Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Zikiwa ni Takribani siku 20 tangu aapishwe kushika Madaraka ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mh. Dr. JPM ameteka mijadala takribani katika viunga vyote vya jamhuri ya muungano wa Tanzania kutokana na kasi aliyoanza nayo. "Tunamuunga mkono na atakayemkwamisha atueleze sisi wananchi tuko tayari kupambana ili kumsaidia kusafisha serikali" alisikika mkazi mmoja wa Morogoro, katika viunga vya mwanjelwa Mbeya ambapo JPM aliwahi kukutana na changamoto za vijana wa ukawa mmoja wa vijana katika maeneo hayo alisikika akijutia kwa kutokumuamini JPM wakati akiomba kura "Natamani uchaguzi urudiwe leo nimpe kura yangu, mimi nilijua lazima atafuata ilani ya chama chake tu" alisikika kijana huyo aliyeonakana kutokujua hata maana ya ilani. Katika viunga vya stand ya mabasi nyegezi vikundi vya vijana vimeonekana kuingia hamasa ya kujadili kila jambo ambalo JPM amekuwa akilifanyia maamuzi "afadhali tulimuamini tungechagua wasanii tungekuwa tumeshaanza kujuta" alisikika mmoja wa mama ntilie katika stand hizo. katika utafiti wa jumla niliofanya katika takribani mikoa 28 inaonyesha gumzo kubwa ni namna JPM alivyouanza uongozi wake kwa style ya kipekee huku wengine wakitamani hata asitangaze baraza la mawaziri "Natamani Rais aendelee kuongoza yeye na Makatibu wakuu maana naona mabo yaliyokwama kwa miaka mingi yanaenda" alisikika Profesa mmoja Nguli kutoka chuo kikuu kimoja kikubwa cha umma nchini.

Propaganda nyepesi sana hii, hiyo ni kawaida watu wengi kama si wote kujadili jambo lililoko kwenye vyombo vya habari kwa wakati huo. Kwa mfano leo hii ukienda Kenya watu wengi kama si wote wanajadili habari ya Pope Francis sio kwa sababu ni rais wa Kenya, hapana ni kwa kuwa ndio vyombo vya habari vimempa kipaombele. Hata majuzi tulikuwa tunajadili kuhusu taifa stars na Algeria huku majina ya Samata yakitawala midomoni mwetu na kwenye maeneo mengi nchi. Baada ya 7 bila unaweza kuamini hata hiyo mechi ilikuwepo?
 
Ndivyo tulivyo watu wa Tanzania, tunahemkwa sana...
...Kazi bado ni kubwa, tunamuombea Mh. Raisi wetu!!
 
Mie mtaani kwetu raha tupu vitu dukani vimeshuka bei, sokoni nyama bei ni kama bure kwa kweli maisha yamekuwa rahisi sana kweli hii ndio Tanzania tuliyoitaka.
 
Propaganda nyepesi sana hii, hiyo ni kawaida watu wengi kama si wote kujadili jambo lililoko kwenye vyombo vya habari kwa wakati huo. Kwa mfano leo hii ukienda Kenya watu wengi kama si wote wanajadili habari ya Pope Francis sio kwa sababu ni rais wa Kenya, hapana ni kwa kuwa ndio vyombo vya habari vimempa kipaombele. Hata majuzi tulikuwa tunajadili kuhusu taifa stars na Algeria huku majina ya Samata yakitawala midomoni mwetu na kwenye maeneo mengi nchi. Baada ya 7 bila unaweza kuamini hata hiyo mechi ilikuwepo?

Kuna vitu havihitaji propaganda nani asiejua kuwa MAGUFULI ndie habari ya mjini, miminajua watu wenye chuki huwa hawakosi neno
 
Kuna vitu havihitaji propaganda nani asiejua kuwa MAGUFULI ndie habari ya mjini, miminajua watu wenye chuki huwa hawakosi neno

Kwa taarifa yako sina chuki na Magufuli japo sikumpa kura yangu lakini nakubali utendaji wake kwani jambo jema ni faida kwetu wote. Nilichomwambia huyo jamaa hiyo ni propaganda maana jambo lolote linapotangazwa sana na vyombo vya habari ndio inakuwa mjadala na mifano ya Pope na taifa stars nikatoa kujazia hoja yangu.
 
Magufuli ni habari nyingine yaani hizo ni rasharasha tu bado mambo mengi yanakuja kuweni watulivu
 
Ukipata kiongozi mwenye upendo na watu wake mambo ndio uwa hivyo. Asante rais wetu Dkt Magufuli kwa upendo wako kwa Watanzania.
 
Hivi huwa ni habari chungu sana kwa UKAWA, Jamaa anawapa wakati mgumu sana,wanaijahidi kumzuia lakini jamaa hazuilkiki! viva magu viva!!!
 
Go go go mtumbua majipu ambaye hajawahi tokea katika sayari hii ya tanzania!!tumechoka na viongozi wazembe!!tumechoka na huduma mbovu!!tumechoka na ufisadi tufanyie surprise nyingine huko chamwino nasikia upo umejifungia ukikagua cv za wakuu wa mikoa na wilaya
 
Mie mtaani kwetu raha tupu vitu dukani vimeshuka bei, sokoni nyama bei ni kama bure kwa kweli maisha yamekuwa rahisi sana kweli hii ndio Tanzania tuliyoitaka.

wapi huko mama mkubwa nihamie na familia yangu? niko kwenye ngome ya jamaa, bei zimepanda kinyemela na mijamaa ina hasira baada ya watz kufanya uamuzi wa busara. nijuze tafadhali.
 
Amewasoma watanzania & akatumia akili ndogo tu, basi!!! Watu hawataki kusikia tena mambo ya siasa. Watanzania ni kawaida yao, wepesi kusamehe & kusahau! Teh!
 
Propaganda nyepesi sana hii, hiyo ni kawaida watu wengi kama si wote kujadili jambo lililoko kwenye vyombo vya habari kwa wakati huo. Kwa mfano leo hii ukienda Kenya watu wengi kama si wote wanajadili habari ya Pope Francis sio kwa sababu ni rais wa Kenya, hapana ni kwa kuwa ndio vyombo vya habari vimempa kipaombele. Hata majuzi tulikuwa tunajadili kuhusu taifa stars na Algeria huku majina ya Samata yakitawala midomoni mwetu na kwenye maeneo mengi nchi. Baada ya 7 bila unaweza kuamini hata hiyo mechi ilikuwepo?

Hata wakenya wanamjadili Magufuli......wanatamani awe Rais wao
 
Hata wakenya wanamjadili Magufuli......wanatamani awe Rais wao

Wakenya wanatamani Magufuli awe raisi wao?Mwambie wabadilisha Uhuru Kenyata aje tanzania na huyu Magufuli aende kuishi huko kenya kwa sababu siyo chaguo letu .
 
sifa zikizidi kuna siku atakata rufaa kwa kesi ya meli ya samaki jodari tulioshindwa,
 
Magufuli anajadiliwa sana kwa sababu siyo chagua la watanzania ni chaguo la ccm
 
Magufuli anajadiliwa sana kwa sababu siyo chagua la watanzania ni chaguo la ccm
Sio kweli, Jamaa alipigiwa kura na watu wengi waliokuwa neutral...!
Tatizo lenu mnaamini kila mtu anaendeshwa kwa misingi ya vyama..poor you!!
 
Back
Top Bottom