Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Zikiwa ni Takribani siku 20 tangu aapishwe kushika Madaraka ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mh. Dr. JPM ameteka mijadala takribani katika viunga vyote vya jamhuri ya muungano wa Tanzania kutokana na kasi aliyoanza nayo. "Tunamuunga mkono na atakayemkwamisha atueleze sisi wananchi tuko tayari kupambana ili kumsaidia kusafisha serikali" alisikika mkazi mmoja wa Morogoro, katika viunga vya mwanjelwa Mbeya ambapo JPM aliwahi kukutana na changamoto za vijana wa ukawa mmoja wa vijana katika maeneo hayo alisikika akijutia kwa kutokumuamini JPM wakati akiomba kura "Natamani uchaguzi urudiwe leo nimpe kura yangu, mimi nilijua lazima atafuata ilani ya chama chake tu" alisikika kijana huyo aliyeonakana kutokujua hata maana ya ilani. Katika viunga vya stand ya mabasi nyegezi vikundi vya vijana vimeonekana kuingia hamasa ya kujadili kila jambo ambalo JPM amekuwa akilifanyia maamuzi "afadhali tulimuamini tungechagua wasanii tungekuwa tumeshaanza kujuta" alisikika mmoja wa mama ntilie katika stand hizo. katika utafiti wa jumla niliofanya katika takribani mikoa 28 inaonyesha gumzo kubwa ni namna JPM alivyouanza uongozi wake kwa style ya kipekee huku wengine wakitamani hata asitangaze baraza la mawaziri "Natamani Rais aendelee kuongoza yeye na Makatibu wakuu maana naona mabo yaliyokwama kwa miaka mingi yanaenda" alisikika Profesa mmoja Nguli kutoka chuo kikuu kimoja kikubwa cha umma nchini.
Propaganda nyepesi sana hii, hiyo ni kawaida watu wengi kama si wote kujadili jambo lililoko kwenye vyombo vya habari kwa wakati huo. Kwa mfano leo hii ukienda Kenya watu wengi kama si wote wanajadili habari ya Pope Francis sio kwa sababu ni rais wa Kenya, hapana ni kwa kuwa ndio vyombo vya habari vimempa kipaombele. Hata majuzi tulikuwa tunajadili kuhusu taifa stars na Algeria huku majina ya Samata yakitawala midomoni mwetu na kwenye maeneo mengi nchi. Baada ya 7 bila unaweza kuamini hata hiyo mechi ilikuwepo?