Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

nyie wote mnaomsifia magu mtarudi hapahapa kumkashifu muda si mrefu....maana wabongo huwa hawakumbuki kabisa...jk alipoingia 2005 moto wake ulikuwa ni zaid ya magu,aliweza kukimbiza majambazi kwa chopa...lakini leo kiko wapi?

Vengu,
Hebu Taja mambo walau matatu ya JK unayoyaita moto,unayoweza kuyali nganisha na Mh, magufuli honourable president of the United Republic of Tanzania.?
 
Heshima kwake rais wa nchi nzuri mno JMT,lakini suala la kuvunja katiba yetu hapana ila kuiboresha/kufuata tume ya mzee wa haki Joseph Sinde Warioba.Miaka 10 itatosha kuitendea haki nchi yetu na kuacha njia za kudhibiti wezi hata akimaliza zamu yake.MUNGU umlinde rais wetu JPM na wasaidizi wake waaminifu.
 
1.naona wawekezaji wengi wakifunga makampuni yao na kukimbia nchi

2.naona mzunguko wa pesa ukipungua kwa kasi kikubwa

3.naiona tanzania yenye watumishi wengi wa uma wakiwa na maisha duni

4.naona biashara nyingi zikidoda(manunuzi kupungua)

5.naona watanzania wengi wakikimbilia vijijini baada ya kushindwa kuishi mjini

6.naona ajira kwenye mashirika binafsi zikiwa adimu sana kuliko za serikalini

7.naona shilingi ikiimarika lakini maisha kuwa duni sana

8.naona ongezeko la wizi,makahaba,watoto wa mtaani na mateja

"HIKI NDICHO NINACHOKIONA MIMI...SIO LAZIMA UKUBALIANE NA MIMI"
 
Kuanzia number moja hadi nane umepatia lakini umeandika kwa kinyume.
 
...

...ha ha ha hiyo ndiyo staili ya kifo cha sisiemu mwenye Nyundo aongeze kasi 50 years ???
 
11029987_437216929801093_8441575378133223487_n.jpg
 
Naweza kukukaribia au kufanana nawe umri lakin nakupa shikamoo kwa haki unayotutendea asubuhi na mapema ya utawala wako.Tulipo mshukuru MUNGU kwa kutupa rais kwa kutumia akili zatu na matakwa yake wenzetu wakatukukana sana eti unaigiza nawe wapenda rushwa. Ahsante maana matendo yako yanathibitisha kauli zako. MUNGU uliyemwomba na kujiapiza kwake kuwa utatutumikia akulinde maana ana nguvu kuliko shetani wacha hizo taka taka changa ziitwazo wezi ikiwa ni sehemu ya watumishi wake.

Thibitisha kipindi chote cha utawala wako kwa kuwapa haki hata waliokukataa bila kuwabeba waliojisogeza kwako ili wanufaike.Thibitisha kuwa Tanzania ingali na watu wasafi,haihitaji kuomba omba bali kusaidia maskini wengine.Tukumbushe kula chakula chetu maana wengine wanaona kula mhogo ni ushamba bali "burger" ili tujue wana fedha.

Ahsante MUNGU kusikia kilio chetu.Shukrani kwa MUNGU wangu ni sehemu ya maisha yangu.Tanzania bila wizi na rushwa inawezekana bila msaada wa wazungu.
 
Natamani hao wakazibue chemba za wahindi pale k'koo 9dec
 
Mwandishi Mwingereza aitwaye Lewis Carroll aliwahi kusema, ''If you don't know where you are going, any road will get you there''.

Wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu, tuliwasikia UKAWA wakimponda mgombea Urais wa CCM kama hana lolote kwa sababu CCM ni ile ile. Kuna wengine walidiriki kusema CCM imeishiwa pumzi na iwekwe kando. Wengine wakasema kama CCM ni kitanda chenye kunguni kama Dk. Magufuli anavyosema, basi wao hawataki kuhangaika kuwauwa kunguni bali watakichoma moto na kununua kitanda kingine.

