Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Mafanikio ya Rais Magufuli: Viva Rais Magufuli, viva Tanzania

Jamani wanajamvi kweli ktk hili nampongeza sana Dkt magu kwa kutunyima kunywa pombe mchana siku za kazi, mbali ya kuwafanya watu kubuni vishughuli vya kufanya lakini pia imerejesha watu wengi karibu na family zao, pia tumeweza hata kuwa na nidhamu na vipato vyetu ambavyo ni vidogo na baadhi ya wababa walikuwa hawachangii pato la family.
Pombe ilikuwa inaongeza hata viwango vya rushwa, umalaya so pengine hata maambukizi ya ukimwi yatapungua VIVA MAGU
 
Angalia na upande wa pili kwamba mzunguko wa fedha nao unapungua na mapato ya serikali nayo yanashuka.
 
Mlevi ni mlevi tuuu!! Akinywa from saa 9 jioni hadi 9 alfajiri, ataamka kweli afanye kazi kama siyo kuamka saa 6 aoge, arudi bar, akule, akimaliza tayari saa 9?
 
Kufika November mwaka huu lazima akusanye kodi za kina mkapa billion 300 enzi zile hata bado twavaa tairi za magari miguuni - katambuga nadhani. Hapo ndiyo lazima tutuie akili, lazma tukae. Hata ushoga utakuwa umetamalaki mara maana hamna namna sasa
 
Akina J Delicious watsongezeka.
Kufika November mwaka huu lazima akusanye kodi za kina mkapa billion 300 enzi zile hata bado twavaa tairi za magari miguuni - katambuga nadhani. Hapo ndiyo lazima tutuie akili, lazma tukae. Hata ushoga utakuwa umetamalaki mara maana hamna namna sasa
 
Nimekusoma ngoja nirudi kwa Jessica Magufuli! Bye bye!!
 
WAKATI wa kampeni, baadhi ya Watanzania walikuwa wakibeza kila mwanasiasa anayetokea CCM na kwa dhana hiyo hiyo walikuwa wakimbeza pia John Magufuli.

Waliona kwamba hana uwezo wa kuongoza nchi na au atakuwa mtu wa kuendeleza baadhi ya mambo ambayo Watanzania kwa muda mrefu wamekuwa wakiyapigia kelele, hususani ufisadi. Lakini sasa wanaanza kuona aibu na wengi wao wamekwishaanza kumuunga mkono japo kimya kimya. Hii ni kwa sababu sasa Magufuli anaonesha mabadiliko ya kweli na siyo yale ya ‘kuzungusha mikono waliyokuwa wanayafikiria waliokuwa wakiunga mkono kambi ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Wengi wao, wameanza kuamini kuwa Taifa lilikuwa linamhitaji kiongozi kama Magufuli kuweza kulinasua mahali lilipo kuliko kiongozi yule mwingine toka upinzani. Hatua zake mbalimbali za mwanzo kushughulikia; kubana matumizi, kupambana na ufisadi na kuondoa watendaji mizigo (majipu) kumewafanya waamini kabisa kuwa Magufuli kazi aliyonayo akiendelea na kasi hiyo basi ndani ya mwaka huu mmoja tu atakuwa ameleta heshima katika utumishi wa umma. Siyo hivyo tu bali pia alikuwa amerejesha heshima kwa Watanzania na fahari ya taifa letu.

Sasa bila shaka kwamba wanaamini kabisa kuwa Magufuli anafanya kazi hii bila woga, huruma, husuda, wivu au kusitasita. Kwamba, hatomwangalia yeyote, popote na kwa lolote. Ndani ya miezi sita hii na ujio wa bajeti ya kwanza ya serikali yakeghakuna shaka kwamba Magufuli ameweka alama za namna gani taifa linataka kwenda na kila kiongozi atakuwa amepata ujumbe. Waliombeza walifanya makosa kwa sababu walidhani hii ni kazi rahisi kwa Rais.

Walidhani ni kazi ya kutimua huyu, kuondoa yule na kumleta yule mwingine. Walidhani ni kazi ambayo akimaliza teuzi mbalimbali basi atakuwa ameipanga serikali yake kwa ajili ya kuchapa kazi. Sasa wanajua kuwa uamuzi wake wa kushughulika na watu kwanza kabla ya mfumo ni jambo muhimu sana. Ulikuwa ni uamuzi sahihi na unahitaji kuungwa mkono na kutetewa.

