Invisble275
JF-Expert Member
- Nov 28, 2014
- 982
- 1,166
Rais wetu apewe ulinzi mkubwa. Wazalendo wa kweli wa nchi hii wanataka maendeleo ya kweli. Wanataka uozo uliopo katika jamii yetu utokomezwe kwa kasi. Viongozi wamekuwa kama miungu watu. Wezi ndio wanapewa nafasi katika taasisi zetu. Waadilifu katika nchi hii ni kama hawatakiwi. Wahuni tu wanapewa madaraka makubwa kwa kujipendekeza kwa viongozi. CCM kumeoza kwa sababu ya kubebana. Serikali nako kumeoza kwa kuwa CCM kumeoza. Taasisi za CCM zimeoza hazina viongozi wa maana wamejaa wababaishaji. Taasisi za serikali nazo zimeoza kwakuwa wanawekwa watu wasio na uwezo. Asilimia 90 ya wakuu wa wilaya hawana uwezo. Uozo uko pia kwenye halmashauri. Halmashauri zimekuwa kitovu cha ulaji. Nchi hii ni lazima ikombolewe kutoka kwa viongozi mafisadi. CCM ijisafishe na serikali nayo isafishwe.
Umenigusa sana mkuu.
Yaani mimi nitaendelea kumchukia kikwete mpaka anaenda kuzimu. Kikwete alishatuharibia nchi. Taasisi nyingi za serikali kuko hovy hovyo tu. Hii ni kwa sababu ya kuendekeza ushikaji. Pia Kikwete alikuwa na ki-element cha udini (najua wengi watapinga lakini wanaomjua kikwete watakubaliana nami). Yaani viongozi wengi wa taasisi za umma walishajiona miungu watu na kama vile wao wana hati milki na taasisi hizo. wengi wao wahana uwezo kabisa, kazi iliyokuwepo ni kuiba tu pesa za walala hoi bila kuogopa chochote. Mungu atamlinda Magufuli ili atukomboe wanyonge.