Wana jf.
Salaam,
Mh Dr John Joseph Pombe Magufuli, wewe ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kutumia madaraka yako ya kikatiba, Mh John pombe Magufuli ninakutunuku sifa za kuwa Rais bora wa Mwaka 2016,
Kutokana na mtindo wa uongozi wako wewe Mh Rais Dr John Pombe Joseph Magufuli maarufu JPM hasa katika kudhibiti matumizi ya serikali,kuboresha na kuimarisha nidhamu ya utendaji kwa watumishi wa umma na kudhibiti rushwa, ni wazi kabisa aina yake ya uongozi haijawahi kutokea kwa dhati ilivyo, mataifa mengi duniani yameanza kuiga mfano Nigeria nao wameanza kuhakiki watumishi hewa na jumla ya wafanyakazi hewa 24000 wamegundulika kati ya mwezi August na september,
Aidha nchini Rwanda wameanza kuangalia na kudhibiti safari za nje, pia nje ya Africa amepata pongezi kwa ubunifu huo wa aina yake ni dhahiri kwamba yeye ndio kinara katika mitindo hiyo hapana shaka ndiye Rais wa karne.