Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Tuko naye rais wetu make hii ni kwa faida yetu na vizazi vyetu

nyie acheni ndoto , Urais ni taasisi si Mtu mmoja ni mapema sana kuanza kumchukiza Mungu , mlisema kikwete ni wa Mungu ona aliyoyafanya , mmeanza tena ! muwe na subira hamjui siasa za nchi hii haina heri
tulia siku ziende ndo utoe sifa bado mapema.

ni sawa ulivyopata Mke ukafunga ndoa , baada ya mwezi ngumi zinapigwa tulia kwanza
 
bila shaka kikwete and co wanajisikia vibaya sana kuona jamaa anavyo wa-prove wrong ktk utendaji wao.nina shaka hao ndio watakuwa wa kwanza kupanga mikakati ya kishetani ya kummaliza.magufuli my president be extra carefully.
 
Umesahau Zile Milion 50 Kwa Kila Kijiji

 

OMG! It is too good to believe that after all sufferings we have a person who believes that he is the president. God bless you dr. Usibadili mwendo ukakutana nawatuhumiwa wa wizi ukasema umewomba warejeshe walichoiba
 
Dk 90 ndo maamuz wa mtanange huu. Hata half time hatujaanza kafika Kati sasa nyie mshaanza kumwaga masifa hakijinga humu
 
Ila hiyo hamishahamisha et atapangiwa kaz nyingine yaleyale.......
 
Jibu hili limekaa vizuri sana. Tatizo la hawa wanaojiita "wapinzani" wanafikiri maana ya upinzani ni kujitoa ufahamu.
Tatizo watu wanashabikia siasa kama wanvyoshabikia mpira. Mtu akishakua yanga basi ni yangu tu milele ndiowanavyofanya siasa, hawaangalii kazi na sera za wanasiasa.
Binafsi nilikua nimeichoka CCM lakini kwa kasi hii ya Mheshimiwa raisi inanipa matumaini. Tunamuomba mungu aje apate wasaidi na mawaziri wema wenye niya nzuri na nchi yetu.
 
Ma-Tanzania sisi majinga sana, mamburura mwanzo mwisho no wonder tunafanya uchaguzi kama tumekatwa vichwa!! Hapa kigeni ni kipi? Waliopita hawakuwahi kufanya haya maigizo? Impact yake ilikuwaje? Hapa hakuna la maana linalofanyika, hebu aende akavunje mikataba mibovu huko kwenye madini na gesi ndo tumwone kweli mwanaume!! Hebu aende Stanbic akapate orodha ya watu waliobeba hela kwenye rumbesa ndo tumwelewe! Hebu afuatlie kujua kwanini home shopping centre imefunga shughuli zake ghafla hapo ndo tutamwelewa! Vinginevyo haya mengine ni maigizo tu kama ya akina Jakaya & Co Ltd.
 
Usemacho ni kweli kabisa.
 
Sipuuzi kinachofanywa na Rais Magufuli, lakini najaribu kuwakumbusha hasa wanandoa wengi ambao walizianza safari za ndoa zao kwa mbwembwe nyingi na bashasha, kwa kulishana keki kwa midomo, kwa kushikana mikono na kutembea pamoja kila pahala n.k., ..., lakini leo ndoa hizo hazitamaniki machoni pao wala machoni pa jamii...!

Ninachosema ni hiki, utukufu wa jambo lolote uko mwisho na sio mwanzo wake. Safari ya miaka mitano IKULU sio lelemama, wacha tuendelea kungoja na kuona mwisho wa safari hii kama utafafana na mwanzo wake, vinginevyo itakuwa ni kama tu 'fungate'...!

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
For sure this is the kind of president we were looking for.Hata tukimtazama usoni tunaona he real mean what he is doing.
 
Magufuli rais wetu inabidi awekewe ulinzi mkubwa na mkali. wako watu wamekaa mkao wa kutaka kuhujumu kila kitu..

Usijali mkuu ulinzi anao wa kutosha kwani hata sisi watanzania tuliotengwa, watanzania kina yahe tuliopigika na ugumu wa maisha, watanzania tunaolitakia mema taifa letu mchana na usiku tunamuombea dua Rais wetu Magufuli, Mungu amlinde ampe afya njema afanye kazi ya kuwatumikia watanzania pasipo kukata tamaa... Amin!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…