Watu ndio hutengeneza mfumo; ni watu ndio ambao hukaa chini na kufanya maamuzi mbalimbali yenye kuathiri (kwa uzuri au ubaya) uwepo na utendaji wa mfumo wa utawala. Ukiwa na watu wabovu, wabinafsi na wenye mwelekeo wa ufisadi basi mfumo utakuwa mbovu, wa kibinafsi na wenye uelekeo wa kifisadi kwa sababu moja kubwa; wale wenye kuiwamba ngoma ngozi huivutia kwao! Matobo (si matundu) kwenye sheria zetu yalitengenezwa na watu ambao walijua wakiziba na wao watakuwa wamejizibia.

Magufuli asingeweza kutengeneza mfumo mwingine kwa kutumia watu wale wale walioutengeneza mfumo huu wa sasa na hasa kama watu hao ni wanufaika wa mfumo huu. Ingelikuwa ni sawa sawa na kumtaka Rais awalazimishe watu wakate matawi ambayo wamekalia huku wakijua kwa kufanya hivyo wataangukia mtoni kwenye mamba wengi. Hakukuwa na jinsi na bado hakuna jinsi. Ni lazima kuwaondoa hawa na kuwashughulikia ili kuleta watu wenye fikra zinazoakisi mwelekeo wa serikali yake.

Ni kwa sababu hiyo, kumbe kazi ile ya miezi sita kwa kweli haiwezekani. Ni kazi ambayo inapaswa kuwa endelevu na yenye matokeo bora. Tayari tumeanza kuona dalili za yaliyomo ndani ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu (CAG) na tayari inatisha kama ilivyotisha kwa miaka kadhaa. Kwa muda mrefu tumekuwa tukijulishwa juu ya uchafu wa watendaji wetu na taasisi zetu na mara karibu hizo zote tumekuwa tukionesha kushtushwa na kusikitishwa tukiamini kuwa labda mwaka unaofuatia mambo yatakuwa tofauti.

CAG aliyepita alikuwa anarudia baadhi ya hoja mwaka baada ya mwaka na wakati mwingine kuhusiana na taasisi au watu wale wale. Na safari hii tusije kushangaa kuwa hata CAG wa sasa anaweza kujikuta amegusa maeneo yale yale; matumizi mabaya ya sheria ya manunuzi ya umma, fedha kutumiwa bila maelezo, kutopatikana kwa vitabu vya masuala ya fedha wakati wa ukaguzi, na upotevu wa fedha za umma kwa namna ambayo inadokeza tu kuwa zimeliwa.

Magufuli basi ana kazi kubwa; kushughulikia viongozi wabadhirifu, wazembe, wezi na wenye kutumia madaraka yao vibaya na wakati huo huo kupanga na kusimamia serikali yake huku akiunda upya mfumo uliojaribiwa na kuharibiwa. Kwa mwendo alioanza nao hakuna shaka yoyote jambo moja lilikuwa sahihi kwa upande wangu; kuunga mkono mabadiliko haya. Wapo wanadhani hali ni ngumu sasa na kuwa serikali inabana, naamini bado hatujaona hasa ugumu kwani hadi hivi sasa bado serikali inahangaika na madudu ya nyuma na yanatisha.

Kusahihisha uchumi (correcting an economy) ambao umejengwa na kusimamiwa na utamaduni wa kifisadi (corrupt culture) haiwezekani kuwa ni jambo jepesi. Ni kwa sababu hiyo sasa mimi na wengine wenye mawazo kama mimi tuamini yafuatayo: Mosi, kuanza kazi kwa mahakama za kushughulikia ufisadi na uhujumu uchumi kunahitajika mara moja.

Pili, sheria ya CAG ifanyiwe mabadiliko mapema zaidi ili CAG awe na madaraka ya kutoa agizo la kusimamishwa kazi na hata kufikishwa mahakamani kwa mtendaji yeyote wa umma ambaye uchunguzi wake (CAG) unaonesha kuwa kuna uvunjaji wa sheria. Ikiwezekana ofisi ya CAG iwe na waendesha mashtaka wake kama ilivyo kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (Takukuru). Haipaswi madudu ya mwaka mzima yanasubiri mwaka mwingine kujulikana.

CAG anapofanya ukaguzi na kukuta madudu na ushahidi wa kisayansi upo (forensic evidence) basi hatua zichukuliwe mara moja. Siyo awe na uwezo wa kupeleka mashtaka lakini kwa kupendekeza kwa DPP. Ikiwezekana, kutegemea ushahidi alio nao, watuhumiwa watiwe mbaroni, mali zao zinazohisiwa kupatikana kwa njia haramu zikamatwe ili zije kufilisiwa wakikutwa na hatia mahakamani.

