hawa cku zoote za maisha yao ya kisiasa ni kuikwamisha sirikali kwa mazuri inayoyafanya ili wajitwalie sifa kwa mashabiki wao wajinga ambao pia nimeanza kwa kuwaita walevi.
Hawapaswi kuwa mfano wa kuigwa hata kidogo,dhahiri wanafikiri kwa kutumia matumbo na sii akili,tuwaache waendelee na ulevi wao mpaka miaka mitano watakapokutana na hukumu zetu kwenye vichinjio.
USHAURI WA BURE KWAO;Pombe habadiliki,labda wao wabadilike kwa kuacha kulewa hata nyakati za kazi.Wenye mapenzi mema na nchi tutamsapoti rais wetu kwa gharama yyt ili atufikishe tunakokusudia,maana anayoyafanya ni kwa niaba ya watanzania wa vyama vyote wazalendo na sii kwa niaba ya wasakatonge wachache wenye nia mbaya na hili taifa.
Woooooooote tuseme...Viva magufuli!