Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Sisi wananchi tunajielewa na ni wazalendo tuunganishe nguvu yetu na Rais wetu kujenga Tanzania mpya. Asante Mungu kutupa huyu Rais.. Pamoja na mama yetu suluhu makamu wa Rais... Wapinzani tuungane tupige hatua miaka hii mitano ACHENI siasa za kijinga za kuandamana.. RAIS huyu tuliyenaye ni mkarimu sana na ameamua kujitoA kwa nchi hii..
 
Amejitoa kwa lipi hasa wakati maisha yanazidi kuwa magumu??
 
Mtu mmoja anapoamua kujifariji kwa niaba ya wengi, eti sisi watanzania?! Utani wa ngumi huu.
 
aisee jitahd kutafuta cheo nafas za uteuz bado anazo nying lkn kiukwel hta nafs yko inakusuta kwa ulicho kiandika lkn sio mbaya kujifariji
 
Ngoja nisubiri boat yng ya Bagamoyo ipone nirudi kijijini, huku mjini sipawezi!
 
Huko ulikopita waliongezewa mishahara,walipewa ajira,walipanda madaraja,sukari haijapanda bei,nk
Kama ni hivyo sawa ila kama sio hawajui kuwa wanatawaliwa na dikteta uchwara pia hawajitambui.

Kumwita mkuu wa nchi dictator uchwala mkuu ni kukiuka maadili.....hujui kwamba hao wanaowahaminisha kuvunja ukuta ndio chanzo cha hayoyote unayoyalalamikia....wafanya bihashara na viongozi na wamiliki makampuni ndio hao wakwepa kodi.....usipolipa kodi nchi itajiendeshaje?.....kodi ilipwe kwa ufasaha na hao wavunja ukuta tupate Tanzania mupyaaaa!
 
Kwahiyo Kikwete alifanyaje mbona aliongeza mshahara kila mwezi wa saba,madaraja watu walipanda na ajira zolitolewa.
Kama dikteta uchwara anakulipa pesa ili upotoshe hapa haina maana.
Mimi nimekata tamaa tangu mwezi uliopita natamani chochote kitokee ili ajue kuwa amebugi step.
 
huyu mheshmiwa alipokua anapita kutafuta wadhamini ndani ya chama chao mikoa kadhaa wanaccm walimkimbia ikabidi atumie nguvu ya ziada kuwatafuta. ni watu wachache sana waliowahi kufikiri kua tungewahi kua nae kama rais kinachonishangaza ni kua ameteka mijadala kwenye media zote za tanzania na jambo kubwa kuliko yote ni kua amechukua hoja zote zilizokua zikiwapa kick wapinzani kias kwamba kwa sasa wamekombewa hoja zoote.
 
Uko sawa japokua utatukanwa hapa!
 
Tumpe two more years ndiyo tutajua kama ni kweli .................!!
 
Kipimo cha kubalika ni pamoja Na kuacha wengine wafanye siasa Kama yeye ili tupime hali ikoje? Ukizunguka pekee yako Na kujiambia unakubalika Kuwa makini kiweza Kuwa kiwi ya macho!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…