Ni wazi pia, kutokana na kazi hii ngumu ambayo tunaamini Magufuli anaiweza kutakuwepo na wasema ‘hapana’ na waleta ‘vikwazo.’ Wale ambao wataona maslahi yao yanaguswa na kuwa pale walipokuwa wakihemea sasa panaanza kuondolewa. Watakuwepo watu ambao watajaribu kudhulumu na kuharibu jitihada hizi; raia wa kawaida, watendaji serikalini, wabunge na tusije kushangaa hata watu wake wa karibu!

La maana ni kukaza mwendo na kuendelea kusafisha serikali, kuleta uwajibikaji, na nidhamu ili hatimaye ujenzi mpya (Reconstruction) wa taifa letu uanze tena kwani pale tulipoacha kulijenga tulianza kulibomoa. Hizi ni zama mpya, zama za ujenzi mpya wa taifa letu. Katika hili, naamini nipo sahihi na bado naendelea kuwa sahihi. Magufuli ni kiongozi wa zama hizi.
 
Akiweza kumtumbua jesca ,billion 256 hewa za wizara ya ujenzi,nyumba za serikali na kivuko chakavu cha bagamoyo na lugumi kweli baba jesca tutaamn hayo unayoyasema.Kwasasa hatuna kiongozi mwenye maono nchi inakwenda kuzama hii
 
Binafsi nimefurahishwa na kasi ya Dkt. Magufuli. Naamini wapo pia wengi wanaoungana nami katika furaha hii. Magufuli ameanza kwa kasi ambayo kama ataimaintain, Tanzania haimalizi miaka mitano itakuwa tayari ni nchi yenye kipato cha kati.

Hata hivyo wapo baadhi yetu ambao wanakejeli kasi hiyo. Hao kwangu ni watu waliozoea ubwete na bora liende!. Wanamwona Magufuli kuwa ni mtu atakayekuwa kauzibe kwao!

Wapigaji wote, wavivu wote na wazee Wa madili wote watamchukia Magufuli ila mi niseme na niwaombe tu kwamba tumpe support huyu jamaa kiukweli atatufikisha mahali Fulani!

Tuwafichue wote wanapanga kumhujumu (najua wanajulikana), tuwakatae kwani hawana nia njema na taifa letu.
ahahaha,miezi saba,kesha anza kuomba poo!
Miaka mi5 ni mingi mno, hiyo kasi ya sasa ni moto wa kifuu.
naona ulisema na ukaweka msisitizo!nashukuru!
Tumechoka dharau kutoka kwa vijinchi vidogovidigo mh. Raisi turudishe kwenye chati ya Afrika turudishe heshima we are big nation.
ahahaha,heshima ipi mkuu,ya sukari ya bure!
Naogopa wasije wakamdedisha
amdedishe nani?
Magufuli rais wetu inabidi awekewe ulinzi mkubwa na mkali. wako watu wamekaa mkao wa kutaka kuhujumu kila kitu..
ahahaha
 
Wewe ni raisi bora kuwahi kutokea katika nchi yangu...Una nia ya dhati kabisa ya kuikomboa nchi hii...Hongerra sana mheshimiwa na ninakuomba usisikilize maneno ya wapinzani kwani si WAZALENDO...Wewe ni mzalendo na unayechukizwa na umasikini wa watanzania...Hili umedhihirisha katika speech zako nyingi sana...Kuna maneno wanayoyasema wapinzani kuwa wewe unakurupuka na hutaki ushauri wa watu...Mimi siamini kama ni kweli...Na hata ukiangalia maneno yao utaona dhahiri kuwa ni uwongo, chuki na ukosefu wa uzalendo...

Mfano wanakuponda kuhusu kutumbua majipu. Umekuwa ukiwafukuza kazi watumishi wasio waaminifu na kuwaadhirisha mbele za watu...Mimi sioni kama unakurupuka mkuu...Maana hata yule marehemu uliyemtumbua siku ya uzinduzi wa daraja pia ni jambo lililofanyika baada ya uchunguzi wa kina na kufanyia tafiti taarifa ulizopewa na mheshimiwa makonda...Iweje leo waseme umekurupuka?

Pia wanakuponda ulipowaambia majaji wamalize kesi mapema na serikali ikishinda katika pesa itakayopatikana utawagaia walipane madeni yao...Wapinzani waliokosa uzalendo wanasema eti hii ni rushwa..Eti unawashawishi ili watoe hukumu kuipendelea serikali..Ni wajinga kiasi gani?...Wanashindwa kutambua kuwa serikali inahitaji pesa za kutosha ili kuboresha maisha ya watanzania masikini...Mimi sioni kama kauli ile itamshawishi jaji aipe ushindi serikali ili naye alipwe madeni yake...Maana asipotoa hukumu kwa haki najua lazma utamtumbua tu mheshimiwa..