UKAWA walicheka na kumdhihaki Rais Magufuli aliposema amepania/kudhamiria kuleta mabadiliko bora pindi atakapoingia madarakani kwa kubana matumizi ya serikali, kuongeza mapato ya serikali, kuboresha mfumo wa utendaji na ufanisi, kupitia kodi na ushuru unaowaumiza wakulima, wafugaji na wavuvi, kupitia upya baadhi ya sheria zinazoleta kero kubwa kwa wananchi, kuunda serikali ndogo, kupunguza au kumaliza kero za watumishi wa umma na kupendekeza muundo wa kitaasisi ili kutekeleza kwa ufanisi ahadi zake.

Two weeks down the line, UKAWA kwa sasa wameanza ''kudandia treni'' ya Rais Magufuli kwa mbele wakati huo huo baadhi yao hawajatuambia kama wanamtambua ni Rais wa Tanzania.

Eti wanadai wameanza kumkubali Rais Magufuli kwa sababu ameanza kutimiza Ilani ya UKAWA! Wamesahau ni wiki mbili zilizopita walikuwa wanasema Rais Magufuli hana lolote jipya katika mchango wa mabadiliko bora nchini. Kuna wengine kwa sasa watadai Rais Magufuli ni UKAWA. Wanachofanya kwa sasa ni kutaka kuhalalisha hii dhana ya kuitwa nyumbu na bendera fuata upepo!

Kabla ya viongozi wa UKAWA kuanza 'kudandia treni' ya Rais Magufuli kwa mbele, lazima wawaombe radhi Watanzania kwa kutaka kuliangamiza taifa kupitia mgombea wao wa Urais wa Tanzania ambaye walituletea na kuanza kutuuzia kwenye gunia wakati wanafahamu ni mra rushwa, fisadi na hafai kuwa Rais wa Tanzania.

Mtu muungwana ni yule anayeomba radhi na pia taifa la waungwana ni lile linalosamehe baada ya kuombwa radhi.

UKAWA kabla hamjaungana na juhudi za Rais Magufuli, lazima muombe radhi kwa wapiga kura wengi, otherwise, endeleeni kusimama na Lowassa mwenye mabadiliko fake yakisaidiwa na Ilani yake ya Uchaguzi yenye vipao mbele vitatu, 1)Elimu, 2)Elimu na 3)Elimu.

Kwa wale wanaoamini uwepo wa Mwenyezi Mungu, kwa sasa wanasema Mwenyezi Mungu bado analipenda Taifa letu kwa kutuletea Rais Magufuli.

mtoa mada ww ni mjinga,mtu akifanya vzr lazima asifiwe na akifanya hovyo alaumiwe kanuni ni hiyo pekee.unataka Ukawa wafanye nn,a cha ukihiyo.
 
Bado sana...tunataka kuona vision ya uchumi kukua. Atawafanya nini wazungu walogawawa migodi bure
 
nyinyi subirini mtakuja sikia hayo makontena ya akina nani isije yakawa yamo na akina fododo
 
mtoa mada ww ni mjinga,mtu akifanya vzr lazima asifiwe na akifanya hovyo alaumiwe kanuni ni hiyo pekee.unataka Ukawa wafanye nn,a cha ukihiyo.
Nadhani wajinga ni wale wametuambia hawamtambui Rais Magufuli halafu wanaingia bungeni kupiga kura ya kumthibitisha Waziri Mkuu, Majaliwa aliyeteuliwa na Rais ambaye hawamtambui kama Rais wa Tanzania.
 
12316391_190132944662235_6283833739405433416_n.jpg

Mtetezi na Mkombozi wa Watanzania..Kiongozi mwenye Hofu ya Mungu..Kiongozi Mwenye Nia ya Kuileta mabadiliko. Rais John Magufuli.
 
sasa u unakataa kuwa magufuli hafanyi walichotaka UKAWA?
 
Back
Top Bottom