Pia wanazungumzia suala la ada elekezi kwa shule binafsi...Pia wanasema ulikurupuka...Sisi wazalendo tulishinda mitandaoni kutetea msimamo huu...Maana ada za shule binafsi ni kubwa sana na watoto wa masikini wanashindwa kusoma...Tulitetea kwa nguvu zote...Lakini mpaka sasa naona umelikalia kimya...Sijui tatizo ni nini lakini nna uhakika kuna watu wanakuhujumu tu....Sisi tutaendelea kukuombea mheshimiwa...

Wengine wanakuponda kuhusu suala maarufu la sukari...Hawa hawana uzalendo hata kidogo..Japo sina uhakika sana kama lengo lako lilikuwa ni kuboresha uzalishaji wa viwanda vya ndani AU ilikuwa ni kuwazuia wanaoingiza sukari zailizoexpire kutoka brazil na kuwasababishia watu wengi magonjwa na kulazwa mahospitalini...Ulikuwa na nia nzuri sana mheshimiwa...Na hata sukari uliyoagiza na kusema itauzwa kwa bei elekezi ya shilingi 1800 nnna uhakika baadhi ya watumishi hewa wameiiba pale bandari..Tunakuombea uwapate na kuwatumbua pia mheshimiwa..

Walikusema pia kuhusu kuzuia bunge live...Lengo lako kubwa lilikuwa ni kupunguza matumizi ya serikali...Halafu wakajitokeza wambea kujifanya eti wao watagharamia zoezi hilo la bunge live...Ulinifurahisha mkuu ulipotumia busara zako na kuwaambia kuwa tukionesha bunge live watakuwa hawafanyi kazi,...Kutwa watashinda kuangalia bunge tu...Hahahah...Wewe una akili sana mheshimiwa...Maana hata wale wakulima wanaolima na redio pembeni wakisikiliza bunge walikuwa hawalimi kwa ufanisi, wengi wanaofanya kazi madukani na television pembeni inayoonesha bunge live walikuwa wakiibiwa na kuharibu hesabu...Inabidi wafane kazi...Na wakijifanya wanaijibu hoja hii we kaa kimya tu mheshimiwa wala usiwajibu..Tutatafuta tukio kubwa litakalowaondoa katika kujadili jambo hili...

Juzi hapa pia wameanza kukusema kuhusu kuwaita wale vilaza wa UDOM kwa jina wanalostahili...VILAZA...Wanasema eti kauli zako zinapingana na waziri wako...Eti wanauliza je wakipatikana wanafunzi wasio na sifa waziri wako utamtumbua kwa kusema uongo kama yule mama wa shinyanga?...Na wanauliza kama wasipopatikana wasio na sifa wewe utajitumbua?...Achana nao hawa mheshimiwa wala usiwajibu...Jifanye hujaskia lolote...Ikiwezekana we kanusha tu kuwa hujawahi kuwaita vilaza wala hujawahi kualikwa UDSM hata siku moja...Sisi tupo kwenye mitandao tutakutetea na litapita tu hili...

Kuhusu matrafiki kutoa magari matairi na kuyauza pia nalo wanafanya ni jambo la kujadili...Hawana uzalendo hata kidogo hawa...Pia hili usilijibu....Na baada ya kuuza matairi yao wakiwa hawakomi tuwapige risasi tu mheshimiwa..Hamna namna...

Wanajifanya pia wakushangaa eti uliposema barabara hewa wakati wewe ndiye uliyekuwa waziri wa husika...Hawajui kuwa ulimi hauna mfupa...

Wapo wachache wanaoliponda baraza lako la mawaziri...Eti ulitumia muda mwingi kuliunda lakini hakuna tija yoyote...Achana nao hawa...Ina maana hawajaona yule aliyemshighulikia dr Mwaka na kumwambia Gardner amuombe msahama Jide Jay Dee...Hawaoni mafanikio haya...Hawaoni jinsi ulivyomtumbua yule mmoja kwa ulevi..Hawa wapinzani kila kitu ni kupinga tu.....

Teuzi zako nyingi wanazipinga bila kujali kuwa watu wanafanya kazi nzito...Mpaka kufikia hatua ya watumishi waliotukuka kuvaa mavazi ya mgambo ili mradi tu kwenda sambamba na kasi ya serikali yako...

Mimi nakupongeza sana mheshimiwa na nakuomba usiwasikilize hawa waliokosa uzalendo...HAPA KASI TU
 
Kanisa limeungana na watanzania wengi wenye uzalendo kumpongeza Magufuli katika kazi zake hasa za kupambana na ufisadi
 
Back
Top Bottom